Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina, tarehe 1 Septemba 2022 amenusurika kifo. Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina, tarehe 1 Septemba 2022 amenusurika kifo. 

Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Anusurika Kifo Nchini Argentina!Papa Atuma Salam!

Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner,, Makamu wa Rais nchini Argentina amenusurika Kifo. Baba Mtakatifu Francisko ametumia fursa hii kwa ajili ya kusali na kuiombea Argentina, ili iweze kurejea tena katika hali ya amani na utulivu wa kijamii, kwa kuheshimu tunu msingi za kidemokrasia, ili ziweze kutamalaki nchini Argentina, dhidi ya aina yoyote ya vurugu, kinzani na mipasuko.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Bwana Fernando Andre Sabag Montiel, mwenye umri wa miaka 35 kutoka Brazil anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini Argentina kwa kufanya jaribio la kutaka kumuua Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina, tarehe 1 Septemba 2022, wakati Makamu wa Rais alipokuwa anarejea nyumbani kwake. Akiwa na lengo la kusalimiana na washabiki na wale wanao muunga mkono pamoja na kutia sahihi kwenye baadhi ya vitabu alivyoviandika mwenyewe, hapo ndipo Bwana Fernando Andre Sabag Montiel, alipochukua bastola na kumfyatulia risasi, lakini kwa bahati nzuri, hakuna risali iliyochomoka kwani badi zilikuwa hazijapelekwa chemba, vinginevyo, leo Argentina ingekuwa inaandika ukurasa mpya wa historia yake. Bwana Fernando Andre Sabag Montiel anafahamika sana kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwani mwezi Machi 2021 alikamatwa kwa kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Amani na utulivu wa kijamii ni muhimu sana nchini Argentina
Amani na utulivu wa kijamii ni muhimu sana nchini Argentina

Katika patshika hii nguo kuchanika, vikosi vya ulinzi na usalama vikafanikiwa kumlinda Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina, sanjari na kumtia pingu Bwana Fernando Andre Sabag Montiel. Baba Mtakatifu Francisko baada ya kupata taarifa hii, amemwandikia Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina, ujumbe wa mshikamano wa kidugu na uwepo wake wa karibu katika kipindi hiki tete. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kwa ajili ya kusali na kuiombea Argentina, ili iweze kurejea tena katika hali ya amani na utulivu wa kijamii, kwa kuheshimu tunu msingi za kidemokrasia, ili ziweze kutamalaki nchini Argentina, dhidi ya aina yoyote ya vurugu na kinzani. Wakati huo huo, Rais Alberto Fernàndes amewaambia wananchi wa Argentina kwamba, hiki ni kitendo kibaya sana kinachotaka kulitumbuka taifa kwenye mgogoro wa demokrasia nchini Argentina uliojitokeza kwenye miaka 1983. Viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka ndani na nje ya Amerika ya Kusini wameonesha mshikamano wao wa kidugu na Dr. Cristina Elisabet Fernández de Kirchner, Makamu wa Rais wa Argentina.

Argentina

 

03 September 2022, 16:12