Papa katika simu ya video na Parokia ya Gaza:"Salamu alaykum,nawaombea"
Vatican News
Saa 1.00 usiku majira ya Italia mara moja, kama kila jioni ya kila siku tangu mwezi Oktoba 9, masaa arobaini na nane baada ya kuanza kwa milipuko ya mabomu katika Ukanda huo wa Gaza hata jioni ya tarehe 22 Januari 2025, Baba Mtakatifu Francisko pia alipiga simu ya video kupitia WhatsApp kwa parokia ya Familia Takatifu huko Gaza, ambayo, kama yeye mwenyewe alivyosema mara nyingi -hata baada ya Katekesi yake Jumatano, kwamba anapiga simu kila jioni ili kuuliza hali ya maisha ya watu zaidi ya 600, Wakristo na Waislamu, wanaopata hifadhi kati ya Parokia na chuo.
“Mlikula nini?"
Uteuzi maalum wa dakika chache, wa kuuliza tu "habari zenu?", Ili kujua ikiwa na wamekula nini, kuona watoto, wazee, kuwabariki na kusalimiana. Huko Gaza ilikuwa ni saa moja mbele, ilikuwa ni saa 2 usiku na kutokana na video hiyo inaweza kuona kwamba kuna baridi, lakini ni baridi tu ya hali ya hewa, si ile ya kifo kinachokaribia ambacho kimetawala kwa karibu miezi kumi na tano; na makubaliano ya amani yameanza kutumika tangu Dominika. Mnamo Januari 12, kila mtu alikuwa nje ili kusherehekea na kushangilia usitishaji huo wa mapigano na simu ya Papa ikawa "sherehe" mitaani, kama Padre huyo wa parokia alivyoambia vyombo vya habari vya Vatican.
Bado hakuna amani lakini watu wanatabasamu tena
“Leo usiku katika boma zima, tumekula kuku! Mabawa ya kuku!”, Padre Yusuf alieleza wakati wa simu hiyo. Yeye ndiye wa kwanza kujibu Papa, akiunganishwa kwa simu ya katibu wake Juan Cruz Villalón. Haikulia mara tano tu kisha mshangao: "Habari za jioni, Baba Mtakatifu!." Alikuwa na sauti ya mtu ambaye utafikiti anamuona na kumsikia Papa kwa mara ya kwanza, lakini Papa Francisko alikuwa amepiga simu si chini ya saa ishirini na nne zilizokuwa zimepita.
Salamu kwa watoto
“Habari yako?” aliuliza. "Sijambo, asante Mungu!", "Na niambie mmekula nini leo?" “Mabawa ya kuku,” alijibu kuhani wa Shirika la Neno lililofanyika Mwili. “Huyo ni Baba Mtakatifu?” Padre Gabrieli aliingilia kati, akisimama karibu naye. “Ni Papa wetu mpendwa!” anapaza sauti kwa watu. Anawaita wote pamoja; watoto, wanaume na wanawake wanafika na mitandio na kofia, katika ua la kiwanja huo. Wanazidi kusogea taratibu. Wa kwanza ni daktari: “Salāmu ʿalaykum,” Papa alimwambia kwa Kiarabu. Huku nyuma, gumzo la wanawake na watoto likisikia. Papa Francisko alitazama kwa furaha, huku akiendelea kupungia mkono kwaheri Karima na watoto wengine: “Bye Bye! Ciao!” “Kwaheri! HII!". Kisha alifanya ishara ya msalaba. Muchas gracias “Asante sana.
Sala ya Papa
“Wanataka kumshukuru, wanamuombea kwa sababu huwa anawaomba kila mara,” alisema Padre Yusuf. "Omba, eh, sio dhidi ya Francisko!" Vicheko, kelele, salamu. "Shukran!", Papa alipaza sauti yake tena kwa Kiarabu. Alitabasamu mwishoni na kutazama skrini ya simu mkononi kwa dakika chache zaidi. Hakuna maneno ya kushangaza, chini ya dakika tano, ya ishara, hata hivyo, ya msingi kwa watu ambao wameishi kwa zaidi ya mwaka kwa hofu, baridi na njaa na ambao hawajui nini kinawangojea katika siku zijazo.
Kumbukeni kwamba Papa mwenye umri wa miaka 88 ambaye anatumia teknolojia mpya kueleza "ukaribu" huo ambao ni moja ya "sifa" za Mungu, kama alivyosema kila mara, pamoja na huruma na upole. Na kutumaini, pia ile ya amani ya uhakika, ya haki, na ya kudumu.
