2025.09.26 Askofu  Filippo Iannone 2025.09.26 Askofu Filippo Iannone 

Papa amemteua Askofu Iannone kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu

Uteuzi wa Kwanza kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa upande wa Papa Leo XIV tangu achaguliwe,amemekabidhi aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maandishi ya Kisheria,kiungo,alichokiongoza tangu Januari 2023 hadi Mei 2025 kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa papa.Mkarmeli anakuwa Mwenyiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu.Atachukua madaraka Oktoba 15.Montanari amethibitishwa kuwa katibu Mkuu na Kovač kama Katibu msaidizi kwa muda wa miaka mitano.

Vatican News

Ulikuwa uteuzi ambao wengi walitarajia kuwa wa kwanza, kama ilivyotokea hata kwa Papa Benedikto XVI na mrithi wake wa Mafundisho Tanzu ya Kanisa, William Joseph Levada. Huo ni uteuzi wa "mrithi" wa kuongoza Baraza la Kipapa la Maaskofu,  chombo cha Curia Romana ambacha Papa Leo  mwenyewe alikiongoza tangu Januari 2023, kwa uteuzi wa Papa Fransisko, aliyemhamisha kutoka huko Peru hadi Roma na kuongoza hadi Mei 2025 wakati alipochaguliwa kuwa mrithi wa Mtume Petro. Ijumaa  tarehe 26 Septemba 2025, Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Askofu Mkuu Filippo Iannone, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Nyakaraka za Kisheria,  kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maaskofu, jukumu ambalo linajumuisha pia urais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini.

Katibu na Naibu Katibu Wamethibitishwa

Hili lilitangazwa katika taarifa ya saa 6:00 kamili mchana  kutoka  Ofisi ya  Vyombo vya habari vya Vatican ambayo inasema kwamba “Iannone atachukua wadhifa wake mnamo tarehe 15 Oktoba  2025.” Wakati huo huo, Papa alithibitisha kuwa “Katibu Mkuu wa Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano zaidi kwa Monsinyo Ilson de Jesus Montanari, Askofu wa Brazil tayari alikuwa katika nafasi yake ya pili  ambayo alianza tangu 2013”, chini ya Uongozi wa Papa Francisko na vile vile Papa pia alimthibitisha Monsinyo Ivan Kovač kama Naibu Katibu kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Uteuzi wa Monsinyo Iannone ni uteuzi wa kwanza wa Papa wa Kiagostino kwa mkuu wa Baraza la Kipapa. Kabla ya uteuzi pekee wa nafasi ya juu katika Baraza la Curia Romana ulifanyika Mei 22, siku chache tu baada ya kuchaguliwa kwake,  kwa Sr Tiziana Merletti, Mtawa wa Taasisi ya Masista wa Kifransiskani wa Maskini, kama Katibu  Mkuu wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Taasisi za Maisha ya Wakfu na Vyama vya Kitume.

Mwanasheria wa Kanoni

Akiwa na umri wa miaka  68,  tarehe 13 Desemba, Askofu Mkuu Iannone, alizaliwa Napoli na ni Mtawa Mkarmeli, mwanasheria, na wakili wa Kanisa, mwenye uzoefu mkubwa katika mahakama, vyuo vikuu vya kipapa, na Vatican ambapo ameshika nyadhifa mbalimbali Roma, kwa kuongeza kuwa  mjumbe wa Baraza Kuu la Saini ya Kitume, mshauri wa Shirika la wakati huo la Taasisi za Maisha ya Wakfu, mjumbe wa Baraza la Masuala ya Kisheria la Baraza la Maaskofu la Italia (CEI), rais wa Kamati ya Majengo ya Kidini, na mjumbe wa Baraza la Maaskofu ya Lazio. Mwaka 2012, aliteuliwa kuwa makamu wa Jimbo Kuu la Roma na Papa Benedikto XVI; Papa mwingine, Francisko, alimhamisha kutoka katika huduma hiyo ya kichungaji hadi ile ya Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maandiko ya Sheria mwaka 2017. Akawa Mkuu wa ofisi hiyo hiyo mwaka uliofuata, kunako tarehe 7 Aprili 2018.

Kazi ya kuchagua maaskofu wa dunia

Sasa inakuja kazi ya kuendeleza kazi ambayo Papa wa sasa  ameifanya kwa miaka miwili. Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu ana kazi nyeti: kumsaidia Papa katika kuchagua wachungaji ambao atawakabidhi jumuiya za kikanisa katika maeneo yaliyo chini ya mamlaka yake. Na baada ya kuwatambua mapadre wa kupendekeza uaskofu, uamuzi wa mwisho ni wa Papa. Ili kusaidia katika utume huu, Papa Francisko aliteua wanawake watatu kuwa washiriki wa Barza la Maaskofu  kunako Julai 2022: Sr Raffaella Petrini, Gavana wa sasa wa Mji wa Vatican; Sr Yvonne Reungoat, Mkuu wa Shrika wa zamani wa Mabinti wa Maria Msaada wa Wakristo; na Bi Maria Lia Zervino, rais wa zamani wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani (WUFC).

 

26 Septemba 2025, 13:13