2026.06.16:Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Ziara ya Papa nchini Uhispania 2026.06.16:Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Ziara ya Papa nchini Uhispania 

Kanisa la Hispania:Ziara ya Papa Leo XIV ilifanikiwa kutokana na ushiriki wa kila mtu

Juni 16 rais wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya ziara ya Papa nchini Hispania alitoa tathmini ya ziara ya Papa Leo XIV katika mkutano na waandishi wa habari.

Vatican News

Ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Leo XIV iliyoanza  tangu tarehe 6 Juni  huko Madrid na kumalizika tarehe 12 huko Tenerife, Papa alitembelea majimbo matano ya Hispania kuanzia:  Madrid, Barcelona, ​​​​ San Feliu de Llobregat, Canarias y San Cristóbal de La Laguna. (Mtakatifu Feliu de Llobregat), (Kanari na Mtakatifu Cristóbal wa ghuba.) Huo ulikuwa ni mwanzo wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Baraza la Maaskofu wa Hispania ambayo ilitaarifa kufanyika kwa Mkutano wa waandishi wa habari tarehe 16 Juni 2026 ili kufafanua zaidi juu ya tukio la ziara ya Baba Mtakatifu nchini Hispania.

Tathimini ya ushriki kwa mamlaka zote

Katika hotuba yake,Askofu Mkuu  Luis Javier Argüello García, Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV alitoa shukrani kwa Papa kwa ziara yake na kwa watu wa Hispania, hasa Wakatoliki, kwa makaribisho yao. Aliakisi kazi ya timu ambazo zimefanya kazi, katika majimbo na katika maandalizi kitaifa, na kuwashukuru waandishi wa habari walioidhinishwa kwa "matokeo  ya  maeneo mengi ulimwenguni shukrani kwa vyombo vya habari." Pia alithamini sana ushiriki wa mamlaka zote za umma katika aina zake mbalimbali: mamlaka za kitaifa, kikanda, na za mahalia, pamoja na vikosi vya usalama vya serikali.

Kujibu maswali ya kibinadamu

Kwa Askofu Mkuu  Argüello alisema kuwa “ziara hiyo ilikuwa ya moyo: kuona uinjilishaji wa Kanisa ukitenda kazi. Neno lilitangazwa, liturujia ilisherehekewa, na upendo uliinuliwa." Kama alivyosema, ukweli huu wa utume wa Kanisa hufanya kazi kama vyombo vilivyounganishwa, ili pasiwepo tangazo bila upendo, au sherehe bila Neno kutangazwa. Rais wa Baraza la  Maaskofu wa Hispania aliendelea, kusisitiza kwamba Baba Mtakatifu "alitualika tutazame msalaba, msalaba ulioangazwa," na pia alitaka kushughulikia maswali ya kibinadamu ili kujibu maswali hayo makubwa ya ubinadamu katika wakati wetu.

Mapendo,wema na changamoto

Kwa hivyo, alisema kwamba mwingiliano mwingi wa Papa Leo XIV nchini Hispania uliandaliwa na kuongozwa na waraka wa Magnifica Humanitas, ambao aliwasilisha  Juma chache zilizopita. Askofu Mkuu Argüello alikumbuka kwamba Papa aliwaambia, "Sasa ni zamu yenu," na akabainisha kuwa hii ndiyo changamoto kubwa. Baada ya wakati huu wa hisia kali, ni muhimu kuzishughulikia kupitia akili na kuzibadilisha kuwa vitendo: "Kubadilisha hisia kuwa wema. Ruhusu mapendo na busara viwe kujitolea. Humo ndimo changamoto ya kusindikizana," Askofu mkuu Argüello akihitimisha hotuba yake kwa kusema, "Tulichopitia Juma hili ni kitu ambacho hakuna mtu anayeweza kutuondolea, na ni sababu ya kutoa shukrani."

MAASKOFU WA HISPANIA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

17 Juni 2026, 10:01