Papa yuko karibu na waathirika wa mafuriko huko Mexico
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa bwana, Baba Mtakatifu leo XIV, Dominika tarehe 26 Oktoba 2025, akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, alieleza ukaribu wake kwa upendo wa “Watu wa Mashariki mwa Mexico walioathiriwa na mafuriko katika siku za hivi karibuni,” Baba Mtakatifu anaomba, “kwa ajili ya familia na wote wanaoteseka kutokana na janga hili,” na kwamba “ninamkabidhi Bwana, kupitia maombezi ya Bikira Mtakatifu, roho za marehemu.”
Papa Leo kadhalika alisema, “Ombi letu la amani linaendelea bila kukoma, hasa kupitia kusali kwetu pamoja wa Rozari Takatifu. Tukitafakari mafumbo ya Kristo pamoja na Bikira Maria, tunayafanya kuwa mateso yetu na tumaini la watoto, mama, baba, na wazee walioathiriwa na vita...”
Na kutokana na maombezi haya ya dhati, Papa aliongeza “ inakuja ishara nyingi za upendo wa kiinjili, ukaribu halisi, na mshikamano... Na kwa wale wote ambao, kila siku, kwa uvumilivu wa kujiamini, huendeleza ahadi hii, ninarudia: "Heri wapatanishi"!
Salamu
Papa akiwageukia mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro alisema “Nawasalimu nyote, Waroma na mahujaji kutoka Italia na kutoka sehemu nyingi za dunia, hasa wale kutoka Logroño, Hispania, Mtakatifu Petro ya Paraguay, Recreio (Brazil), na Wacuba wanaoishi Ulaya.
Pia aliwasalimu waamini wa Ginosa, Genova, Corato, Fornovo Mtakatifu Giovanni kutoka Milano, Mtakatifu Giovanni Ilarione, Porto Legnago, vijana wa Scicli, wa Kipaimara wa Jimbo la Saluzzo, Masista wa Moyo Mtakatifu, wakisherehekea miaka 150 ya kuanzishwa kwao, kikundi cha Umoja na Ukombozi (CL)cha Pavia, na Kwaya ya Polyphonic ya Milazzo. Asanteni nyote! Dominika Njema, alihitimisha.
