2026.05.11 Askofu Mkuu Amani wa Jimbo Kuu la Arusha,Tanzania akiweka mashada ya maua kwenye makaburi ya wahanga 3 wa bomu la Mei 5,2013. 2026.05.11 Askofu Mkuu Amani wa Jimbo Kuu la Arusha,Tanzania akiweka mashada ya maua kwenye makaburi ya wahanga 3 wa bomu la Mei 5,2013. 

Ask.Mkuu Amani:"Maisha ya Mkristo ni kujisadaka na kumdhihirisha Kristo kwa Matendo"

Siku kuu ya Mtakatifu Yosefu mfanyakazi,kuzindua Kikanisa cha kuabudia,siku kuu ya Mama na kumbukizi ya mlipuko wa mabomu ndani ya Kanisa mnamo 5 Mei 2013,yalikuwa ni kiini cha mahubiri ya Askofu Mkuu Amani wa Jimbo Kuu la Arusha,Tanzania wakati wa misa Takatifu ya Dominika ya Sita ya Pasaka,Mei 10 katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi huko Olisti,Arusha.

Na Sr.Ernestina Patrick Lasway, SAC - Tanzania. 

Mhasham Askofu Mkuu Isaac Amani wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha nchini Tanzania, aliongoza Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya Sita ya Pasaka katika Parokia ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi huko Olasiti, jimbo Kuu la Arusha,  tarehe 10 Mei 2026. Misa hiyo iliunganisha matukio kadhaa ya kumbukumbu kama vile:  kumbukizi ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi,  msimamizi wa Parokia hiyo,  uzinduzi rasmi na kubariki Kikanisa kidogo cha “Nazareth,“ cha  kuabudia, kama kituo cha hija, Siku ya Mama Ulimwenguni na kumbukumbu ya mlipuko wa Bomu, uliotokea miaka kumi na tatu iliyopita. Ni katika muktadha huo ambapo Askofu Mkuu wa Jimbo hilo alitoa wito kwa waamini kuwa waaminifu katika imani, ujasiri na kufuasa maisha ya Mtakatifu Yosefu.

Askofu Mkuu Amani akiongoza misa katika Parokia ya Olasiti huko Arusha,Tanzania]
Askofu Mkuu Amani akiongoza misa katika Parokia ya Olasiti huko Arusha,Tanzania]

Kumwabudu Yesu katika kimya

Askofu Mkuu Amani kwa njia hiyo alibariki na kuzindua Kikanisa cha “Nazareth“ mahali ambapo waamini wataweza kumwabudu Yesu wa Ekaristi katika ukimya kila siku. Kila mkristo alialikwa kufika katika kikanisa hicho kidogo cha kuabudia na kikanisa cha hija chenye makaburi matatu ya wakristo waliofariki wakati wa mlipuko wa mabomu, katikati ya adhimisho la kutabaruku Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi mnamo tarehe 5 Mei 2013. Askofu Mkuu Amani alisema, “Kila mmoja analo hitaji la kumshirikisha na kumuomba Kristo, aliye katika fumbo la Ekaristi Takatifu.

Misa katika Parokia ya Olasiti, Arusha, Tanzania
Misa katika Parokia ya Olasiti, Arusha, Tanzania

Siku ya Mama: Malezi ni Tunu Msingi 

Akiangazia siku ya akina Mama ulimwenguni,  iadhimishwayo kila ifikapo Mei 8 ya kila mwaka, Askofu Mkuu Amani aliwataka wazazi kuwa karibu na familia na watoto wao kwa malezi na majiundo ya kiroho na kimwili. Wazazi wote wana jukumu la kuwalea watoto kwa upendo kama Mtakatifu Yosefu na Mama Bikira Maria. Katika siku hii muhimu ya “wakina mama“ kwa kuwashukuru na kuwaombea akina mama wote, wakubwa kwa wadogo na alikemea mila na desturi zenye kuwadhalilisha watoto na akina mama. "Tuwashukuru kwa ukarimu na ujasiri wa kutuleta duniani na kutuleta kwa upendo," Askofu Mkuu alisisitiza.

Misa katika Parokia ya Olasiti huko Arusha, Tanzania kuongozwa na Askofu Mkuu Amani
Misa katika Parokia ya Olasiti huko Arusha, Tanzania kuongozwa na Askofu Mkuu Amani

Ushuhuda katika Yesu Kristo Mfufuka

Askofu Mkuu Amani alisema,  "wakristo wawe mashuhuda wa imani katika Kristo Mfufuka na kwenda kwenye vijiji vingine ili kumpeleka Kristo kwa mataifa kwa kulisikia neno la Mungu na kuliishi kwa matendo kama alivyofanya Philipo katika Maandiko Matakatifu. "Kama mashuhuda wa ufufuko, kila mmoja analo jukumu la kumuishi Kristo kwa matendo." Pasaka kama zawadi ya ufufuko inatualika kuwa "Wakristo wanaoishi furaha ya ufufuko, hata katikati ya changamoto na majaribu ya maisha." Maisha ya fadhila na uaminifu katika kazi, utume na shughuli za kila siku ni njia ya kumfunua Kristo kwa matendo.

Zawadi ya Roho Mtakatifu na Mateso kwa Ajili  ya Kristo

Kwa nguvu ya roho Mtakatifu Askofu Mkuu Amani alisisitiza "Mkristo anaimarishwa kuwa shuhuda wa Kristo kwa maneno na matendo yetu. Zawadi hii ni upendo wa Mungu kwa mwanadamu unaomwezeesha mwanadamu kuona na kutenda kama anavyostahili." Kwa mfano wa maisha ya jumuiya ya kwanza ya mitume, "Mkristo leo hii anaalikwa kuishi kwa upendo na amani katika familia na jumuiya, huku tukitafuata suhulisho kwa changamoto na magumu katika familia na wala siyo kuisambaratisha familia kwa ajili ya changamoto yoyote."

Kupelekwa Yesu katika Kikanisa cha Kuabudia
Kupelekwa Yesu katika Kikanisa cha Kuabudia

"Umoja, mshikamano na upendo, ni msingi wa maisha ya ukristo," alisisitiza Askofu Mkuu. Zawadi ya roho Mtakatifu "ni zawadi kwa wanaompenda Yesu Kristo mfufuka. Hii ni zawadi ya milele, ni msaidizi katika maisha ya Mkristo, yeye ni mshauri wa maisha ya kiroho na kimwili wa maisha ya Mkristo, ambaye  analo jukumu la kumtumia vizuri na kuzaa matunda katika Imani," Alikazia Askofu Mkuu.

Kupelekea Yesu katika Kikanisa kipya cha Kuabudia
Kupelekea Yesu katika Kikanisa kipya cha Kuabudia

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu yanamtia nguvu Mkristo

Kwa njia ya mapaji saba ya Roho Mtakatifu aliyoyapokea Mkristo, anapata nguvu ya kumshuhudia na kumuishi Kristo katika hali zote. "Kudhulumu ukristo siyo kurudisha ukristo nyuma, bali ni mbegu inayomea kati yetu. Hata katika mateso, Mungu yupo pamoja nasi." Kwa njia hiyo Petro, katika somo la Pili, "anatualika kuwa waaminifu katika imani."

Yesu wa Ekaristi katika Kikanisa cha kuabudia
Yesu wa Ekaristi katika Kikanisa cha kuabudia

Kwa njia hiyo "Maisha ya Mkristo yawe na ukaribu na Kristo, na utayari wa kukabidhiana na changamoto za kibinadamu kama magonjwa, na dhambi, ugomvi, uadui, kutosameheana." Kukosana na mpendwa wako na kushindwa kumsameheni ni “sawa na mtu kuweka misumari kwenye kiatu “alibanisha Askofu Mkuu, huku akiwahimiza "Wakristo umuhimu wa kusamehe, hasa katika maisha ya ndoa."

Kuabudu Yesu katika Kikanisa Kipya cha kuabudia
Kuabudu Yesu katika Kikanisa Kipya cha kuabudia

Mlipuko wa mabomu:watu watatu walikufa 5 Mei 2013

Akirejea katika mlipuko wa mabomu uliotokea wakati wa adhimisho la Misa Takatifu la kutabaruku Kanisa Olasiti,  nje kidogo ya mji wa Arusha, Tanzania Dominika asubuhi tarehe 5 Mei 2013, Askofu Mkuu Amani alisema kuwa "damu ya Wakristo imeendelea kuwa mbegu ya imani yao." “Ushuhuda wa imani unadhihirishwa kwa Wakristo wa Parokia hii kwa kuwepo wafiadini watatu wakati wa kumbukizi ya sherehe za kutabaruku Kanisa la Parokia hii.”

Kikanisa chenye makaburi ya wahanga wa bomu lililotokea Mei 5,2013
Kikanisa chenye makaburi ya wahanga wa bomu lililotokea Mei 5,2013

Kuhusiana na tukio hilo,  watu kadhaa walijeruhiwa,  huku Balozi wa Vatican, mapadre na watawa waliokuwa katika shughuli hiyo maalum ya kuzindua Parokia mpya wakanusurika. Mlipuko huo ulitokea wakati wanajiandaa kubariki maji kwa ajili ya uzinduzi wa Kanisa, ambapo hafla hiyo ilikuwa ikiongozwa na Balozi wa Vatican. Kwa bahati mbaya watu watatu walikufa na wengine waliojeruhiwa walikimbizwa hospitali ya Mount Meru mjini Arusha na kupata matibabu na kurudi nyumbani. Katika kuwakumbuka, walizikwa hapo hapo ambapo kikanisa kimekuwa cha hija kama ushuhuda wa imani. Wahanga watatu waliofariki hapo siku ya mlipuko ni:  Regina Long'o Laizer (1963-2013) mama wa familia,  James Gabriel Kessy (1997-2013) pamoja na Patricia Joachim Assey (2003 - 2013) pacha aliyefariki na na mwenzake  Patrici akanusurika katika mlipuko huo. Furaha ya Milele uwape ee Bwana.

Wahanga 3 wa mlipuko wa bomu katika Parokia ya Olasiti huko Arusha nchini Tanzania
Wahanga 3 wa mlipuko wa bomu katika Parokia ya Olasiti huko Arusha nchini Tanzania

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

10 Mei 2026, 15:38