Papa Francisko huko Hospitalini Gemelli amelala salama
Vatican News
Jumatatu tarehe 24 Februari 2024 Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican, saa 2.18 asubuhi ilitoa sasisho ya hali ya Papa Francisko kwa waandishi wa habari kwamba: "Papa Francisko alilala salama usiku na anaendelea kupumzika."
Sala ya Rozari Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari kuanzia tarehe 24 Februari kutakuwa na Rosari Takatifu katika uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya kuombea afya ya Baba Mtakatifu saa 3 kamili usiku.
"Kuanzia usiku huu, Makardinali wanaoishi Roma na wahudumu wote wa Curia Romana na Jimbo la Roma, kwa kupokea hisia za Watu wa Mungu, watakusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, saa 3.00 kamili masaa ya Ulaya ikiwa ni saa 5 saa za Afrika mashariki na Kati, ili kusali Rozari Takatifu kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu. Sala ya Usiku wa leo, itaongozwa na Mwadhama Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican."
Sasisho la tarehe 23 Februari
Kwa siku ya Dominika tarehe 23 Februari 2025, Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican ilitoa taarifa kuhusu matibabu ya Baba Mtakatifu Francisko, Dominika jioni kuwa: "Hali ya Baba Mtakatifu bado ni tete, lakini tangu jana jioni, hajapata matatizo zaidi ya kupumua. Alifanyiwa vipimo viwili vya seli nyekundu za damu zilizojilimbikizia na matokeo ya vipimo vyake vya damu vimeongezeka. Thrombocytopenia(uwepo wa idadi ndogo za seli za damu), zinabaki thabiti; hata hivyo, baadhi ya vipimo vya damu vinaonesha kushindwa kidogo kwa figo, ambayo kwa sasa iko chini ya udhibiti. Anatumia mtiririko wa oksijeni kwa ajili ya kupumua.
