Papa Leo XIV:Kusaidia,kukaribisha na kuhamasisha binadamu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana mjini Vatican na kikundi cha wale wanaohudumia wahitaji cha Mtakatifu Francis kwa ajili ya Maskini kutoka Milano nchini Italia tarehe Mosi Septemba 2025 katika Jumba la Kitume mjini Vatican. Katika hotuba alionesha furaha ya kukutana nao. Karibu miaka 60 tangu kuanza kwa jitihada hiyo ya kuwakikisha utunzaji na makaribisho ya watu wanye hali ya uhitaji na (…) kusaidia kuhamasisha ubinadamu ulimwenguni wa mti katika muktadha wa utamaduni wa kikristo na hasa ule wa kifransiskani, wa mafundisho ya kanisa na Majiterio yake”( rej.Mfuko wa kazi ya Mtakatifu Francis kwa ajili ya maskini, kanuni 3). Jumuiya ya kazi hii ilizaliwa kutokana na moyo wa ukarimu wa mlinda mlango mnyenyekevu,Ndugu Cecilio Maria Cortinovis, aliyejali mahitaji ya maskini waliobisha hodi kwenye mlango wa Konventi ya Wakapuchini huko Viale Piave, Milano. Yule Padre mwema alikuwa amemwomba Bwana amsaidie kuwapa marafiki hawa huduma bora zaidi, na Majaliwa ya Mungu akamjibu, akiweka mtu mwingine mkarimu kando yake: Dk. Emilio Grignani. Ndivyo ilianza tukio zuri ambalo nyote ni mashuhuda na wahusika wakuu leo.
Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kusema kwamba, kile wanachofanya ni katika muktadha wa tamaduni ya kifransiskani, na ni vema kukumbuka baadhi ya maneno ya Mtakatifu Francis kuhusu maskini: “ Unapoona maskini, alikuwa anasema Mtakatifu wa Assisi, unawekwa mbele ya kioo cha Bwana na Mama yake maskini. Ndivyo pia kwa wagonjwa watambue kuona ndani ya ugonjwa wa Yesu aliojivika(Mt Boneventure, Leggenda maggiore, 8, 5: Fonti francescane, 1142). Na siku moja akitaka kumpatia mwenye shida joho lake, na kwa kutafakari juu ya kushirikishana kidugu zawadi za Mungu alikuwa amethibitisha: “Lazima turudishe joho(…) kwa maskini: kwa sababu ni lake. Kiukweli sisi tulipokea kama mkopo, hadi tutakapokuwa tumekumbana na aliye maskini zaidi yetu( Fonti, 1143). Papa Leo XIV kwa kuongeza: “ sisi leo tunakumbuka historia ya upendo ambayo ilizaliwa na imani ya mtu, na kuchanua katika maisha kwa jumuiya kubwa inayohamasisha amani na haki. Tunaadhimisha historia iliyofanya si wafadhili na wanaofadhiliwa, bali kaka na dada ambao wanajitambua, mmoja na mwingine, zawadi ya Mungu, uwepo wake msaada wa pamoja katika safari ya utakatifu. Tunatukuza Mwili wa Kristo, ulio na majeraha na wakati huo huo ukiendelea kupona, ambapo wajumbe wake wanasaidiana mmoja na mwingine, wakiwa wamungana na Mkuu wa upendo wenyewe(Mtakatifu Agostino,Sermo 53/A,6); na kweli hivyo tunaona mwili hai, ambao unakua kila siku kuelekea ukamavu kamili.
Katika Kanuni ya Kazi ya Mtakatifu Francis, kwa Maskini, inasisitiza mambo matatu msingi ya kazi yao ambayo inajumuisha vipengele vya ziada kukamilishana na vya msingi wa kutoa msaada: kusaidia, kukaribisha na kuhamasisha. Kusaidia kuna maana ya kuwepo halisi kwa mahitaji ya jirani. Na katika mapendekezo hayo inashangaza wingi na huduma mbali mbali ambazo katika muktadha wa miaka, waliweza kupanga na kutoa kwa yule aliyewaelewa wao: kuanzia vituo vya chakula hadi mavazi kuanzia vituo vya kuogea hadi zahanati, kuanzia kwenye huduma za usaidizi ksaikolojia hadi ushauri kwa ajili ya kazi, kwa kutoa baadhi ya mifano tu, hadi kufikia kusaidja kwa nana mbali mbali zaidi ya watu 30,000 kwa mwaka. Baba Mtakatifu alisisitiza kuwa katika hilo karibu kuna ukaribisho yaani kutoa nafasi kwa mwingine katika moyo binafsi, katika maisha binafsi, kutoa muda, kusikiliza, kusaidia na sala. Ni tabia za kutazama machoni, kushikana mikono, kuinama, ambazo zilikuwa pendwa kwa Papa Francisko(Katekesi ya Jubilei 9 Aprili 2016) ambaye anatusukuma kukuza katika mazingira yetu, hali ya kifamilia, na ambaye anatusaidia kushida upweke wa “umimi” kupitia umoja angavu wa “sisi” (Rej. Mkesha wa sala na vijana wa Italia 11 Agosti 2018). Papa aliongeza “ kuna uhitaji wa kueneza hali hii ya hisia katika jamii yetu, mahali ambapo wakati mwingine ambapo kinyume kujetenga ni janga kubwa!
Na ya tatu ni ile ya kuhamasisha. Papa alisema kuwa “ hapa ndipo kuingia katika mchezo wa kutokuwa na mafao ya zawadi na heshima ya hadhi ya watu, ambapo ni kushughulika na mtu tunayekutana naye tu kwa sababu ya wema wake, kwa sababu aweze kukua katika uwezo wake wote na kuendelea katika njia yake bila kusubiri saburi yoyote na wala bila kupendekeza masharti. Kama vile Mungu anavyofanya na kila mmoja wetu, akituonesha njia, akitupa msaada wote tunaohitaji kuufuata, lakini kisha kutuacha huru. Kuhusiana na hilo, Papa aliongeza: “Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika: "Ni jambo [...] la kuongeza kwa ufanisi heshima na ubunifu wa kila mtu binafsi, uwezo wao wa kuitikia wito wao wenyewe na, kwa hiyo, kwa wito wa Mungu ulio ndani yake." (Waraka wa Centesimus annus, 1° Mei 1991, 29). Kwa kuhitimisha, Papa Leo XIV kwa wajumbe hao alisema “ni Kazi ambayo Kanisa inawakabidhi kwa faida ya watu wanaozunguka taasisi mnazosimamia na jamii kwa ujumla. Kutekeleza upendo kwa kuzingatia ustawi wa watu wengine, kiukweli, "ni fursa nzuri kwa ukuaji wa maadili, kiutamaduni, na hata kiuchumi kwa wanadamu wote" (ibid., 28). Asante kwa kile mnachofanya na kwa ushuhuda mnaotoa kwa safari yenu ya pamoja! Ninasindikiza kwa maombi yangu na kuwabariki kwa moyo wote.”
