Papa akutana na Rais wa Ujerumani Bwana Walter Steinmeier. Papa akutana na Rais wa Ujerumani Bwana Walter Steinmeier.   (ANSA)

Papa na Rais wa Ujerumani:vita vya Ukraine na haja ya kufikia usitishaji na amani ya haki

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana Jumatatu asubuhi Septemba 22 katika Mkutano wa faragha na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier, na mkewe,Elke.Mkuu wa nchi alisema yeye na Papa walijadili "hali ya kimataifa,vita na amani,na hali ya Makanisa ya Kikristo." Walijadili vita vya Ukraine na Gaza hasa. Katika hali hizi,aliongeza,Papa ni mmoja wa watu wachache ambao wanaweza kutoa ushawishi kwa wahusika kwenye mzozo.

Vatican News

Jumatatu asubuhi tarehe 22 Septemba 2025,  Papa Leo XIV alikutana na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier, katika Mkutano wa faragha, akifuatana na mke wake, Elke.

Papa na  rais wa Ujerumani
Papa na rais wa Ujerumani   (@Vatican Media)

Katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Makaburi ya Teutonic huko Vatican, mkuu wa nchi ya Ujerumani alisema fursa ya kuzungumza kwa muda mrefu na Papa na "kubadilishana maoni, kwa kawaida juu ya hali ya kimataifa, juu ya vita na amani, na juu ya hali ya Makanisa ya Kikristo."

Wakati wa mazungumzo ya faragha
Wakati wa mazungumzo ya faragha   (@Vatican Media)

Alieleza kwamba walijadili hasa vita vya Ukraine, mateso ya watu wa Ukraine, na haja ya kufikia usitishaji vita na amani ya haki. Hali ya kibinadamu huko Gaza pia ilijadiliwa, na rais wa Ujerumani alisisitiza kuwa katika hali hizi za kimataifa, sauti ya Papa ni muhimu kama sababu ya mazungumzo na upatanishi. "Nilimtia moyo sana kudumisha jukumu hilo," alisema Steinmeier, ambaye ni Mprotestanti, wakati mke wake ni Mkatoliki. Na ninaamini kwamba nyakati ambazo kuna wapatanishi wachache duniani na watu wachache wanaoweza kuwa na ushawishi kwa pande zinazozozana, hatuwezi kufanya bila msaada unaotolewa na Papa.” Rais alimkaribisha Papa Leo kutembelea Ujerumani.

Wakati wa kubadilishana zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi   (@Vatican Media)

Wakati wa kubadilishana zawadi Papa Leo XIV alimpatia mgeni wake paneli ya fedha iliyopakwa rangi ya enamel ya moto, inayoonesha "Musa Aliyeokolewa kutoka katika Maji," iliyoongozwa na Picha ya mchoraji Raphael katika Chumba cha  pili cha Jumba la Kitume.

Wakatif Rais Steinmeier alimkabidhi Papa nakala ya alama Mchoro wa Clavier, mkusanyiko wa maandishi ya Johann Sebastian Bach, na chupa kadhaa za mvinyo kutoka shamba la mizabibu la Monasteri ya Kibenediktini,  awali ilikuwa ya kiagostiniani, ya Hildegard wa Bingen, Eibingen-Rüdesheim, huko Asia. Hii ni ya aina ya kitawa ya kale, ambalo sasa linaendeshwa na watawa wa Kibenediktini ambao huzalisha mvinyo za hali ya juu zilizochochewa na tamaduni  ya milenia iliyohusishwa na Hildegard wa Bingen (1098-1179).

Papa na Rais wa Ujerumani

 

 

22 Septemba 2025, 18:16