Mwezi mmoja baada ya Tetemeko kali huko Venezuela. Mwezi mmoja baada ya Tetemeko kali huko Venezuela.  (ANSA)

Watawa kufungua milango ya elimu baada ya tetemeko la ardhi nchini Venezuela

Mwezi mmoja baada ya tetemeko kubwa la ardhi nchini Venezuela,juhudi za kibinadamu zinaendelea kushughulikia mahitaji ya dharura huku zikiunga mkono urejeshaji wa muda mrefu nchini humo.Shirika la watawa la Wamisionari wa Familia Takatifu ya Nazareti(MHSFN),kwa kushirikiana na CADIS International,wanarejesha upatikanaji wa elimu kwa kufungua tena shule yao ili kuwahudumia wanafunzi waliopo na waliohamishwa.

Na Sr. Christine Masivo, CPS - Vatican.

Mashirika ya kibinadamu yanaendelea kushughulikia mahitaji ya dharura ya watu walioathiriwa nchini Venezuela baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba nchi mwezi mmoja uliopita. Shirika la watawa la Wamisionari wa Familia Takatifu ya Nazareti (MHSFN), kwa ushirikiano na Huduma ya wakamilliani ya Maafa kimataifa(CADIS), pamoja na Huduma ya maafa ya Wacamillian ya Kanda ya Brazil wanaratibu misaada ya dharura huku wakiongoza kampeni ya kuchangisha fedha ili kutoa msaada muhimu kwa familia zilizo katika mazingira magumu.

Elimu ni muhimu kwa juhudi za uokoaji

Pamoja na hatua za dharura, CADIS imeshirikiana na watawa wanapotafuta kurejesha elimu kama jambo muhimu, ni hatua muhimu katika uokoaji wa jamii. Tetemeko la ardhi liliharibu majengo ya shule zaidi ya 400, na hivyo kuvuruga masomo kwa maelfu ya watoto ambao tayari wanaishi katika hali ngumu ya kijamii na kiuchumi.

Watawa kujitolea katika elimu

Licha ya changamoto watawa wa Shirika la watawa la Wamisionari wa Familia Takatifu ya Nazareti, wanajiandaa kufungua tena shule yao ambayo iliharibiwa kiasi huko Caracas Septemba hii huku juhudi za urejesho zikiendelea kufanywa kaskazini magharibi na katikati mwa nchi. Kujitolea kwa watawa hao kunahakikisha kwamba elimu inaendelea kupatikana kwa watoto walioathiriwa na janga hilo. Kulingana na shirika la habari za kimisionari Fides, Watawa hao wanapanga kuendesha shule hizo kwa ratiba ya zamu mbili, huku saa za asubuhi zikihudumia takriban wanafunzi 400 - 600 waliojiandikisha shuleni huku alasiri ikihudumia watoto ambao shule zao katika jamii jirani ziliharibiwa na tetemeko la ardhi. Hii itawaruhusu masista kuwapa watoto fursa za kielimu bila kusubiri ujenzi ukamilike ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaendelea na masomo yao.

Utoaji wa misaada katika changamoto

Operesheni za kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi zinaendelea chini ya hali ngumu. Uwanja wa Ndege wa Caracas kwa sasa, unatumika kama kitovu cha shughuli za dharura, misaada mingi ya kibinadamu inaelekezwa kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Arturo Michelena huko Valencia, na hili ni changamoto kufikisha vifaa kwa mashirika ya misaada kwa wakati unaofaa. Kulingana na takwimu rasmi kama ilivyoripotiwa na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari,(FIDES) baada ya tetemeko la ardhi kaskazini magharibi na katikati mwa Venezuela mnamo tarehe 24 Juni 2026, lilibainisha kwamba watu takriban 5,346 wamepoteza maisha yao, na watu 16,740 kujeruhiwa. Zaidi ya watu 16,300 walipoteza nyumba zao kabisa. Zaidi ya watu 23,000 wanabaki katika makazi ya muda, na Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba hadi watu 50,000 bado wanaweza kuwa wamo chini ya vifusi.

Mahitaji ya kibinadamu bado yanaendelea pamoja na juhudi za watawa wa Shirika la Wamisionari wa Familia Takatifu ya Nazareti, (MHSFN), zinazoonesha jinsi mashirika ya kidini yanavyoendelea kuchangia katika kupona kwa janga hilo kwa kuhakikisha kwamba watoto wanaendelea na elimu ingawa maisha yao yamevurugwa na janga hilo. Ushirikiano wa watawa hawa na CADIS International unaonesha kujitolea kwa vitendo na endelevu kwa kusaidia jamii wanapojenga upya.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

24 Julai 2026, 14:53