Hadi kufikia Jumanne tarehe 14 Januari 2025 idadi ya watu waliokuwa wamepoteza maisha ilikuwa ni watu 25. Hadi kufikia Jumanne tarehe 14 Januari 2025 idadi ya watu waliokuwa wamepoteza maisha ilikuwa ni watu 25.  (AFP or licensors)

Moto Wasababisha Maafa Makubwa Los Angeles, Califonia, Marekani

Hadi kufikia Jumanne tarehe 14 Januari 2025 idadi ya watu waliokuwa wamepoteza maisha ilikuwa ni watu 25 na kwamba, idadi hii inaweza kuongezeka kadiri ya muda unavyozidi kusonga mbele. Taarifa zinaonesha kwamba watu 180, 000 wameokolewa na kwamba, moto huu umesababisha miundo mbinu zaidi ya 12, 401 kuharibiwa vibaya sana. Juhudi za uokoaji zinaendelea kupambana hasa kutokana na upepo mkali unaoendelea kuvuma na hivyo kusababisha madhara.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha moto uliotokea Los Angeles na viunga vyake nchini Marekani, tarehe 7 Januari 2025 na hivyo kusababisha maafa makubwa kwa maisha ya watu na mali zao. Hadi kufikia Jumanne tarehe 14 Januari 2025 idadi ya watu waliokuwa wamepoteza maisha ilikuwa ni watu 25 na kwamba, idadi hii inaweza kuongezeka kadiri ya muda unavyozidi kusonga mbele. Taarifa zinaonesha kwamba watu 180, 000 wameokolewa na kwamba, moto huu umesababisha miundo mbinu zaidi ya 12, 401 kuharibiwa vibaya sana. Juhudi za uokoaji zinaendelea kupambana hasa kutokana na upepo mkali unaoendelea kuvuma na hivyo kusababisha madhara makubwa.

Moto umesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao
Moto umesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 12 Januari 2025 amewahakikishia watu wa Mungu Los Angeles huko Califonia uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na kwamba, anawaombea marehemu huruma ya Mungu pamoja na wale wote waliofikwa na msiba huu mkubwa. Katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu José H. Gómez wa Jimbo kuu la Los Angeles, nchini Marekani, Baba Mtakatifu anapenda kutuma salam zake za rambirambi kwa wale wote wanaowaombolezea ndugu zao waliofariki dunia kutokana na janga la moto. Anawaombea majeruhi waweze kupona haraka na hivyo kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Anawaombea wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya kuokoa maisha na mali za watu. Wote hawa anapenda kuwapatia baraka zake za kitume, ili wapate faraja na nguvu za kupambana na janga hili la moto linaloendelea kusababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao huko Los Angeles, Califonia.

Janga la Moto Los Angeles
14 January 2025, 14:13