Papa:Kukomesha silaha nchini Ukraine na njaa huko Gaza na mateka waachiliwe!
Vatican News
Makubaliano ya kusitisha mapigano na amani nchini Ukraine, azimio la mgogoro wa kibinadamu na njaa, na kuachiliwa kwa mateka wa Israel huko Gaza. Haya ndiyo malengo ya "diplomasia laini" ya Vatican, kwa matatizo ambayo "hayawezi kutatuliwa kwa vita," na hili ndilo ambalo Papa Leo XIV anaomba na kutarajia. Alisema hayo jioni tarehe 13 Agoati 2025 kwa waandishi wa habari alipowasili huko Castel Gandolfo, ambapo atatumia mapumziko ya pili ya majira ya joto, hadi Agosti 19. Akiwasalimia watu wengi waliomsubiri kuwasili kwake, mbele ya lango la Villa Barberini, makazi yake kwa siku chache zijazo, Papa Leo alijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu mambo ya kimataifa ya sasa.
Daima kutafuta mazungumzo, kazi ya kidiplomasia
Alipoulizwa nini anachotarajia kutoka katika mkutano wa kilele katikati ya Agosti kati ya Rais wa Marekani, Bwana Donald Trump na Rais wa Urusi, Bwana Vladimir Putin, Leo XIV alijibu: "Lazima siku zote tutafute usitishaji vita, lazima tukomeshe ghasia, vifo vingi. Hebu tuone jinsi wanavyoweza kufikia makubaliano." Kwa nini vita baada ya muda mrefu? Kusudi ni nini? Lazima kila wakati tutafute mazungumzo, kazi ya kidiplomasia, na sio vurugu, sio silaha. Na alipoulizwa kama alikuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa kuwafukuza wakazi wa Gaza, Papa alisema: "Mgogoro ya kibinadamu lazima utatuliwe, hatuwezi kuendelea hivi. Tunajua ghasia za ugaidi na tunaheshimu wengi waliokufa, pamoja na mateka; wanahitaji kuachiliwa. Lakini lazima pia tufikirie wengi wanaokufa kwa njaa."
Matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa na vita
Hatimaye, aliulizwa kile ambacho Vatican inafanya kukomesha migogoro hii na mingineyo. Papa Leo XIV alijibu kwamba “Kiti kitakatifu hakiwezi kuacha… lakini tunafanya kazi, tuseme, kuelekea ‘diplomasia laini,’ siku zote tukialika na kusukumana kutafuta uasi kwa njia ya mazungumzo na kutafuta suluhisho, kwa sababu matatizo haya hayawezi kutatuliwa kwa vita.”
Katika Katekesi: Mungu awape amani watu wote
Asubuhi tarehe 13 Agosti 2025 wakati wa Katekesi yake katika Ukumbi wa Paulo VI, katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland, Baba Mtakatifu alitoa angalizo la dunia kwa watu wa nchi zilizokumbwa na migogoro na ghasia: "Tuombe Mungu awape amani watu wote wanaokumbwa na janga la vita." Ombi la Papa lilitokana na mfano wa Mtakatifu Maximilian Maria Kolbe, Mfransiskani wa Poland ambaye alikufa katika kambi ya mateso ya Auschwitz, ambapo alijitolea kuchukua nafasi ya baba aliyewekwa jela afe kwa njaa. Kumbukizi yake, inafanyika kila ifikapo tarehe 14 Agosti yak ila mwaka, katika mkesha wa Siku kuu ya Bikira Maria Mpalizwa mbingini.
Misa na Sala ua Malaika huko Castel Gandolfo kwa ajili ya Sikukuu ya Kupalizwa mbinguni
Katika kipindi hiki cha pili cha mapumziko katika makazi ya Villa Barberini, ndani ya Bustani za Kipapa, Baba Mtakatifu Leo XIV atakuwa na mipango kadhaa kwa umma. Siku ya Ijumaa, Agosti 15, Siku kuu ya Kupalizwa kwa Bikira Maria Mbinguni, Saa 4.00 asubuhi masaa ya Ulaya, Papa ataadhimisha Misa Takatifu katika Parokia ya Mtakatifu Tommaso wa Villanova huko Castel Gandolfo, na saa 6:00 mchana atasali sala ya Malaika kutokea kwenye mlango wa Ikulu ya Papa huko Uwanja wa uhuru (Piazza della Libertà), Castel Gandolfo.
Albano, Misa na Chakula cha Mchana na Maskini wa Caritas Jimbo
Dominika, tarehe 17 Agosti 2025 saa 3:30 asubuhi masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu Leo XIV ataadhimisha Misa Takatifu katika madhabahu ya Maria wa Rotonda huko Albano Laziale, wakiwa na maskini wakisaidiwa na watu wa kujitolewa wa Caritas Jimbo. Saa 6.00 kamili mchana atasali sala ya Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Uhuru(Piazza della Libertà,) huko Castel Gandolfo. Hatimaye, atashiriki chakula cha mchana pamoja na maskini na wale wanaowasaidia wa Caritas Jimbo katika ukumbi wa Borgo Laudato si', ndani ya Majengo ya Kipapa.
