2025.10.20 Wanahija waliofika kwa ajili ya kutangazwa watakatifu 7 walikutana na Papa Leo XIV. 2025.10.20 Wanahija waliofika kwa ajili ya kutangazwa watakatifu 7 walikutana na Papa Leo XIV.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Watakatifu wapya wawe mfano wa kuigwa kwa kila mtu!

Jumatatu Oktoba 20 Papa Leo XIV alihutubia mahujaji,katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican kwa mahujaji waliofika kwa ajili ya kutangazwa Watakatifu wapya 7 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican,Oktoba 19 ambapo aliwakumbusha “Umoja wa Kanisa unajumuisha waamini wote kama mtindo wa kisinodi,katika nafasi na wakati,katika kila lugha na utamaduni na kutuunganisha kama Watu wa Mungu,Mwili wa Kristo na hekalu hai la Roho Mtakatifu."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo  Jumatatu tarehe 20 Oktoba 2025, akikutana  na mahujaji kutoka duniani kote hasa waliofika kwa ajili ya kutangazwa kwa watakatifu: shahidi Askofu Ignazio Choukrallah Maloyan na Katekista Petro To Rot;  wainjilishaji na wamisionari kama Sr Maria Troncatti;  wenye karama waanzilishi kama Sr Vincenza Maria Poloni na Sr Carmen Rendiles Martínez;  wenye moyo unaowaka kwa ibada na wafadhili wa ubinadamu kama vile Bartolo Longo na José Gregorio Hernández Cisneros. Katoka hotuba ya Papa  alihutubia kwa lugha ya kiitaliano, Kiingereza na kusipanyola. Kwa njia hiyo Papa alielezea jinsi ambavyo Maisha yao yaliyofanywa kuwa ya ajabu kwa upendo wa Mungu ambaye aliwavuvia na kuwaunga mkono katika kujitolea kwao kwa walio hatarini zaidi, katika kutetea ukweli wa imani, na katika mapendo ambayo hayakatishi tamaa katika uso wa dhiki.

Papa akutana na mahujaji waliofika kwa ajili ya kutangazwa watakatifu 7
Papa akutana na mahujaji waliofika kwa ajili ya kutangazwa watakatifu 7   (@Vatican Media)

Akiwalekea katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican Papa alionesha furaha kukutana nao siku moja baada ya kutangazwa watakatifu 7 wapya, ambapo wao wamefika kwa sababu mbali mbali, zinazowaunganisha sana. Aliwasalimia kila mmoja wao,  kwa namna ya pekee makardinali, Maaskofu, wakuu wa mashirika ya watawa, Mamlaka ya kiraia waliokuwepo. “Tukio la furaha na siku kuu ambalo tuliadhimisha jana linatukumbusha kuwa umoja wa Kanisa unawahusisha waamini wote, katika nafasi na katika wakati kwa kila lugha na utamaduni, kwa kutuunganisha kama watu wa Mungu, mwili wa Kristo na Hekali hai la Roho Mtakatifu. Wanaume na wanawake ambao jana tumewatangaza Watakatifu kwa wote ni ishara angavu ya matumaini, kwa sababu walitoa maisha yao katika upendo wa Kristo na kwa ndugu.”

Mtakatifu Maloyan

Papa Leo akizungumza kwa Lugha ya Kiingereza alisema “ tunashiriki wote furaha ya watu wapendwa wa Armenia wakati tutazama utakatifu wa Askofu Shahidi Ignatius Maloyan.  Alikuwa mchangaji kwa mujibu wa moyo wa Kristo na katika kipindi kigumu cha kuachwa kwa zizi, lakini paomoja na hayo kuwatia mouo kuinuka katika imani. Alipoombwa kukana imani yake ili apata kuachiwa huru, yeye hakuacha kumchangwa Bwana, hata kwa amwage damu yake kwa ajili ya Mungu. Katika hilo, Papa leo amebainisha kuwa limemfanya afikiri kwa upendo watu wa Armenia ambao wanatengeneza msalaba wa mawe kama ishara ya msimamo wa  imani na thabiti kama mwamba. Wanaweza kumuomba Mtakatifu mpya apyaisha ari ya waamini na kuzaa matunda ya upatanisha na amani kwa wote.

Mtakatifu Peter To Rot

Tunaweza kuona imani ya kina ya watu wa Papua New Guinea inavyoakisiwa katika Mtakatifu Peter To Rot, anayetutolea kielelezo cha mvuto cha uthabiti na uhodari katika kuhubiri ukweli wa Injili mbele ya magumu na changamoto, hata vitisho kwa maisha yetu. Ingawa alikuwa Katekista wa kawaida, alionesha ujasiri wa ajabu, akihatarisha maisha yake ili kutekeleza utume wake kwa siri, kwani kazi yake ya kichungaji ilikatazwa na majeshi yaliyovamia wakati wa Vita Kuu ya II. Wakati huo huo, wakati mamlaka hizo ziliporuhusu tamaduni za  mitala, Mtakatifu Peter To Rot alitetea kwa uthabiti utakatifu wa ndoa na hata kukabiliana na watu fulani wenye nguvu. Hebu tusikilize maneno yake mbele ya uadui: "Huu ni wakati mgumu sana kwetu, na sote tunaogopa. Lakini Mungu Baba yetu yuko pamoja nasi na anatujali. Ni lazima tuombe na kumwomba awe pamoja nasi daima."Kwa njia hiyo Papa Leo XIV alikazia kuwaeleza kwamba “mfano wa Mtakatifu Peter To Rot ututie moyo kutetea ukweli wa imani hata kwa gharama ya dhabihu ya kibinafsi, na kila wakati kujikabidhi kwa Mungu katika majaribu yetu.”

Mtakatifu Hernandez na Carmen

Papa Leo XIV akiwaelekea kaka na dada wanauzungumza lugha ya kisipanyoa alisema kuwa , maaskofu wa Venezuela walichapisha barua Oktoba 7 iliyopita kuhusu tukio la furaha la kuwaona wana wawili wa nchi yao waipendayo, Mtakatifu José Gergorio Hernández na Mtakatifu Carmen Rendiles, wakiinuliwa kwa heshima katika madhabahu. Walimwomba Bwana awe kichocheo kikubwa kwa WanaVenezuela wote kuungana na kujitambua kuwa wana na ndugu wa nchi moja, hivyo kutafakari mambo ya sasa na yajayo kwa kuzingatia fadhila walizoishi watakatifu hawa kishujaa. Ni lazima tujiulize: ni fadhila zipi hizi zinazopaswa kutuhamasisha? Imani, hakika. Mungu alikuwepo maishani mwao na kuwabadilisha, na kufanya uwepo rahisi wa mtu wa kawaida, kama sisi sote, nuru ambayo ilimulika kila mtu katika maisha ya kila siku kwa nuru mpya. Kisha, bila shaka, wema wa tumaini: ikiwa Mungu ndiye thawabu yetu ya milele, kazi na mapambano yetu hayawezi kuishia katika malengo ambayo, pamoja na kutostahili na kudhalilisha, ni ya kudumu.

Hatimaye, upendo, ambao huzaliwa kutokana na kukaribisha na kushiriki zawadi iliyopokelewa, hutusaidia kugundua maana ya kweli ya maisha na inatuomba tuijenge kupitia huduma kwa wagonjwa, maskini, na wadogo zaidi. Papa Leo aliendelea kusema kuwa "Vema, kutafakari juu ya fadhila hizi kunaweza kutusaidiaje wakati huu wa sasa? Inawezekana kufanya hivyo ikiwa, kwa kuangalia sura  hizi mbili kubwa, tunaona ndani yao juu ya watu wote sawa na sisi wenyewe, ambao waliishi wakikabiliana na changamoto ambazo si ngeni kwetu, na ambao sisi wenyewe tunaweza kukabiliana nazo kama wao, kwa kufuata mfano wao. Na pia kwa kuzingatia kwamba wale wanaoishi karibu nami - kama mimi, kama wao - wameitwa kwa utakatifu huo huo, na kwamba ni lazima kwa hiyo niwaone, kwanza kabisa, kama ndugu wa kuheshimiwa na kupendwa, wakishiriki njia ya uzima, wakisaidiana katika magumu, na kujenga ufalme wa Mungu pamoja kwa furaha.

Mahujaji waliofika kwa ajili ya utakatifu wa watakatifu 7
Mahujaji waliofika kwa ajili ya utakatifu wa watakatifu 7   (@VATICAN MEDIA)

Kwa lugha ya kiitaliano, Baba Mtakatifu alizingumza akisema kwa “ katika majaliwa yake, Mungu alilipatia Kanisa Sista Vincenza Maria Poloni, mwanzilishi wa Masista wa Huruma. Ukarimu wake unashuhudia huruma ya Yesu kwa wagonjwa na waliotengwa. Kukuza uwajibikaji wake wa kijamii kwa hali ya kiroho ya Ekaristi na ibada ya Maria, Mtakatifu Vincenza anatuhimiza kudumu katika huduma ya kila siku kwa walio hatarini zaidi: ni pale hasa ambapo utakatifu wa maisha unastawi!"

Papa Leo aliendelea kusema kuwa "Vema, kutafakari juu ya fadhila hizi kunaweza kutusaidiaje wakati huu wa sasa? Inawezekana kufanya hivyo ikiwa, kwa kuangalia sura  hizi mbili kubwa, tunaona ndani yao juu ya watu wote sawa na sisi wenyewe, ambao waliishi wakikabiliana na changamoto ambazo si ngeni kwetu, na ambao sisi wenyewe tunaweza kukabiliana nao kama wao, kwa kufuata mfano wao. Na pia kwa kuzingatia kwamba wale wanaoishi karibu nami - kama mimi, kama wao - wameitwa kwa utakatifu huo huo, na kwamba ni lazima kwa hiyo niwaone, kwanza kabisa, kama ndugu wa kuheshimiwa na kupendwa, wakishiriki njia ya uzima, wakisaidiana katika magumu, na kujenga ufalme wa Mungu pamoja kwa furaha. Kwa lugha ya kiitaliano, Baba Mtakatifu alizingumza kuwa, “ katika majaliwa yake, Mungu alilipatia Kanisa Sista Vincenza Maria Poloni, mwanzilishi wa Masista wa Huruma. Ukarimu wake unashuhudia huruma ya Yesu kwa wagonjwa na waliotengwa. Kukuza uwajibikaji wake wa kijamii kwa hali ya kiroho ya Ekaristi na ibada ya Marian, Mtakatifu Vincenza anatuhimiza kudumu katika huduma ya kila siku kwa walio hatarini zaidi: ni pale hasa ambapo utakatifu wa maisha unastawi!"

Mtakatifu Bartolo Longo

Mabadiliko haya, ambayo neema ya Mungu hufanya kazi ndani ya moyo, yanapata mfano mkali sana katika Bartolo Longo. Baada ya kuongoka kutoka katika maisha ya mbali na Mungu, alijitolea nguvu zake zote kwa matendo ya huruma ya kimwili na ya kiroho, akikuza imani katika Kristo na upendo kwa Maria kwa njia ya upendo kwa yatima, maskini na waliokata tamaa. Kwa shukrani kwa mwanzilishi wake, Madhabahu ya Pompei yalihifadhi na kueneza ari ya Mtakatifu Bartholomayo, mtume wa Rozari. Kwa moyo mkunjufu ninapendekeza sala hii kwa kila mtu, kwa : makuhani, watawa, familia, na vijana. Tukitafakari mafumbo ya Kristo kupitia macho ya Maria, siku baada ya siku tunaiga Injili na kujifunza kuitenda. “Wapendwa mahujaji, ninatumaini mtarudi katika nchi zenu na mioyo iliyojaa shukrani na hamu kubwa ya kuwaiga watakatifu wapya." Maombezi yao yawaongoze na mfano wao uwatie moyo. Kwa upendo Papa alitoa baraza kae za kitume kwao wote.

Papa kwa mahujaji na ushuhuda wa masisita wa Huruma

Asante sana kwa kusoma makala hii. Kama unataka kubaki na sasisho la kila siku, jiandikishe kwa kubonyeza hapa: Just click here

20 Oktoba 2025, 16:00