Tarehe 20 Aprili Papa alikuta na Maaskofu,Mapadre,watawa kike na kiume na wahhudumu wa kichungaji. Tarehe 20 Aprili Papa alikuta na Maaskofu,Mapadre,watawa kike na kiume na wahhudumu wa kichungaji.  (@Vatican Media)

Padre Msudan huko Angola:Sudani Inahitaji ujumbe wa Papa wa amani

Kutokana na wito wa mara kwa mara wa Papa Leo XIV kwa ajili ya amani wakati wa Ziara yake ya Kitume,Padre Samir Alrafayne,wa Sudan ambaye amekuwa Angola kwa miaka 13,alitoa wito wa kuzingatia upya hali mbaya nchini Sudani,ambapo mzozo mkali umeendelea kwa miaka mingi na kuua makumi ya maelfu na kuwafukuza mamilioni ya watu.

Na Claudia Torres-Luanda,Angola na Sr.Christine Masivo,Cps–Vatican.

"Inawezekana kujenga pamoja nchi ambapo mgawanyiko wa zamani unashindwa mara moja na kwa wote, ambapo chuki na vurugu hutoweka, na ambapo janga la ufisadi huponywa na utamaduni mpya wa haki na ushiriki." Maneno ya Papa Leo XIV wakati wa Misa Takatifu huko Kilamba, tarehe 19 Aprili 2026, yalimgusa sana Padre Samir Alrafayne Padre wa Sudan ambaye amekuwa nchini Angola kwa miaka 13. Alipewa daraja la Upadre miaka minne iliyopita baada ya kupokea malezi ya kipadre katika Seminari ya Mater ya Redemptoris huko Luanda, seminari ya kimisionari na Jimbo kuu  na pia uzoefu wa Njia ya Neokatekumenali. Leo yeye ni padre katika Jimbo Kuu la Luanda.

Makaribisho ya Papa  huko Angola kabla ya Misa
Makaribisho ya Papa huko Angola kabla ya Misa   (@Vatican Media)
Wakati wa Misa huko Angola
Wakati wa Misa huko Angola   (@Vatican Media)

Vikwazo vya uinjilishaji

Akizungumza na Vatican News pembeni mwa mkutano wa Baba Mtakatifu na Maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume na wahudumu wa kichungaji katika Parokia ya Mama yetu wa Fatima huko Luanda, mnamo tarehe 20 Aprili 2026 Padre Alrafayne alisema ziara ya Papa inaweza kusaidia kuimarisha jamii ya Angola. Alielezea mapambano ya nchi dhidi ya dhuluma za kijamii na umaskini, na akataja madhehebu mapya kama yanahusu hasa uinjilishaji katika nchi ya Afrika, kwani yanaunda “mipasuko au migawanyiko katika familia."

"Tunahitaji Baba Mtakatifu kama Petro kutuimarisha katika imani," alisema, akiongeza kwamba uwepo wa Papa "pia huleta furaha nyingi" na "neema nyingi kwa watu." Padre Alrafayne kisha alitafakari ujumbe wa Papa Leo XIV kwa ajili ya amani. "Kama unavyojua, Angola inatoka katika historia ya vita," alisema, akikumbuka mahubiri ya Baba Mtakatifu huko Kilamba. Sasa Angola inahitaji zaidi roho ya "undugu," ya "roho ya Kikristo," alisisitiza.

Umati katika kumpokea Papa na misa
Umati katika kumpokea Papa na misa   (@Vatican Media)

Ombi la amani nchini Sudan

Padri Alrafayne alisema ombi la Baba Mtakatifu la amani nchini Angola pia linaenea hadi nchi zingine za Afrika, ikiwa ni pamoja na Sudani nchi yake ya asili, ambapo migogoro inayoendelea imewafukuza mamilioni ya watu, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu ambao bado haujaangaziwa kimataifa. "Watu wachache huzungumza kuhusu Sudan," alisema. "Tunajua kwamba katika wakati huu kuna mvutano mwingi duniani, maeneo mengi ya vita, lakini nchini Sudan tunahitaji umakini zaidi."

Wakati wa Mkutano
Wakati wa Mkutano   (@Vatican Media)

Kwa hivyo alithamini ombi la mara kwa mara la Papa la amani. “Papa Leo XIV kwa njia hiyo alitaja kifungu hiki: 'Hakuna vita, hakuna vita tena.' Hiki ndicho tunachohitaji Sudan," alisisitiza Padre. "Sudan imeteseka na vita kwa muda mrefu," alisema, akibainisha kuwa miaka mitatu iliyopita ya migogoro imesababisha "zaidi ya watu milioni 15" kuwa wakimbizi. "Wanateseka, wanakufa," na wengine wanaishi katika "hali ngumu sana," alisema Padri Alrafayne. "Sudan inahitaji umakini wako, inahitaji msaada wako, inahitaji maombi yako kweli."

USHUHUDA WA PADRE WA SUDAN KUSINI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

23 Aprili 2026, 11:58