Maandalizi ya Roazari kwa ajili ya Hija ya Papa Leo XIV huko Hispania Maandalizi ya Roazari kwa ajili ya Hija ya Papa Leo XIV huko Hispania 

Rozari zilizotengenezwa na watawa wa ndani ili kumsindikiza Papa nchini Hispania!

Shirika la Watawa kumi wa ndani wametengeneza maelfu ya Rozari kwa ajili ya Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV nchini Hispania kuanzia 6-12 Juni 2026.Vitu vidogo vilivyotengenezwa kwa mikono vinatokana na ukimya wao,sala,kazi za mikono na msaada wa vijana wa kujitolea.

Na Silvina Pérez

Matumaini yaliyotengenezwa kwa shanga za mbao, ikiwa ni kazi ya mikono katika ukimya,  inapenya kwa ukimya nchini Hispania siku hizi. Mwanzo wake ni katika nyumba za watawa wa ndani zilizosambazwa huko Castilia, Navarre, Catalonia, na Andalusia, zinafikia umati wa mahujaji wanaomsubiri Baba Mtakatifu Leo XIV. Ni Kazi ya uzi wa na shanga ya rozari: hazina ndogo ndogo zilizoundwa katika ukimya wa nyumba za watawa wa ndani, na kuwa moja ya alama zenye maana zaidi za kusindikiza  ziara ya Papa. Nyuma ya kila shanga kuna maisha yaliyofichwa, sauti ya chini na ya unyenyekevu, kazi ya upendo ambayo haitaonekana kamwe katika ratiba rasmi au picha za televisheni.

Hata hivyo, ni katika nyumba hizo za watawa ambapo mtu anaweza kuona ulimwengu ambao hapo awali Hispania uliujua kwa undani na sasa unaonekana karibu kusahaulika. “Katika nchi yetu, kuna zaidi ya monasteri mia saba. Sisi ni mmojawapo wa hali halisi kubwa za monasteri duniani," alielezea Alejandro Simón wa Mfuko wa Kutafakari, ambao ni mtandao kwa miaka mingi umesaidia Jumuiya za Watawa wa ndani kujiendeleza kupitia kazi za ufundi na, zaidi ya yote, kupitia uhusiano wa kiroho waliouanzisha na wale wanaowatembelea na kugundua uzuri uliofichwa unaopatikana ndani ya monasteri.”

Kushiriki katika hija ya Papa

Monasteri hazijatengwa na ulimwengu, badala yake, zipo nje ya mantiki kuu ya ulimwengu wa haraka na kelele. Monasteri zinabaki pembezoni mwa kelele za kisiasa na kijamii. Na bado, kwa kushangaza, kupitia maandalizi ya ziara ya Kitume ya  Papa, ghafla zimerejesha umakini. Wazo la kutengeneza  Rozari lilikuwa la kawaida: kitu rahisi na cha unyenyekevu kinachoweza kumsindikiza Papa Leo XIV katika Ziara yake ya Kitume. Mfuko chama cha Watawa wa ndani ulianza kuwasiliana na monasteri nchini  kote,  kuuliza kama ingewezekana kutoa Rozari elfu kadhaa katika majuma kadhaa tu. Jibu lilikuwa la haraka. "Wote walijibu  ndiyo, sio kwa sababu ya ukubwa wa ombi, ambalo ni kubwa kwa Jumuiya yenye wanashirika wachache sana, lakini kwa sababu walielewa kwamba hii ilikuwa njia ya kushiriki katika hija ya Papa,” Simon alieleza. “Tangu wakati huo, mwelekeo wa kazi ndani ya monasteri umebadilika. Ndani ya karakana ya mishumaa na ubani na ya manukato ya mbao, katika vyumba vya ushonaji na sehemu ndogo za ufundi, watawa wa ndani wote wa kike na wa kiume wameongeza muda wa kazi. Baadhi hukusanya shanga moja baada ya nyingine, wengine huandaa misalaba au mifuko midogo ya kitambaa ambayo itatumika kusambaza Rozari hizo.

Mchango wa Watu wa kujitolea

Katika Monasteri nyingi, vijana wa kujitolea wamefika kusaidia. Wanafunzi wa vyuo vikuu, familia, na vikundi vya Parokia wamevuka vizingiti vya nyumba ya watawa wa ndani zilizofungwa ili kushirikiana kwa ukimya na Jumuiya ya kitawa. Kwa wengi wao, imekuwa mkutano wao wa kwanza wa moja kwa moja na maisha ya watawa wa ndani. "Wanagundua ulimwengu ambao hawakuujua, ulimwengu ambao una mwelekeo tofauti, mahali ambapo kazi hufanywa bila wasiwasi, na ambapo ukimya si utupu bali uwepo,” alifafanua Simon. Rozari si vitu vya kifahari. Nyingi zimetengenezwa kwa mbao rahisi, kamba, na misalaba midogo ya chuma. Lakini ni katika urahisi huo ndipo thamani yake ipo. Kila moja ya Rozari inahitaji uvumilivu  na  muda kuitambua katika sala na kujitolea, ambako kumejificha kwa yule anayetengeneza.

Kwa Jumuiya za watawa wa ndani, ziara ya Papa imekuwa zaidi ya tukio la kitaifa. Ni fursa ya kuikumbusha Jamii kwamba maisha ya watawa wa ndani bado yapo, na mara nyingi katika ukimya, kwa siri, na kwa shida, lakini bado yapo hai yanaendelea. Monasteri nyingi nchini Hispania zinashughulikia masuala yanayotokana na jumuiya zinazozeeka, ugumu wa kiuchumi, na ukosefu wa miito. Baadhi ya Monasteri zimelazimika kufungwa katika miaka ya hivi karibuni. Nyingine bado zipo kutokana na kuuuza pipi, ushonaji wa maua, uchoraji wa picha  za Kanisa, utengenezaji wa sabuni, au bidhaa zingine zilizotengenezwa kwa mikono.

Mtandao wa maombi

Na bado, licha ya udhaifu wao, Monasteri hizi zinaendelea kudumisha mtandao usioonekana wa maombi ambayo waamini wengi, bado wanaona kuwa muhimu. “Kuna watu wanaotuomba maombi kila mara,"Simón alisema. "Kwa magonjwa, hali za kifamilia, ukosefu wa ajira na upweke. Monasteri hubeba mzigo mkubwa wa kiroho ambao mara nyingi hubaki bila kuonekana." Kwa sababu hiyo, Rozari zilizoandaliwa kwa ajili ya ziara ya Papa ni zaidi ya vitu rahisi vya ibada. Pia ni ishara ya uwepo uliofichwa wa maisha ya watawa wa ndani katika Kanisa na katika jamii.

Katika siku zijazo, maelfu ya mahujaji watapokea moja ya rozari hizi mikononi mwao. Na wachache watajua zilitoka wapi. Wachache watafikiria ukimya wa monasteri,  kazi ya uvumilivu ya mikono ya wazee, au mazungumzo ya utulivu yaliyoambatana na utengenezaji wake. Lakini katika kila rozari kutabakia kitu cha ulimwengu huo uliofichwa: sala ya watawa wa ndani ambayo, kutoka nyuma ya kuta zao, inaendelea kusindikiza safari ya Kanisa.

Imesasishwa tarehe 2 Juni 2026 saa 5.01 asubuhi na Angella Rwezaula.

Rozari papa Hispania

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

02 Juni 2026, 11:00