Papa Leo XIV akutana na Rais wa Moldavia
Vatican News
Ijumaa asubuhi tarehe 12 Septemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Bi Maia Sandu, Rais wa Jamhuri ya Moldovia, katika Jumba la Kitume, mjini Vatican.
Baada ya Mkutano huo na Papa pia alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican, akifuatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Majadiliano katika Sekretarieti ya Nchi
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican, ilibainisha, "Wakati wa mkutano wa kidugu katika Sekretarieti ya Vatican, shukrani ilioneshwa kwa uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili, kwa matumaini ya kuimarishwa zaidi." Kadhalika, majadiliano yalilenga juu ya hali ya amani na usalama katika ngazi mahalia, kikanda na kimataifa, kwa kuzingatia hasa hali inavyoendelea ya hivi karibuni nchini Ukraine.
