2026.07.31  Sr. Jane Wakahiu,LSOSF, PhD,wakibadilishana mawazo na masisita wengine wakati wa Kongamano la Kwanza la Wanasheria Watawa Katoliki barani Afrika 30-31 Julai 2026. 2026.07.31 Sr. Jane Wakahiu,LSOSF, PhD,wakibadilishana mawazo na masisita wengine wakati wa Kongamano la Kwanza la Wanasheria Watawa Katoliki barani Afrika 30-31 Julai 2026. 

Wanasheria Watawa Katoliki waombwa kutoa ushuhuda wa kinabii na kulinda hadhi ya wote

Washiriki karibu 200 walikusanyika katika Kongamano la I la Wanasheria Watawa Katoliki barani Afrika,Nairobi-Kenya Julai 30-31.Kwa mada:“Ushuhuda wa Kinabii,Kulinda kama kielelezo cha Injili.”Sr Wakahiu,LSOSF,Makamu Rais Mshiriki wa Operesheni za mpango na Mkuu wa Watawa Katoliki wa Mfuko wa Conrad N.Hilton alisema:“Ulinzi wa mtu si lazima uwe wajibu wa kisheria tu,bali ni sharti la Injili linalotokana moja kwa moja na amri ya Kristo ya kumpenda jirani.”

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Kongamano la Kwanza la Wanasheria Watawa Katoliki, liliwaleta pamoja watawa wanasheria wa Kanisa na wa kiraia, wakuu wa mashirika, wataalamu wa ulinzi, watafiti, na washiriki wengine waliojitolea katika dhamira ya Kanisa, Jijini Nairobi Kenya ambapo kwa  siku mbili 30-31 Julai lilitoa fursa kwa washiriki kutafakari jukumu la kinabii la wataalamu wa sheria katika kukuza ulinzi, haki, na uwajibikaji ndani ya maisha ya kitawa. Akitoa hotuba kuu, Sr. Jane Wakahiu, LSOSF, PhD, Makamu Rais Mshiriki wa Operesheni za mpango na Mkuu wa Watawa Katoliki wa Mfuko wa Conrad N. Hilton Foundation, aliwakaribisha washiriki na kuelezea shukrani  kwa juhudi zilizowekwa katika kuandaa Kongamano hilo, ambalo ni ishara ya matumaini yenye maana na kujitolea kwa pamoja katika kuimarisha maisha ya kitawa barani Afrika kupitia mazungumzo, ushirikiano, na huduma.

Kongamano la Kwanza la Watawa wanasheria barani Afrika 30-31 Julai 2026,Nairobi Kenya.
Kongamano la Kwanza la Watawa wanasheria barani Afrika 30-31 Julai 2026,Nairobi Kenya.

Shuhuda wa kinabii ni agizo la Injili

Akitafakari mada ya mkutano: “Shuhuda wa Kinabii: Kulinda kama  kielelezo cha Injili," Sr. Wakahiu alielezea kwamba ushuhuda wa kinabii una mizizi katika kuishi kwa uaminifu kwa maadili ya Injili. Inamaanisha kuwa na mshikamano na wale wanaoteseka, kusema ukweli kwa upendo, na kupinga udhalimu kupitia, huruma, upendo na haki ya Mungu. Kwa kutazama   Maandiko, Matakatifu alibainisha kwamba Manabii wa Kibiblia hawakutabiri wakati ujao tu,  bali walitazama wakati uliopo kupitia macho ya Mungu, wakiwapatia sauti wale ambao mateso yao yalipuuzwa huku wakiwaita watu wa Mungu warudi kwenye ukweli na agano. Pia aliakisi uongozi wa kinabii wa wanawake katika Maandiko, wakiwemo Miriam, Deborah, na Anna, ambao maisha yao yalionesha hatua ya ujasiri katika utumishi wa Mungu. Akinukuu changamoto ya Nabii Ezekieli kwa wachungaji walioshindwa kuwatunza wanyonge, wagonjwa, na waliopotea, Sr. Wakahiu aliwaalika washiriki kufanya uchunguzi wa dhamiri kwa uaminifu kuhusu wajibu wao wa kuwalinda wale waliokabidhiwa uangalizi wao.

Ulinzi wa sera na utaratibu

Sr. Wakahiu alisema kwamba ulinzi wa mtu,  si sharti uwe wajibu wa kisheria tu, bali ni sharti la Injili linalotokana moja kwa moja na amri ya Kristo ya kumpenda jirani. Sr. Wakahiu alielezea kuwa ulinzi kama usemi wa vitendo wa kuwalinda watu kutokana na madhara, unyonyaji, na vurugu huku akithibitisha kwamba kila mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Alisisitiza thamani kubwa za familia, jamii, na utunzaji wa pande zote unaopatikana ndani ya jamii za Kiafrika huku akibainisha kuwa kila utamaduni, ikiwa ni pamoja na tamaduni za Kanisa, unahitaji uongofu endelevu katika nuru ya Injili. Aliwahimiza washiriki kutambua na kubadilisha desturi ambazo zinaweza kuficha unyanyasaji kupitia heshima isiyofaa kwa mamlaka, kutoelewana kuhusu utii, utegemezi wa kiuchumi, au hofu ya kuleta aibu kwa familia na jumuiya.

Kukabiliana na unyanyasaji kupitia mabadiliko

Kwa upande wa athari za unyanyasaji, Sr. Wakahiu alisisitiza kwamba unyanyasaji haurudishi kamwe heshima na kwamba desturi za kiutamaduni zenye madhara lazima zipimwe dhidi ya Injili kila wakati. Akikumbuka historia ya mtoto wa miaka kumi na tatu aliyenusurika unyanyasaji wa kijinsia ambaye jamii yake ilipendekeza kitendo kingine cha unyanyasaji kama njia ya kurejesha usawa kati ya familia, alionesha jinsi udhalimu unavyozidisha mateso badala ya kuyaponya. Alitoa changamoto kwa mashirikika ya watawa kuchunguza mawazo na desturi zinazodhalilisha heshima ya wanawake, watoto, na watu wazima walio katika mazingira magumu. Akirejea ripoti ya Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto ya 2024, aliakisi changamoto za ulinzi zinazoathiri mazingira mengi ya Kiafrika, ikiwa ni pamoja na miongozo dhaifu ya kitaifa, usindikizaji mdogo wa walionusurika, wataalamu wa kutosha wa ulinzi, rasilimali duni, na mapengo katika uwajibikaji.

Wanasheria watawa katoliki barani Afrika wakisikiliza hotuba
Wanasheria watawa katoliki barani Afrika wakisikiliza hotuba

Utamaduni wa utunzaji na uwajibikaji

Kulingana na Sr. Wakahiu, unyanyasaji unaenea zaidi ya madhara ya kimwili kwa kuharibu uaminifu, mahusiano, mamlaka, na uhusiano wa mtu na Mungu na jamii. Alibainisha kuwa unyanyasaji unaweza kuchukua mitindo ya kingono, kiroho, kihisia, kisaikolojia, kifedha, au kitaasisi, na akatoa wito wa ulinzi unaozuia madhara kabla hayajatokea badala ya kujibu tu baadaye. Sr hiyo alisisitiza kwamba kulinda kunahitaji kuunda mazingira ambapo watu hupata usalama, uponyaji, na heshima. Malezi ya utawa, yanapaswa kusaidia watawa kutambua majeraha yao wenyewe, kukomaa kupitia uponyaji, na kusindikizana na wengine kwa huruma. Akirejea taswira ya Henri Nouwen ya "mponyaji aliyejeruhiwa," alielezea kwamba maumivu ya kibinafsi yaliyobadilishwa yanaweza kuwa chanzo cha uponyaji kwa wengine.

Wajibu wa siku zijazo

Kwa kumalizia, Sr. Wakahiu alithibitisha kwamba mabadiliko ya utamaduni yanahitaji zaidi ya sera au warsha. Mabadiliko ya kudumu hutokea wakati viongozi wanapoiga tabia tofauti, jamii zinauliza maswali tofauti, ukimya unapeana nafasi kwa ukweli na usindikizaji wa huruma, na waathirika wanagundua kuwa hawatatembea peke yao. Sr Wakahiu alisisitiza ishara za kutia moyo wa matumaini, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa malezi ya ulinzi, ushirikiano kati ya wanasheria wa Kanisa na wa kiraia, utafiti unaotoa taarifa za kinga, mipango ya usaidizi kwa waathirika, na kujitolea kukua katika taasisi za kitawa ili kuimarisha utawala na uwajibikaji.

Pia alielezea kujitolea kuendelea kwa Mfuko wa Conrad N. Hilton kuisadia Kanisa katika malezi ya ulinzi, utafiti, usaidizi kwa waathirika, mipango ya kurekebisha malalamiko, uimarishaji wa utawala, na ushirikiano unaojenga jamii salama zaidi. Akiomba mwongozo wa Roho Mtakatifu na maombezi ya Bikira Maria, aliwahimiza washiriki kukumbatia dhamira yao ya pamoja ya kuwa "Miali Hai ya Upendo wa Mungu na manabii wa kweli wa wakati wetu" katika kutumikia Kanisa na jamii.

Hatimaye Kongamano la Watawa wanasheria limefanyika huko Nairobi Kenya 30-31 Julai.
Hatimaye Kongamano la Watawa wanasheria limefanyika huko Nairobi Kenya 30-31 Julai.
Wanasheria watawa na Sr Jane Wakahiu

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

 

31 Julai 2026, 18:11