Papa kwa Umoja wa Vipofu na Ulemavu wa Macho:muwe ishara za matumaini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko akikutana tarehe 3 Januari 2025 na ujumbe wa Umoja wa Wasioona na wenye Ulemavu wa Macho nchini Italia katika ukumbi wa Clementina mjini Vatican ameanza hotuba yake akiwa wakaribisha na kumsalimia Rais na wote. Amewatakia mwaka Mpya mwema na kwamba: “Uwe mwaka wa ukuaji wa kibinafsi na pia katika urafiki kati yenu. Kwa Kanisa, 2025 ni mwaka wa Jubilei, kulingana na mapokeo, kila miaka 25 kuna mwaka wa Jubilei. Na Jubilei hii ina kaulimbiu, kauli mbiu ... "Mahujaji wa matumaini." Papa amewaomba wote warudie kwa pamoja kauli mbiu hiyo: "Mahujaji wa matumaini" na aliomba wasema kwa nguvu zaidi ili asikie!
Neno "mahujaji" Papa ameongeza kusema kuwa hutufanya tufikirie kutembea, kwa hivyo alipenda kuwatakia kila wakati kuwa watu walioko kwenye safari. Katika kila umri: watoto, vijana, watu wazima, wazee, daima ni juu ya hoja hiyo , hawakuacha kamwe, hawakufika, daima wamekuwa na hamu ya kusonga mbele. Hata hivyo, "hujaji" si mtu ambaye anatembea tu, bali anayo hatma fulani. Hatma ya mhujaji ni mahali patakatifu, ambapo humvutia, ambapo huhamasisha safari, ambayo inamuunga mkono katika jitihada zake.
Kwa upande wa Jubile lengo ni mlango. Ni jambo la kushangaza amesema Papa. Mlango Mtakatifu. Kwa kawaida ni ishara: Mlango Mtakatifu unamwakilisha Yesu Kristo, Fumbo lake la wokovu, linalotuwezesha kuingia katika maisha mapya, huru kutoka katika utumwa wa dhambi, huru kumpenda na kumtumikia Mungu na wengine. Na kwa hiyo Papa alipenda kuwatakia wasiwe wasafiri tu bali pia wanahija, yaani, kuwa na shauku ya kukutana na Yesu, kumjua, kusikiliza Neno lake ambalo hutoa maana ya maisha, huijaza na mapya, tofauti, na furaha ambayo haibaki nje, na juu ya uso tu, bali ambayo inajaza moyo na kuupasha joto, furaha ambayo ni amani, wema, huruma,” Papa alifafanua
“Furaha ya Yesu iko hiyo Papa amesisitiza na kwamba: “Ni Yesu pekee anayeweza kutoa furaha hiyo. Hili linadhihirishwa na ushuhuda wa watakatifu wengi wa nyakati zote, wakiwemo wetu. Hebu tumfikirie Pier Giorgio Frassati, kijana kutoka Torino aliyeishi miaka mia moja iliyopita. Na kisha kuna "mabingwa" wakuu, kama Francis na Clare wa Assisi, ambao nyote mnawajua; au kama Teresa wa Mtoto Yesu, msichana Mfaransa mwishoni mwa karne ya 19: alikuwa akimpenda sana Yesu, kiasi kwamba alitaka kusafiri ulimwengu mzima kumtangaza kwa kila mtu, na aligundua hiyo njia ya kufanya hivyo, kwamba ajipende mwenyewe, katika maisha yaliyowekwa wakfu kwa maombi na huduma kwa dada zake,” Papa alibainisha.
Papa Francisko kwa njia hiyo alisema kuwa hawa ni “mahujaji wa matumaini:” watoto na vijana ambao wamekutana na Bwana Yesu na kutembea naye, naye ndiye tumaini la kila mwanaume, na kwa kila mwanamke pia kwa ulimwengu. Kwa hiyo tufuate njia hiyo, na sisi pia tutakuwa ishara ndogo za matumaini kwa wale tunaokutana nao.” Papa alihitimidha kwa kusema kuwa haya ndiyo matakwa anayojitakia na kuwatakia wao. Aliongeza Papa kushukuru kwa kufika kwao. Amewabariki wote na kuwaomba watembee kwa furaha, wakati huo huo wasisahau kumwombea.