Siku uya Vijana huko  Seoul 2027 Siku uya Vijana huko Seoul 2027 

Msalaba wa amani wa Siku ya Vijana Duniani 2027 huko Seoul

Jimbo Kuu la Seoul lilizindua mpango wenye nguvu kwa Siku ya Vijana Duniani 2027:"Msalaba wa Amani"uliotengenezwa kwa waya wenye miiba uliochukuliwa kutoka Eneo Lisilo na Jeshi.Mpango huu wa mfano unatafuta kubadilisha nyenzo za mgawanyiko kuwa ishara ya upatanisho,matumaini,na upyaisho wa kiroho.Kupitia ufundi wa jumuiya na sala,Msalaba utajumuisha hamu ya amani kati ya Korea Kaskazini na Kusini.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Katika maandalizi ya Siku ya Vijana Duniani 2027, Jimbo Kuu la Seoul lilianzisha nembo ya kuvutia wa Msalaba wenye urefu wa mita tano uliotengenezwa kwa waya wenye miiba uliokuwa umetupwa ambao hapo awali ulikuwa umefunika ‘Eneo Lisilo na Jeshi’ lenye ngome nyingi. Kwa muda mrefu ikizingatiwa kama ukumbusho mkali wa mgogoro ambao haujatatuliwa kati ya Korea Kaskazini na Kusini, waya wenye miiba sasa unabadilishwa kuwa ishara kubwa ya umoja. "Msalaba huu wa Amani" utasimama kama ishara kuu ya kiroho wakati wa mkutano wa kimataifa wa vijana na utabarikiwa na Papa, akisisitiza ujumbe wake wa upatanisho wa ulimwengu wote.

Kubadilisha maumivu kuwa maombi

Mpango huu, unaoongozwa na " Mfuko wa kutembea pamoja," si wa kisanii tu bali wa kiroho kwa  dhati. Kila kipande cha waya wenye miiba kimewekwa pamoja kwa kutumia nyundo na kusokotwa ndani ya muundo, na kugeuza vipande vya utengano kuwa kitu kimoja. Washiriki kuanzia vijana na wanaparokia hadi watu binafsi kutoka sekta za kiutamaduni na kijamii walishiriki katika tafakari na maombi wakati wakifanya kazi. Mchakato huo unawaalika wote kukabiliana na majeraha ya kibinafsi na ya pamoja, na kuyabadilisha kuwa nia za amani na uponyaji.

Warsha hai ya imani

Msalaba uliwekwa katika uwanja wa  Kanisa Kuu la Myeongdong, ambapo ni msingi wa maisha ya Kikatoliki jijini. Kila Dominika, watu wa kujitolea hukusanyika kwa saa nyingi za kazi wakiambatana na kutafakari na uzoefu wa pamoja wa kiroho. Jitihada hizi zinazoendelea zimepangwa kuendelea hadi mwezi Aprili 2027, ilibadilika kuwa warsha hai ambapo ufundi hukutana na tafakari. Inawakilisha safari ya kijamii kuelekea upatanisho, ikienea zaidi ya mipaka ya kidini hadi kwa jamii yote.

Ujumbe kwa Korea na ulimwenguni

Askofu Mkuu Peter Soon-taick Chung, ambaye aliongoza kamati ya maandalizi, alisisitiza maana ya kina ya mpango huo. Akilinganisha na uelewa wa Kikristo kuhusu msalaba, alibainisha kwamba kile ambacho hapo awali kilikuwa chombo cha mateso kinaweza kuwa ishara ya upendo, sadaka, na amani. “Msalaba wa Amani” hatimaye unatafuta kuhamasisha si tu Ghuba ya Korea bali pia jamii ya kimataifa. Ujumbe wake uko wazi: hata alama zenye uchungu zaidi za mgawanyiko zinaweza kubadilishwa kuwa ishara za kudumu za matumaini, umoja, na upyaisho.

MSALABA 2027 SEOUL

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

21 Aprili 2026, 10:52