Wanawake wa Miao nchini India wakisali. Wanawake wa Miao nchini India wakisali. 

Kanisa nchini India:Siku ya Maombi Dhidi ya Mgogoro wa Ufadhili

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India (CBCI)linawaalika waamini wote mnamo Juni 28 kuadhimisha Siku ya Maombi ya Kitaifa.Kiini cha tukio hilo ni wasiwasi wa muswada unaorekebisha kanuni za ufadhili wa kigeni,ambao Kanisa linaamini unaweza kuathiri shughuli za kielimu,huduma za afya na upendo nchini humo.

Vatican News

Baraza la Maaskofu Katoliki nchini India (CBCI) limetangaza Siku ya Kitaifa ya Maombi Dominika tarehe 28 Juni 2026, likiwataka Wakatoliki wote nchini kuungana kiroho licha ya wasiwasi uliotolewa na Muswada wa Marekebisho ya Sheria wa Udhibiti wa Michango ya Kigeni (FCRA) kwa 2026. Hatua hii ya kisheria, ambayo itawasilishwa hivi karibuni katika Bunge la India kwa ajili ya kuzingatiwa, inaweza kuwa na athari kubwa kwa kazi ya kijamii na kichungaji ya Kanisa, kulingana na uongozi wa Kikatoliki.

Wito wa Baraza la Maaskofu  

Mpango huo ulitangazwa katika mkutano na kusainiwa na Rais wa Baraza hilo (CBCI), Kardinali Anthony Poola, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Hyderabad, na kuelekezwa kwa maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na waamini wote wenye mapenzi mema. Katika hati hiyo, Kardinali anaalika jumuiya ya Wakatoliki kuombea taifa, mamlaka za umma, na ulinzi wa uhuru wa Kanisa ili kuendelea na dhamira yake ya kuhudumia jamii.

Hatari kwa Kazi za upendo

Marekebisho yaliyopendekezwa ya kanuni zinazosimamia michango ya kigeni yamezua wasiwasi, hasa kuhusu athari zinazowezekana kwa shughuli za upendo, elimu, afya, na kijamii zinazoendelezwa na Makanisa na taasisi za Kikristo India yote. Maaskofu wanaogopa kwamba kanuni mpya zinaweza kuathiri vibaya kujitolea kwa Kanisa mahalia, ambalo kwa miongo kadhaa limewaunga mkono mamilioni ya watu, hasa miongoni mwa makundi yaliyo katika mazingira magumu zaidi ya idadi ya watu. Kazi hizi, Kardinali Poola alisisitiza, zinawakilisha ushuhuda thabiti wa maadili ya kiinjili ya upendo, haki, na huruma. Kwa sababu hiyo, uwezekano wa kuanzishwa kwa vikwazo vipya unaibua maswali na wasiwasi miongoni mwa jumuiya za Kikristo.

Siku ya Kitaifa ya Maombi

Rais wa CBCI aliwaalika waamini kuadhimisha siku hiyo  kwa roho ya imani, umoja, na ushirikiano wa kiekumene, pia ikihusisha Makanisa na madhehebu mengine ya Kikristo. Kwa lengo hili, maaskofu wa India wanawaalika waamini wote kuongeza muda wa sala ya kijumuiya, kushiriki katika kusali Rozari na ibada ya kuabudu Ekaristi, kufanya mafungo ya kiroho kwa hiari kama ishara za kumwamini Mungu na ushiriki wa uwajibikaji katika maisha ya nchi.

Mtazamo wa kiekumene na kitaifa

Mwongozo huo unahimiza majimbo, parokia, taasisi, na jumuiya za kitawa kuandaa mikutano ya maombi ya kiekumeni, iliyo wazi kwa ushiriki wa vikundi vingine vya Kikristo. Wakati huo huo, aina ya maonesho ya kidemokrasia na ya amani kwa ajili ya  wasiwasi pia yanapendekezwa: maandalizi ya kumbu kumbu hiyo lazima itumwe serikali kuu kupitia wabunge na wawakilishi wa mabaraza ya wabunge wa ndani. Nyaraka hizi, zilizosainiwa na waamini na watu wenye mapenzi mema, zinalenga kuakisi matokeo yanayowezekana ya mageuzi katika shughuli za kikanisa.

Kukabidhiwa Bikira Maria

Akikumbuka maneno ya Mtakatifu Paulo katika Barua yake kwa Wafilipi: "Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila jambo, kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, mjulisheni Mungu haja zenu," Kardinali Poola aliwasihi Wakatoliki kubaki imara katika imani na kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya amani, haki, maelewano ya kijamii, na manufaa ya taifa. Akiikabidhi India na Kanisa kwa maombezi ya mama Bikira Maria, anayeheshimiwa kama Malkia wa India, Baraza la Maaskofu wa Italia (CBCI) hatimaye limeomba kwamba waraka huo utafsiriwe katika lugha za wenyeji na usomeke katika makanisa yote na vituo vya misa ya Dominika tarehe 21 Juni 2026, ili waamini wengi iwezekanavyo waweze kushiriki kikamilifu katika Siku ya Maombi ya Kitaifa mnamo Juni 28.

Kanisa la India:Maombi Juni 28

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

18 Juni 2026, 13:53