2025.09.04 Papa na Rais  Isaac Herzog, wa Serikali ya Israel. 2025.09.04 Papa na Rais Isaac Herzog, wa Serikali ya Israel.  (@Vatican Media)

Papa akutana na Rais Herzog:Kusitishwa mapigano,Gaza na kuingia misaada ya kibinadamu

Wakati wa Mkutano na Rais wa Israel,hali ya Mashariki ya Kati na hasa mkasa katika Ukanda huo,ilichambuliwa.Kuachiliwa kwa mateka wote kuliakisiwa na Vatican na "suluhisho la serikali mbili kama njia pekee ya kutoka katika vita."

Vatican News

Wakati ujao thabiti lazima uanzishwe katika eneo ambalo limevumilia historia ndefu ya migogoro ambayo bado ni "nyingi." Na lengo hili, hasa kutokana na "hali ya kutisha" huko Gaza, linaweza kufikiwa kwa "kurejesha mazungumzo ya haraka" kati ya pande zinazohusika, kwa "utayari na maamuzi ya ujasiri" na "msaada wa jumuiya ya kimataifa, kwa lengo la "kupata kuachiliwa kwa mateka wote, kufikia haraka usitishaji wa kudumu wa mapigano, kuwezesha kuingia kwa usalama kwa misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathirika zaidi, na kuhakikisha heshima kamili kwa sheria ya kibinadamu, pamoja na matarajio halali ya watu wote wawili."

"Njia pekee ya kutoka katika vita"

Haya ndiyo mambo makuu ambayo yalibainishwa asubuhi Alhamisi ya tarehe 4 Septemba 2025, katika Mkutano wa Papa Leo XIV na Rais wa Israel Bwana Isaac Herzog. Baada ya kukutana na Papa katika Jumba la Kitume, Rais Herzog alikutana katika Sekretarieti ya Vatican na Kardinali Pietro Parolin Katibu Mkuu wa Vatican  na Askofu Mkuu Paul R. Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Rais wa Israel akutana na Sekretarieti ya Vatican.
Rais wa Israel akutana na Sekretarieti ya Vatican.   (@Vatican Media)

Katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican iliripoti kwamba mjadala huo ulilenga "hali ya kisiasa na kijamii katika Mashariki ya Kati" na, kutafakari jinsi ya "kuhakikishia mustakabali wa watu wa Palestina" na "amani na utulivu katika eneo hilo," Vatican, kwa mujibu wa taarifa hiyo inasisitiza kuwa ilithibitisha "suluhisho la serikali mbili kama njia pekee ya vita vinavyoendelea."

Mahusiano ya Vatican na Israel

Taarifa hiyo pia inasema kwamba "rejeo lilifanywa katika matukio katika Ukanda wa Magharibi na suala muhimu la Jiji la Yerusalem," na kwamba "umuhimu wa kihistoria wa uhusiano kati ya Vatican na Israel" pia ulishughulikiwa. Taarifa hiyo pia ilizungumzia "masuala fulani kuhusu uhusiano kati ya mamlaka ya serikali na Kanisa la mahali, kwa uangalifu mkubwa," taarifa hiyo ilisema, "kwa umuhimu wa jumuiya za Kikristo na kujitolea kwao huko na Mashariki ya Kati yote kwa maendeleo ya binadamu na kijamii, hasa katika maeneo ya elimu, kukuza mshikamano wa kijamii, na utulivu wa eneo."

04 Septemba 2025, 16:42