Papa,Taasisi ya Kipapa ya Kireno:Ndani ya Moyo wa Yesu kuhani ajifananishe mchungaji mwema
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo, tarehe 20 Oktoba 2025, alikutana na Jumuiya ya Taasisi ya Kipapa la Kireno iliyoko Roma. Katika hotuba yake alianza na salamu kwa Kardinali, Askofu, Gambera na Mapadre Walezi na kaka na baadhi ya Masista aliowaona na kuwa na furaha ya kuwakaribisha katika siku ambayo miaka 125 ilizaliwa Taasisi ya Kipapa la Kireno. Kiukweli, Papa Leo XII kwa kuhuishwa na wema wa kiroho ambao Maaskofu wa Ureno na kwa malezi Roma ambayo kwa hakika Uklero, walikuwa wakitazamia kwa ajili ya maijimbo yao, alianzisha katika hilo mchakato wa ambao ulikuwa nafasi muhimu sana. Kwa kutazama nyuma kwa hiyo na kufikia msingi wa Taasisi yao, Papa alisema tunapata kwa pamoja Wakleri na Walei, wameungana katika safari ya pamoja, kwa jitihada zilezile za lengo, ili kuweza kusaidia vema tangazo la njili.
Mtindo wa Kanisa uwe wa kisinodi
Siku zote likizingatia utume, Kanisa, linaloitwa leo kuimarisha mtindo wake wa sinodi, linathamini kwa furaha mang’amuzi haya ya kikanisa na, katika kuyahifadhi kama urithi wa kiroho, linapata ndani yake msukumo wa kukuza Umoja. Wakati, kwa ajili ya maendeleo ya kibinadamu na utukufu wa Mungu, tunaposikilizana na kuheshimu kile ambacho Roho Mtakatifu huvuvia katika kila mwamini, tunatambua ishara za nyakati kwa uwazi zaidi na ujasiri, tukifanya kazi pamoja kujenga Ufalme wa Kristo. Na kuwa Roma ili kukuza somo letu la theolojia au sayansi ya kibinadamu na kijamii kunamaanisha kuzidi kufanya ustadi wa kusikiliza, ambao ni muhimu sana kwa umoja wetu sisi wanafunzi wa Bwana.
Kuanzishwa kwa chuo cha Kipapa cha Kireno Roma
Kuanzishwa kwa Chuo, hasa wakati wa Jubilei ya 1900, Papa alisema kumemruhusu kutafakari na wao juu ya pande mbili za kukaa kwao Roma, ambayo Miaka Mitakatifu inakumbusha sana: mwelekeo wa umoja wa Kanisa na ule wa huruma ya Mungu. Jubilei huturuhusu kushuhudia ujio wa mahujaji wengi sana, na hivyo kuongeza uelewa wetu wa umoja wa Kanisa, unaoupata katika mji huu kwa njia mbalimbali, kwa kushiriki uzuri wa tamaduni zao na kwa kushuhudia utajiri wa Makanisa yao ya mahali pamoja na uzoefu wa kichungaji unaofika nao. Kupitia haya yote ni zawadi kutoka kwa Bwana, na njia bora ya kumshukuru ni kuingia, bila hofu, katika uhai wa kubadilishana hii, kuchangia umoja katika ushirika. Na zaidi tunajua, miaka ya kijubilei ni uwezekano kwa ajili ya kupata dhamiri ya kina zaidi zawadi ya huruma ambayo inabubujika katika moyo wa Yesu. Na ndiyo hiyo Moyo Mtakatifu wa Yesu ambao unatufundisha tangu mwanzo wa historia ya Taasisi ya Kipapa, inaonekana wazi hata kwa Moto wake. Kwake yeye kiukweli wanafunzi wamewekwa wakfu kwake. Papa ameomba waendeel kufanya hivyo. Kuendelea kukabidhi maisha yao kwa Moyo wa Bwana; kumkaribia zaidi duma yeye na kujifunza kutoka kwake Huruma.
Chuo kimewekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu
Chuo kilichowekwa wakfu kwa Moyo wa Yesu ni shule ya huruma ya Mungu, ambapo wanafunzi, wakimwiga mfuasi mpendwa (rej. Yh 13:25), husikia mapigo ya moyo wa upendo wa Mungu na hivyo kuwa wataalimungu wa kweli. Kwa hakika, kuhani, hata utume wowote aliokabidhiwa, daima anapata ndani yake fursa ya kujifananisha na Mchungaji Mwema: hahitaji moyo wa nyama tu, moyo wa kibinadamu na wa hekima, bali pia moyo kama ule wa Yesu, ambao daima umeunganishwa na Baba, wenye shauku juu ya Kanisa, na wenye huruma nyingi. Kukaa mbele ya uwepo wa Bwana baada ya siku za kazi zinazohitaji sana, unaweza kupata ndani Yake burudisho na "kutengeneza" umoja wa maisha. Daima muombe moyo wenye uwezo wa kulipenda Kanisa kama alivyolipenda, ambaye “alijitoa nafsi yake kwa ajili yake” (Ef 5:25); wawasilisha kwake Maaskofu wao na jumuiya zao za majimbo, na kuanzia sasa na kuendelea, waombee waamini watakaowatumikia katika nchi zao. Papa aliwaomba washikilie Bwana Yesu kwa kulisikiliza Neno lake, katika kuadhimisha Sakramenti, hasa Ekaristi, katika kuabudu, katika utambuzi wa rohoni, na katika wema wa kidugu kati yao.
"Jijengee hali ya nyumbani Roma"
Papa Leo XIV amewaomba kwamba wakiwa Roma, wajijengee "nyumba," hali ya kinyumbani ambapo, wakirudi kutoka katika majukumu yenu ya kielimu, mnaweza kujisikia uko nyumbani. Ningependa kukumbuka hapa kile ambacho Mtakatifu Paulo VI aliwaambia wanafunzi wa Collegio San Pietro: "Nyumba hii ni nini?" Aliuliza. "Tunawezaje kukifafanua Chuo hiki? Labda si rahisi kusema. Sio hoteli, ambapo wageni huingia na wageni hutoka; sio nyumba ya bweni rahisi, ambapo makaazi hupatikana kwa madhumuni mengine, ambayo haiwezi kufuata. […] Ni jambo la karibu zaidi na la kibinafsi zaidi. Ni Chuo kinachotaka kuzalisha umoja, yaani, ushirika, urafiki, muunganiko wa roho, ulioanza hapa na kufurahia umoja; na kisha kukumbukwa na kufufuliwa, katika miaka ijayo, mtakapotawanywa ulimwenguni kote, katika Ukatoliki” (Hotuba kwa Chuo cha Mtakatifu Petro Mtume kwenye Janiculum, Januari 6, 1970).
Shukrani kwa masista wanaotoa huduma katika Taasisi hiyo
Tunaona haya yameandikwa katika historia ya Chuo, ambacho kilipokea jina la "Nyumba ya Uhai" kwa sababu ya kuwakaribisha Wayahudi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia. Kichwa hiki ni urithi na wajibu katika ujenzi wako wa kila siku wa udugu. Ili kufikia, Papa amewaomba wafanya kazi pamoja, na kumsaidia Gambera na Mapadre Walezi, na hata kwa uwepo wa Masista Wafransikani wa mama Yetu wa Ushindi. Amewashukuru masisita hao kwa kujitoa kwa ajili ya mapadre, kwa ajili ya sala ambazo wanaziinua Mbinguni kwa ajili yao na kwa ajili ya tabia ya kimama. Ukaribu wa kimama kiroho hakuna ambaye anaweza kuubadilisha na wao kwa kuutoa na kuwa makini kwa miaka hamsini, licha ya unyeti, haukujifishwa kwa Mungu. Papa amewashukuru wa ona hata wahuumu ambao wanatimisha familia ya Taasisi hiyo. Kwa kuhitimisha, kuomba sala kwa ajili ya wote. Wakati wa mwezi huu,kusali Rozari, Papa aliombea kwa maombezi ya Mama Maria wa Fatima, hta kwa ajili yake , kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya Amani. Mungu awabariki.
