Sr. Kakali (katikati) akiwa na wanafunzi katika shule ambapo anatoa semina kuhusu afya ya akili (picha na mwalimu shuleni hapo). Sr. Kakali (katikati) akiwa na wanafunzi katika shule ambapo anatoa semina kuhusu afya ya akili (picha na mwalimu shuleni hapo). 

Saikolojia na Injili:Sr.Kakali aleta matumaini kwa vijana nchini India

Kuhusiana na teknolojia na utandawazi wa kidijitali,wanafunzi wanapitia matatizo ya afya ya akili yanayoongezeka na kutengwa.Kwa kuchanganya usikilizaji wa kisaikolojia na uzoefu wake wa kitawa,Sr. Kakali, wa Shirika la Masista Wasaidizi wa Roho Takatifu Toharani anawasaidia vijana katika safari yao ya uponyaji.

Sr.Ilaria de Lillo,S.A na Sr. Christine Masivo,CPS

Kuwapa vijana pahali panapokuza uaminifu na kuwasikiliza na kuwaunga mkono wakati wa shida ni utume wa Sr. Kakali Majhi wa Shirika la Masista Wasaidizi wa Roho Takatifu Toharani, mwanasaikolojia katika Chuo Kikuu cha Kolkata kinachoendeshwa na Wajesuit, huko Magharibi mwa Bengal, India. "Muktadha wa kijamii wa nchi hiyo una ushawishi mkubwa kwenye mfadhaiko ambao umeenea miongoni mwa vijana. Wanahisi wamekandamizwa katika nyanja mbali mbali, kuanzia kutokuwa na uhakika wa sasa hadi matumizi yaliyoenea ya mitandao ya kijamii," Sr. Kakali alielezea. Katika hali hiyo, kazi yake kama mwanasaikolojia inamruhusu kuwasindikiza wanafunzi katika safari yao ya uponyaji, huku hekima ya Biblia ikimwongoza katika safari ya matumaini anayofanya nao, katika juhudi za kuamsha mwali uliozimika wa shauku.

Kusikiliza pamoja na kuongoza kishauri

Baada ya kupata Shahada ya Uzamili katika Masomo ya Saikolojia huko Kalkuta na Shahada ya Uzamili katika Ushauri Nasaha huko chuo Kikuu cha  Chicago, Sr. Kakali alianza kufanya kazi kama mtaalamu wa tiba mwaka 2024, akiunga mkono ustawi wa kihisia na kiakili wa wanafunzi. Polepole aligundua umuhimu wa kutumia ujuzi alioupata katika Saikolojia, na kuunganisha na ujuzi wa kibinadamu na wa kiroho wa Mtawa.

Kwa upande mmoja, sifa maalum za kitaaluma za kusikiliza kisaikolojia zinampatia fursa ya kuingilia kati katika hali zenye matibabu. Kwa upande mwingine, uzoefu wa utume wake katika Kristo unamsaidia kujikita katika matumaini, wakati migogoro ya jamii inaonekana kutokuwa na mwisho. "Kama mwanasaikolojia na mtawa, kazi yangu imeunganishwa na karama ya kuwasaidia wale waliojeruhiwa mioyoni mwao," Sr. Kakali alisema. “Katika hali za dharura au yenye uchungu, kuwa karibu na wagonjwa na kuwaelekeza maishani ni kama safari kutoka usiku wa Jumamosi Takatifu hadi kwenye mwanga wa Ufufuko,” aliongeza. Katika wakati uliosimamishwa ambapo vijana wanahisi wamepoteza maana katika maisha yao, Sr. Kakali anasimama nao.

Mahali pa ukaribisho na huruma

Katika muktadha wa kijamii ambao hauna sehemu za marejeleo, kutoa msaada wa kisaikolojia kwa vijana kunaweza kuwa kama mahali pa kujishikilia. Sr. Kakali hutoa mahali pazuri kwa vijana wanaokuja kwake. "Katika mchakato wa ushauri nasaha, mimi hujitahidi kuunda mazingira salama ambayo hayahukumu na yenye huruma, ambapo vijana wanaweza kujieleza kwa uhuru," alisema. Kuwa na nafasi ya kuzungumza kunawapa uhuru hatua kwa hatua na "huwasaidia kugundua tena nguvu zao za ndani na uwezo wao wa kukua." Safari hiyo ni ya polepole na haitabiriki na inahitaji mtazamo wa Msamaria mwenye huruma, mchakato unaohusisha jamii nzima ya walimu, utafiti unaoendelea na mazoezi ya kitaalamu yenye huruma, alielezea.

Athari za jamii na teknolojia katika mfadhaiko

Masuala ambayo Sr. Kakali aliyaona kwa vijana ni pamoja na wasiwasi kuhusu mustakabali, kuamini, kuvunjika kwa kihisia na mahusiano yasiyo imara. "Baadhi yao wana matarajio makubwa, lakini hawana ustahimilivu," alielezea, akiongeza kuwa "wanapokutana na vikwazo, mara nyingi huvitafsiri kama kushindwa binafsi badala ya changamoto za kushinda." Chanzo cha wasiwasi ni mfumo tata wa kijamii, ambao Sr. Kakali na wenzake huzingatia: kutokuwa na uhakika wa kisiasa, shinikizo la kijamii na jukumu kubwa la mitandao ya kijamii vimebadilisha uhusiano wa kibinadamu.

Kulingana na Sr. Kakali, mgawanyiko wa kisiasa husababisha mgawanyiko wa kijamii, ambao husababisha vurugu na umaskini; muunganisho mkubwa na mwingiliano wa kidijitali hupunguza kujithamini kwa vijana na kuongeza mapambano na ushindani. Utambulisho wa kibinafsi huchukua thamani na huundwa na kiasi cha "vipendwa" vinavyopokelewa. "Wengi wao," Sr. Kakali anasema, "wana matarajio yasiyo ya kweli, uwezo mdogo sana wa kuwasiliana na huwa na mwelekeo wa kutengwa."

Kusafiri pamoja nao kuelekea mabadiliko ya pamoja

Sr. Kakali anakubali changamoto, ambayo anaona kama utume wa dharura, kuwa sauti kwa wasiwasi unaohisiwa na vijana na kuandamana nao katika kujenga utambulisho wao. Alihisi kwamba, kupitia huduma hii, yeye pia anajifunza kutumaini.

"Nina fursa ya kusafiri  karibu na vijana, wanapokuwa katika hatari kubwa zaidi. Kwa kufanya hivyo, ninapitia mabadiliko ya kibinafsi," alielezea. Akipitia hayo kila siku ni somo la kusikiliza, udhaifu na ustahimilivu, Sr. Kakali anajifunza kujiunganisha na maisha ya vijana na kuwa mwenza wao wa kusafiri. Ili kusaidia katika njia za uponyaji, Kuona dalili ndogo lakini za sasa za mabadiliko kwa vijana, huimarisha hamu yake ya kuwa kando yao. Inaweza kuonekana kama tone baharini lakini, "tumaini ni daraja kati ya kukata tamaa na uwezekano," anahitimisha.

USHUHUDA WA SR KAKALI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 11:13