2026.05.29 Medjugorje 2026.05.29 Medjugorje 

Medjugorje:Uharibifu wa eneo la Ibada kwa Bikiria Maria Julai 28

Kuhusu uharibifu uliotokea usiku wa tarehe 28 Julai 2026,Ofisi ya Kiparokia ya Eneo la Ibada kwa Bikira Maria huko Medjugorje inatoa wito wa maombi,msamaha na kufunga baada ya madhabahu ya nje ya Kanisa la Mtakatifu Yakobo kuchomwa moto na kusababisha uharibifu mkubwa.Sanamu ya Bikira Maria pia iliharibiwa.Nafasi hizo zimesafishwa na zinafaa tena kwa ibada kulingana na taarifa kutoka ofisi hiyo hiyo.

Vatican News

Kitendo kikubwa cha uharibifu kilifanyika usiku kati ya Jumatatu na Jumanne (27-28 Julai)katika Madhabahu ya Bikiria Maria wa Medjugorje, huko Bosnia na Herzegovina. Mtu, ambaye bado hajatambuliwa, alimwaga mafuta yanayowaka kwenye madhabahu ya nje ya Parokia ya Mtakatifu Yakobo na kuwasha moto, na kusababisha uharibifu mkubwa. Kisha mtu huyo huyo aliharibu sanamu ya Maria na kuandika michoro ya kukera.

Kusafisha na kutengeneza maeneo yaliyoharibiwa

Katika taarifa, Ofisi ya Parokia ya Medjugorje ilitangaza kwamba imeanza kusafisha na kutengeneza mara moja ili kufanya maeneo yote yafae kwa sala tena. Kwa hivyo mahali pa madhabahu  panaendelea kuwa wazi kwa mahujaji wote, na waamini wanaalikwa kujibu tukio hili la kusikitisha kwa maombi, kufunga, na msamaha: "Tuombe kwa ajili ya uongofu wa mioyo ya wale waliofanya kitendo hiki, ili Bwana awaguse kwa neema yake na kuwaongoza kwenye njia ya wema."

Medjugorje imekuwa eneo la sala ya waamini kutoka ulimwenguni kote
Medjugorje imekuwa eneo la sala ya waamini kutoka ulimwenguni kote

Kutoa ushuhuda kwa maisha kwa upendo, msamaha, na matumaini

Habari za uharibifu huo zilisomwa "kwa majuto makubwa,"taarifa hiyo inaendelea, ikiwashukuru wote wanaofanya kazi kuhakikisha kwamba mahali patakatifu panabaki kuwa mahali pa kukutana na Mungu, mahali pa amani, na mahali ambapo Bikira Maria, Malkia wa Amani, anaheshimiwa. Mbali na kufunga na kusamehe, ofisi ya Parokia pia inatoa mwaliko wa kuomba "kwa ajili ya amani mioyoni mwa kila mtu," kwa sababu "Mama yetu anatuita kila mara kuwa wabebaji wa amani." Tukio hili linaweza hata "kututia moyo kuchukua wito wake kwa uzito zaidi: si kujibu uovu kwa uovu, bali kushuhudia kwa maisha yetu kwa upendo, msamaha, na matumaini."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

28 Julai 2026, 16:47