Papa Leo XIV:Taasisi za Ulaya zinahitaji kukuza usekula wenye afya
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Leo XIV Jumatatu tarehe 29 Septemba 2025 alikutana katika Jumba la Kitume na wajumbe wa "Kikundi Kazi cha Mazungumzo ya Kiutamaduni na Kidini," chombo cha Bunge la Ulaya. Baba Mtakatifu XIV akianza hotuba yake alionesha furaha ya kukutana nao katika muktadha wa Bunge la Ulaya kwamba walianzisha maisha “Kikundi Kazi cha Mazungumzo ya Kiutamaduni na Kidini ambapo Papa aliwapongeza kuanzishwa huko na kuwatakia kwamba wanaweza kupelekea matunda bora.
Ushuhuda wa wakristo kuhamasisha mazungumzo ya kidini
Papa alisisitiza kwamba uhuisho wa kikristo na shukurani kwa Mungu hawakosekani watu ambao walitoa ushuhuda mzuri katika maana hiyo. Baba Mtakatifu alieleza kwamba, “kufanya kazi kwa ajili ya mazungumzo ya kidini, yenyewe inapelekea kutambua kwamba dini ni ya thamani, iwe kwa ngazi kibinafsi, na iwe katika muktadha wa kijamii. Neno lenyewe dini linaelezea uhusiano ambao ni kitu cha asili ya binadamu.” Kwa njia hiyo mantiki ya dini, ikiwa ni ya dhati na kukuzwa vizuri, inathibitisha ubora wa mahusiano ya kibinafsi na kusaidia sana kuunda mtu aishi katika jumuiya na katika jamii. “ Papa Leo aliongeza kusema, ni kwa jinsi gani leo hii ilivyo muhimu kutoa thamani na maana ya mahusiano ya kibinadamu!”
Kujua kuunganisha Usekula na dini yenye afya
Taasisi za Ulaya zinahitaji watu wanaojua jinsi ya kuzoea Usekula na dini yenye afya, yaani, mtindo wa kufikiri na kutenda unaothibitisha thamani ya dini huku wakihifadhi tofauti yake - si kutengana au kuchanganyikiwa, kuhusiana na nyanja ya kisiasa. Hata katika hili, zaidi ya maneno, inatosha kuona mfano wa Robert Schuman, Konrad Adenauer e Alcide De Gasperi,” hawa ni waanzilishi wa Umoja wa Ulaya. Kwa kuhitimisha Papa aliwashukuru tena kwa ziara hiyo na anawaombe wa ona kazi yao Baraka ya bwana.
