2026.08.11 Mkutano wa Baraza la Amani,uliofanyika mwishoni mwa Mei huko Mtakatifu Gregori  huko Celio. 2026.08.11 Mkutano wa Baraza la Amani,uliofanyika mwishoni mwa Mei huko Mtakatifu Gregori huko Celio. 

Baraza la Amani,ukimya unaojenga amani

Padre Cyprian Consiglio,Katibu Mkuu wa DIM MID,aliwasilisha Baraza la Amani kwa vyombo vya habari vya Vatican.Baraza hili la kidini katika muktadha wa Monastiki liliundwa ili kuhamasisha mazungumzo na kuchangia amani.Katikati ya uzoefu huo ni urafiki,uelewa wa pande zote na ukimya kama nafasi ya kukutana.Baada ya mafungo ya kwanza huko Roma,washiriki walipokelewa na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini.

Na Fabio Colagrande - Vatican.

Padre Cyprian Consiglio mtawa na Padre Mkamaldoli, katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini (DIM·MID), kwa ajili ya Wamonaki wa kike na Kiume na Mazungumzo ya Kidini alizungumzia juu ya maana ya Mafungo ya Baraza la Amani na baraza dogo la ushauri la kimataifa lililoanzishwa ndani ya Shirika la Kikatoliki linalowaleta pamoja watawa wa kike na kiume wanaoshiriki katika mazungumzo ya kidini.

"Kujionyesha tu kama kundi la marafiki tayari ni ishara katika ulimwengu ulioraruliwa na mgawanyiko, chuki, ujinga, na kukata tamaa,"alisema hayo na  kwamba hili ni Baraza la Amani, la  Wakristo, Wayahudi, Waislamu, Wabudha, Wahindu, Watao, na wawakilishi wa tamaduni za kidini za kiasili: watu kutoka ulimwengu tofauti, walioitwa kutofuta upekee wao, bali kujuana, kusikilizana, na kuhoji mchango ambao uzoefu wa kidini unaweza kutoa kwa amani. "Maneno ya kawaida, msingi wa pamoja, matamanio ya pamoja, mahitaji ya pamoja," Padre Consiglio alikumbuka Nostra Aetate kuwa, "Lazima tupate kile tunachoshiriki, kama 'Nostra Aetate' inavyothibitisha: kutambua, kuhifadhi, na kukuza."

Kutoka kwenye hisia hadi mpango wa amani

Wazo hilo linaanzia Roma hadi kuwasili kwa Padre Consiglio kama Katibu mkuu wa DIM·MID. Miongoni mwa mikutano iliyopendekezwa na mtangulizi wake, Padre William Skudlarek, ilikuwa ni moja na Gianni La Bella wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. "Nilimuuliza alichofikiri nifanye na shirika langu, pamoja na mazungumzo ya kidini ya kitawa, na yeye, bila kusita, aliniambia kwamba ninapaswa kudhamini tukio la kila mwaka, la kimataifa, la kidini ili kujadili na kuomba amani kama urithi wa ulimwengu wote."

Padre alikuwa tayari anafikiria kundi la washauri kutoka tamaduni tofauti za kidini ili kuunga mkono kazi yake. Mawazo hayo mawili hatimaye yaliungana: "Nilidhani itakuwa wazo zuri kwangu kuunda kundi hili, kwa lengo la kubuni na kuandaa tukio hili." Baraza la Amani lilianza kukutana mtandaoni, likiwa na mikutano ya mara kwa mara iliyojitolea kwa maandishi na mada za kidini. Lengo linabaki vile vile kama lilivyokusudiwa awali: kuunda mkutano mpana wa kimataifa na wa kidini ambapo kutafakari na kuombea amani, inayoeleweka kama "urithi wa ulimwengu wote."

Mtakatifu Gregori na Mazungumzo yanakuwa uzoefu

Baada ya mwaka mmoja wa mikutano ya mbali, mwishoni mwa Mei iliyopita kikundi kilikutana kwa mara ya kwanza ana kwa ana katika monasteri ya Camaldoli ya Mtakatifu Gregorio, Celio huko Roma. Zaidi ya mkutano, Padre Consiglio alitaka mapumziko: siku tano za maisha ya pamoja, kutafakari, nyakati za sala ya watawa, mazungumzo, na vipindi sita vilivyoongozwa na mbinu ya Kusikiliza Neno la Mungu. Washiriki kutoka tamaduni zinazotegemea Maandiko waliombwa kuchagua maandishi kuhusu amani ambayo yaliwakilisha imani yao hasa.

"Jambo zuri zaidi kwangu lilikuwa kuona upendo na kujitolea kwao kwa tamaduni zao, shauku yao,  na kwa maandiko yao," Consiglio anasema. Mbinu ya mafunzo ya Kikatoliki ilitumika kama mfumo wa majadiliano: kusoma kwa sauti, kushirikisha neno au kifungu cha maneno, kuelezea maandishi, majadiliano, na hatimaye, ukimya. "Huu ulikuwa wakati muhimu sana kwa sababu si mara zote hufanyika wakati wa mafunzo ya maandishi ya Kimungu kwa pamoja, lakini kila mara tuliishia kwa kutafakari kimya kimya."

Un momento del ritiro a San Gregorio al Celio

Wakati wa Mafungo huko Mtakatifu Gregori, Celio

Ukimya uliopita  zaidi ya maneno

Ukimya wenyewe ukawa mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vya uzoefu. Chaguo hili liliwawezesha washiriki kubaki na mizizi katika utambulisho wao wa kidini, na kuepuka mkutano kuwa mkimya wa maombi. "Tulidhani tulikuwa wa tamaduni tofauti, kila moja akiwa na sifa zake maalum," anaelezea mtawa wa Camaldoli. "Kwa mtazamo huu, ilitusaidia kumaliza mafungo kwa muda wa ukimya, badala ya kusali sala kwa sauti." Kwa Padre Consiglio, ukimya wa kutafakari unaweza kuwa nafasi ambayo kusikiliza hutangulia hitaji la kuunda ufafanuzi wa pamoja: "Zaidi ya maneno, hata kabla ya maneno, kwa sababu ukimya ndio chanzo cha maneno; pia ni kilele cha maneno.

Hii ndiyo mbinu ya kutafakari.” Pia ni kupitia uzoefu huu ambapo mazungumzo kati ya dini yanaweza kuchangia amani. Sio kupitia ukuzaji wa fmtindo wa pamoja hasa, bali kwa kujenga mahusiano na kukuza uelewa mdogo wa imani ya mwingine. “Kwangu mimi, ni kuhusu, kwanza kabisa, urafiki, uelewa mkubwa wa pande zote, uelewa wa kweli wa kiini cha dini ya mwingine, badala ya kudai ukweli tu.”

Kujuana ili Kuondoa Silaha za Ujinga

Katika jamii ambapo watu wa dini tofauti wanazidi kuishi pamoja, Padre Consiglio anasisitiza juu ya jukumu la kujuana. “Siku hizi, ni dhambi kutojua kitu kuhusu dini zingine zinazotuzunguka, hasa kwetu sisi viongozi wa kidini. Kwa Kiingereza, tunaita ‘ujinga unaoweza kuhukumiwa.’ Huu ungekuwa ujinga unaoweza kuhukumiwa.” Anasisitiza kwamba msingi ambao wanakutana hauhitaji kupunguza tofauti za kimafundisho, bali kutambua kile kinachowaunganisha watu hata zaidi ya uhusiano wao:

"Ni mara ngapi tunapata kitu ambacho tayari tunashirikisha kama wanadamu? Msingi ambao hati za mazungumzo hutegemea ndiyo msingi wa ubinadamu wetu." Uzoefu huo mjini Roma ulimalizika mnamo Juni 1 kwa ziara ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini, ambapo kundi hilo lilikutana na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Kardinali George Jacob Koovakad, katibu, Monsinyo Indunil Janakaratne Kodithuwakku Kankanamalage, na maafisa wengine wa Baraza. Hatua ya kitaasisi ambayo Baraza linaita "tukio kubwa, muhimu sana.

 

I partecipanti al ritiro del Peace Council in visita al Dicastero per il Dialogo Interreligioso, in una foto di gruppo con il prefetto, il cardinale George Jacob Koovakad

Washiriki wa mafungo ya Baraza la Amani wakitembelea Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wake, Kardinali George Jacob Koovakad

Kuelekea Mkutano mpana

Sasa Baraza la Amani linaangalia zaidi ya uzoefu wake wa kwanza huko Roma. "Hatua inayofuata sasa ni kufikiria kuandaa tukio kubwa na pana zaidi," anaelezea Padre  Consiglio. Mahali na utaratibu bado haujabainishwa, lakini mpango wa awali unabaki kupanua majadiliano polepole na kuanzisha mkutano wa kimataifa uliowekwa wakfu kwa amani. Mbinu iliyojaribiwa huko Mtakatifu Gregori tayari inaelekeza kwenye mwelekeo unaowezekana: sio kuficha tofauti, bali kuwaruhusu watu waliounganishwa sana na imani yao kukutana, kusikilizana, na kuwa marafiki. Katika wakati uliojaa vita na migawanyiko, hii pia, kwa mtawa wa Camaldoli, ina thamani halisi: kuonesha kwamba kuwa na tamaduni tofauti hakutuzuii kutambua kwa pamoja hitaji la amani.

MAFUNGO YA AMANI KWA DINI TOFAUTI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

12 Agosti 2026, 09:07