2026.08.11 Tanzanian President Samia Suluhu Hassan met with the Catholic bishops of the Tanzania Episcopal Conference (TEC) at the Chamwino State House in Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan Akutana na Kuzungumza na Maaskofu Katoliki Tanzania

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayogusia jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa. Aidha mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na viongozi wa dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano wa kitaifa.

Na Ikulu, Chamwino, - Dodoma, Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Chamwino, Dodoma inasema kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Jumatatu tarehe 10 Agosti 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, “Tanzania Episcopal Conference, TEC,” Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma.

Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania   (State House of Chamwino, Tanzania)

 

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayogusia jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.

Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakutana na Rais Samilia
Viongozi wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania wakutana na Rais Samilia   (State House of Chamwino, Tanzania)

Aidha mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na viongozi wa dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa. Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikiana na viongozi wa dini na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.  

Rais Samia na Maaskofu TEC
11 Agosti 2026, 10:17