Askofu Emmanuel Badejo,Nigeria Askofu Emmanuel Badejo,Nigeria  

Nigeria:Ask.Badejo arudia wito wa Papa katika uwajibikaji na vyombo vya kidijitali

Askofu Badejo wa Jimbo Katoliki la Oyo nchini Nigeria alirudia ujumbe wa Papa Leo XIV wa Siku ya 60 ya Hupashanaji Ulimwenguni kuwa hautenganishi.Alisema haya baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana cha Roma kuhusu:"Kuhifadhi sauti na nyuso za binadamu"hivi karibuni mnamo 21 Mei 2026.

Na Paul Samsumo – Vatican.

Akitafakari ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya 60 ya hupashanaji Ulimwenguni, Askofu Emmanuel Adetoyese Badejo wa Jimbo Katoliki la Oyo nchini Nigeria alisema mada ya "Kuhifadhi Sauti na Nyuso za Binadamu," ni onyo la wakati unaofaa ambalo ulimwengu unahitaji kusikia na ambalo "linaonesha wasiwasi wa Papa kwamba tunapaswa kuzingatia jukumu linalopungua la nyuso na sauti ya binadamu katika mahusiano ya kisasa ya mawasiliano ya kijamii." Alisema hayo mara baada ya Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana Roma kuhusu mada ya:"Kuhifadhi sauti na nyuso za binadamu" uliofanyika mnamo tarehe 21 Mei 2026.

Mawasiliano lazima yakuze ushirika

"Mawasiliano halisi lazima yakuze ushirika na Mungu na na wanadamu wenzetu. Mawasiliano mabaya hufanya kinyume kabisa, na kusababisha mgawanyiko, msongo wa mawazo na migogoro," alisema Askofu huyo wa Oyo nchini Nigeria, ambaye pia ni mtaalamu wa mawasiliano na vyombo vya habari. Mawasiliano, Askofu Badejo alisema, hayapaswi kamwe kuwatenga au kuwatenganisha wenzetu, hata wakati migogoro inapotokea. Kwa maneno mengine, mawasiliano hayapaswi kamwe kuwatenga wengine. Ujumbe wa Siku ya Hupashanaji Ulimwenguni unakusudiwa "kutusaidia kusawazisha Imani, Ubinadamu na Uwepo wa Kidijitali katika mahusiano yetu ya kila siku," alisisitiza.

“Epuka kudhalilisha vyombo vyote vya habari vya kidijitali”

Askofu Badejo alionya zaidi dhidi ya utegemezi mkubwa wa teknolojia za kidijitali na kile alichokiita "Akili unde." Utegemezi mkubwa wa teknolojia, alisema, unaweza kudhuru familia, urafiki, na mahusiano ya kijamii. Hata hivyo, Askofu alionya dhidi ya kudhalilisha vyombo vya habari vya kidijitali au Akili Unde(AI). Badala yake alitoa wito wa "ushirikishwaji unaowajibika na uelewa wa vyombo vya habari." "Ni kwa kuhifadhi sauti na nyuso za wanadamu katika jamii yetu pekee ndipo tunaweza kuhakikisha urejesho wa ubinadamu wa ulimwengu wetu, ambao kwa njia nyingi umedharauliwa sana," Askofu Badejo alisema.

ASKOFU BADEJO,NIGERIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

02 Juni 2026, 16:04