2025.08.19 Mkutano wa Maaskofu Kanda ya Amazonia huko Bogota, Colombia. 2025.08.19 Mkutano wa Maaskofu Kanda ya Amazonia huko Bogota, Colombia. 

Papa:Kutangaza Injili,Haki na Mazingira ndio Vipaumbele vya Maaskofu wa Amazonia

Katika telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Parolin,Katibu Mkuu wa Vatican iliyotumwa katika Mkutano wa Kikanisa wa Amazonia(CEAMA),unaondelea huko Bogotá,Papa Leo XIV aliwahimiza Maaskofu wa eneo hilo kuendelea na utume wao kwa niaba ya wakazi wa eneo pendwa la Amazonia.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV alituma telegram iliyosainiwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican kwa Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Amazonia, ikielekezea kwa Kardinali Pedro Ricardo Barreto Jimeno, S.J. Rais wa Baraza la Kikanisa la Amazonia. Katika telegrama hiyo, Papa Leo XIV aliwasalimu kuanzia kwake na hata kwa washiriki wa Mkutano wa Maaskofu wa Amazonia(CEAM), ambao walianza Mkutano tarehe 17 Agosti na utahitimishwa tarehe 20 Agosti 2025 huko Bogotà.  Baba Mtakatifu aliwashukuru kwa jitihada zao katika kuhamasisha wema mkuu zaidi wa Kanisa kwa ajili ya waamini wapendwa wa Amazonia na kuzingatia kile ambacho kilichukuliwa kwenye Sinodi ya Usikivu na ushiriki wa miito yote ya Kanisa, na kuwashauri kutafuta msingi wa umoja na mshikamano wa kila kiungo cha kiaskofu(Hati ya mwisho wa Sinodi Maalum kwa ajili ya Amazonia, 115), kwa namna ambayo husaidia kwa dhati na mwafaka wa Maaskofu wa majimbo na vikarieti za kitume kutimiza utume wao.

Kutoa mkate na habari njema

Kwa mtazamo huo, Papa anawaalika kuzingatia mambo makuu matatu yanayosukana katika matendo ya kichungaji katika kanda hiyo: Utume wa Kanisa wa kutangaza Injili kwa watu wote (Hati ya Ad gentes 1), kuwahudumia watu wote sawa ambao wanaishi humo na utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja. “Ni muhimu kwamba Yesu Kristo, ambaye vitu vyote viko juu yake(Ef 1,10), ili aweze kutangazwa kwa uwazi na upendo mkuu kati ya wakazi wa Amazonia, kwa namna ambayo tunajibidisha kutoa kwao mkate hai na safi wa habari njema na umwilisho wa mbingu wa Ekaristi, njia moja ya kuwa kweli watu wa Mungu na mwili wa Kristo.”

Asili inazungumza 

Katika utume huu, tunasukumwa na uhakika, unaothibitishwa na historia ya Kanisa, kwamba mahli popote pale ambapo jina la Kristo linahubiriwa, ukosefu wa haki hupungua kwa uwiano, kwani, kama mtume Paulo anavyothibitisha, kuwa kila unyonyaji wa mwanadamu unatoweka ikiwa tunaweza kukaribishana kama ndugu(rej. Flp 1:16). Katika muktadha wa fundisho hilo la kudumu, si kidogo zaidi ni haki na wajibu wa kutunza “nyumba” ambayo Mungu Baba ametukabidhi sisi kama mawakili wanaojali, ili kwamba mtu yeyote asiharibu bila kuwajibika kwa vitu vya asili ambavyo vinazungumza juu ya wema na uzuri wa Muumba, sembuse  anayenyenyekea kwao kama mtumwa au mwabudu wa asili, kwa vile Mungu amepewa na kutimiza malengo yetu ya mwisho ya kumsifu Mungu na kupata wokovu wa roho zetu(rej.Mtakatifu Ignatius wa Loyola, Mafungo ya kiroho,23).  Kwa matashi haya, Baba Mtakatifu anawapa kwa moyo mkunjufu Baraka ya Kitume waliyoomba, ambayo kwa hiari yake anawapatia hata wale wote waliokabidhiwa uchungaji wake.

Telegram ya Papa huko Amazonia

 

19 Agosti 2025, 08:43