Watakatifu wapya 7:Papa Leo XIV,Sala ya Kanisa inatukumbusha Mungu anatenda haki kwa wote

Papa atangaza Watakatifu 7 katika siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 99 ya Kimisonari:“Waamini hawa rafiki wa Yesu ni Mashahidi kwa ajili ya Imani yao,kama Askofu Ignazio Choukrallah Maloyan na Katekista Pietro To Rot;Ni wainjilishaji na wamisionari kama Sr Maria Troncatti;ni wenye karama waanzilishi kama Sr Vincenza Maria Poloni na Sr Carmen Rendiles Martínez;wale wenye moyo unaowaka kwa ibada na wafadhili wa ubinadamu kama vile Bartolo Longo na José Gregorio Hernández Cisneros.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mbele ya waamini kutoka ulimwenguni kote, waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro karibu 55,000, katika Siku ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Dominika ya 99 ya Kimisionari Ulimwenguni katika Mwaka wa Jubilei ya 2025, Baba Mtakatifu amewatakangaza Watakatfu 7 wa Kanisa. Mara baada ya kusomwa masomo yote, Baba Mtakatifu alianza mahubiri yake akisema kuwa Wapendwa kaka na dada, swali linalofunga Injili iliyotangazwa punde linafungua tafakari yetu: “Je atakapokuja Mwana wa Adamu! atakuta imani duniani?(Lk 18,8). Swali hilo linatuonesha kile ambacho ni chenye thamani machoni mwa Bwana: Imani, yaani uhusiano wa upendo kati ya Mungu na binadamu. Na hasa leo hii, mbele yetu wapo mashuhuda saba, watakatifu wapya wa kike na kiumbe ambao kwa neema ya Mungu waliacha taa zao zinawaka za imani, na zaidi wamekuwa wao wenyewe taa zenye uwezo wa kueneza mwanga wa Kristo.

Misa ya Papa Leo kutangazwa Watakatifu
Misa ya Papa Leo kutangazwa Watakatifu   (@Vatican Media)

Ikilinganishwa na nyenzo kuu na za kiutamaduni, kisayansi na kisanii, imani inashinda sio kwa sababu ya kudharauliwa, lakini kwa sababu bila imani hupoteza maana yake. Uhusiano na Mungu ni muhimu sana kwa sababu Yeye aliumba kutoka katika utupu kila kitu, mwanzoni mwa nyakati, na anaokoa yote …. Kwa yale yanaoisha katika wakati… Dunia isiyo na imani isingekuwa na wana ambao wanaishi na Baba, yaani kwa kiumbe bila wokovu. Hii ndiyo sababu Yesu, Mwana wa Mungu aliyefanyika mwanadamu, anahoji imani: ikiwa ingetoweka kutoka katika ulimwengu, nini kingetokea? Mbingu na dunia zingebaki kama zamani, lakini tumaini lisingekuwepo tena mioyoni mwetu; uhuru wa wote ungeshindwa na kifo; hamu yetu ya maisha ingeporomoka kuwa kitu. Bila imani kwa Mungu, hatuwezi kutumaini katika wokovu. Wokovu huu ni zawadi ya maisha ya milele ambayo tunayapokea kutoka kwa Baba kwa njia ya mwana, na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Misa ya kutangazwa Watakatifu
Misa ya kutangazwa Watakatifu   (@Vatican Media)

Papa alisema kuwa,  kwa sababu hiyo Kristo anazungumza na wafuasi wake “ulazima wa kusali daima, bila kuchoka(Lk 18,1): kama ambavyo hatuchoki kupumua, ndiyo hatupaswi kuchoka kusali. Kama ambavyo kupumua kunasaidia maisha ya mwili, ndiyo ilivyo sala inayosaidia maisha ya roho: imani, kiukweli inajieleza katika sala na katika sala ya dhati inaishi kwa imani. Yesu anatuonesha uhusiano huu kwa kutumia mfano: hakimu anabaki kiziwi kwa maombi yenye mkazo ya mjane, ambaye msisitizo wake hatimaye unamfanya atende. Kwa mtazamo wa kwanza, ukakamavu huu unakuwa kwetu mfano mzuri wa tumaini, hasa nyakati za majaribu na dhiki. Ustahimilivu wa mwanamke na tabia ya mwamuzi, ambaye anatenda kwa kusitasita, hutayarisha Yesu kwa swali la uchochezi: Je! Mungu, Baba mwema, "hatawapatia kisasi wateule wake wanaomlilia mchana na usiku?"(Lk 18,7).

Papa Leo XIV katika misa
Papa Leo XIV katika misa   (@Vatican Media)

Hebu tuache maneno haya yasikike katika dhamiri zetu, Papa alikazia kusema kwamba “Bwana anatuuliza ikiwa tunaamini kwamba Mungu ni mwamuzi wa haki kwa wote. Mwana anatuuliza kama tunaamini kwamba Baba daima anatamani mema yetu na wokovu wa kila mtu. Katika suala hili, majaribu mawili yanajaribu imani yetu: la kwanza huchota nguvu kutoka katika kashfa ya uovu, na kutufanya tuamini kwamba Mungu hasikii kilio cha wanyonge na hana huruma kwa mateso yasiyo na hatia. Jaribio la pili ni tarajio kwamba Mungu lazima atende kama tunavyotaka: sala basi inatoa nafasi ya amri kwa Mungu, ili kumfundisha jinsi ya kuwa na haki na ufanisi. Kutokana na majaribu yote mawili, Yesu, shahidi mkamilifu wa uaminifu wa kimwana, hutuweka huru. Yeye ndiye asiye na hatia, ambaye, hasa wakati wa Mateso yake, anaomba hivi: “Baba, mapenzi yako yatimizwe” (taz. Lk 22:42). Haya ni maneno yale yale ambayo Mwalimu anatupatia katika sala ya Baba Yetu.

Misa ya kutangazwa Watakatifu
Misa ya kutangazwa Watakatifu   (@Vatican Media)

Chochote kitakachotokea, Yesu anajikabidhi kama Mwana kwa Baba; kwa hiyo, kama kaka na dada katika jina lake, tunatangaza: “Ni kweli na haki, ni wajibu wetu na wokovu wetu kuwashukuru ninyi sikuzote na kila mahali; Bwana, Baba Mtakatifu, Mwenyezi na Mungu wa milele, kwa njia ya Kristo Bwana wetu” (Misale ya Kirumi, Sala ya Ekaristi II, Dibaji). Sala ya Kanisa inatukumbusha kwamba Mungu anatenda haki kwa wote, anatoa maisha yake kwa ajili ya wote. Kwa hiyo, tunapomlilia Bwana: “Uko wapi?”, tunageuza ombi hili kuwa sala na kisha kutambua kwamba Mungu yuko pale ambapo wasio na hatia wanateseka. Msalaba wa Kristo unaonyesha haki ya Mungu. Na uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni msamaha: Anauona ubaya na kuukomboa, akajitwika. Tunaposulubishwa kwa maumivu na vurugu, kwa chuki na vita, Kristo tayari yuko pale msalabani kwa ajili yetu na pamoja nasi. Hakuna kilio ambacho Mungu hafariji; Hakuna chozi mbali na moyo wake. Bwana hutusikiliza, hutukumbatia jinsi tulivyo, ili kutubadilisha jinsi alivyo. Wale wanaokataa Huruma ya Mungu hubakia kutokuwa na uwezo wa kuwahurumia wengine. Wale wasiokaribisha amani kama zawadi hawataweza kutoa amani.

Misa ya kutangazwa watakatifu
Misa ya kutangazwa watakatifu   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo kwa njia hiyo alieleza kuwa, “sasa tunaelewa kwamba maswali ya Yesu ni mwaliko wenye nguvu wa tumaini na hatua: Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atapata imani katika usimamizi wa Mungu?” Ni imani hii, kiukweli, ambayo hudumisha kujitolea kwetu kwa haki, hasa kwa sababu tunaamini kwamba Mungu anaokoa ulimwengu kutokana na upendo, akituweka huru kutoka katika kushindwa. Basi na tujiulize: tunaposikia mwito wa wale walio katika shida, je, sisi ni mashahidi wa upendo wa Baba, kama Kristo alivyokuwa kwa wote? Yeye ndiye mnyenyekevu ambaye huwaita wenye kiburi kwenye uongofu, mwenye haki anayetufanya tuwe waadilifu, kama vile watakatifu wapya wa leo wanavyothibitisha: si mashujaa au mabingwa wa baadhi ya watu bora, lakini wanaume na wanawake halisi.

Misa ya kutangazwa Watakatifu
Misa ya kutangazwa Watakatifu   (@Vatican Media)

Waamini hawa rafiki wa Yesu ni Mashahidi kwa ajili ya Imani yao , kama Askofu  Ignazio Choukrallah Maloyan na Katekista Pietro To Rot; Ni wainjilishaji na wamisionari kama Sr Maria Troncatti;, ni wenye karama waanzilishi kama vile Sr Vincenza Maria Poloni na   Carmen Rendiles Martínez;  wale ambao moyo wao unawaka kwa ibada na wafadhili wa ubinadamu kama vile Bartolo Longo na  José Gregorio Hernández Cisneros. Maombezi yao na yatusaidie katika majaribu yetu, na mfano wao ututie moyo katika wito wetu wa pamoja wa utakatifu. Tunaposafiri kuelekea lengo hili, na tuombe bila kuchoka, tukiwa thabiti katika yale tuliyojifunza na kuamini kwa uthabiti (taz. 2 Tim 3:14). Hivyo, imani duniani hudumisha tumaini la mbinguni. Hata hivyo katika Misa hiyo uliimbwa wimbo wa Roho Mtakatifu kwa kumuomba neema ya kufanikia na kuongoza tukio hilo. Ilifuatiwa kuwatangaza Watakatifu ha ona misa kuendelea. Wakati wa sala, ambazo Shemasi alitangulia kueleza, zilikuwa kwa lugha mbali mbali tukianza na na lugha ya kiarmeni: Tuombe kwa ajili ya Kanisa la Mungu, aweze kulidumisha msimamo daima wa imani yake, litangaze na kuongoza wote katika tumaini ambalo halikatishi tamaa.

Kutangazwa kwa Watakatifu 7
Kutangazwa kwa Watakatifu 7   (@Vatican Media)

Kwa Kiingereza:  Tuombe kwa ajili ya watawala na watu wa duniai: kwa kuitwa waongoze hatima ya watu na wazalendo, watumie chaguzi zisizokandamiza na wasaidie amani na wema kwa wote.

Kwa lugha ya kiarabu:Tuombee Wakristo wanaoteseka: ili wawe na nguvu na uvumilivu katika taabu na sadaka yao isaidie  wokovu wa ubinadamu.

Kwa lugha ya Kireno:Tuombe kwa ajili ya maskini, wagonjwa na waaoteseka; kwa kuunganisha mateso yao na yake ya Kristo, maisha yao yafungulie matumaini na kuweza kuibua kati wa Wakristo wahudumu wa huruma na upendo.

Kwa lugha ya Tok Pisin

Tuombe kwa ajili ya vijana wanaofanya mang’amuzi ya miito ili kuwa kuhuishwa na Bwana Yesu, ambaye alijifanya mtumishi, wasikilize kwa upole na furaha ya utashi wa Bwana kwa ajili ya kumtumia kikamilifu.

Mahubiri ya Papa Oktoba 2025
19 Oktoba 2025, 12:07