Gionea ya Ikweta yamkaribisha Baba Mtakatifu kwa shangwe kuu Gionea ya Ikweta yamkaribisha Baba Mtakatifu kwa shangwe kuu  (@Vatican Media)

Padre Mklareti atafakari mabadiliko ya Kanisa nchini Guinea ya Ikweta

Padre Inocencio Moisés,Mclaretian huko Malabo alitafakari umuhimu wa uwepo wa Papa Leo XIV katika nchi yenye Wakatoliki wengi,na aliakis njia muhimu ambazo Kanisa nchini Guinea ya Ikweta limebadilika tangu ziara ya mwisho ya Papa ya mwaka 1982.

Claudia Torres–Malabo,Guinea ya Ikweta na Sr.Christine Masivo,CPS.

Padre Inocencio Moisés, Claretian huko Malabo, alikuwa anagli mtoto wakati Mtakatifu Papa Yohane Paulo II alipotembelea Guinea ya Ikweta miaka 44 iliyopita. Sasa yeye ni mratibu wa Jimbo kuu ya ziara ya Papa Leo XIV nchini mwake, kazi ambayo ameikumbatia kwa shukrani. Akizungumza na Vatican News pembeni mwa uzinduzi wa ‘Kampasi ya Papa Leo XIV’ ya Chuo Kikuu cha Kitaifa huko Malabo, alitafakari umuhimu wa uwepo wa Baba Mtakatifu katika nchi yenye Wakatoliki wengi. Pia alitoa muhtasari wa njia muhimu ambazo Kanisa limebadilika tangu ziara hiyo ya mwisho ya Papa mwaka wa 1982, akiangazia ongezeko la miito ya ukuhani na Kanisa la mahali hapo zaidi.

Watoto wakicheza mbele ya Papa katika Chuo Kikuu cha Kitaifa
Watoto wakicheza mbele ya Papa katika Chuo Kikuu cha Kitaifa   (@Vatican Media)

Je, umuhimu wa ziara ya Papa Leo XIV nchini Guinea ya Ikweta ni upi?

Kweli, kwetu sisi huu ni wakati maalum. Papa alifika Guinea ya Ikweta kwa mara ya kwanza, lakini tunaweza kusema ilikuwa  safari ambayo sisi kwa walio wengi wetu tulikuwa watoto tu. Pia ilikuwa wakati mfupi mno; Papa Mtakatifu Yohane Paulo II, mwenye kumbukumbu nzuri, hakukaa hata usiku kucha. Miaka mingi baadaye, karibu miaka 44, tuna fursa kwa Papa kututembelea tena katika nchi yenye Wakatoliki wengi, na tunaweza kumuona Mtakatifu Papa Leo XIV. Kwetu sisi, kama wimbo tuliotunga unavyosema, ni sababu ya matumaini na furaha.

Wanachuo kwa furaha ya kumuona Papa Leo XIV
Wanachuo kwa furaha ya kumuona Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Tunaishi katika muktadha wa matatizo mengi ya kifamilia, katika muktadha wa Kiafrika pia ulio na migogoro ya silaha, chuki nyingi, lakini pia matumaini. Kwa hivyo, tunaamini huu pia ni wakati wa matumaini, umoja, na uimarishaji wa imani yetu. Tumetumia muda mrefu tukiinjilisha. Tayari kuna makanisa mengi hapa, madhehebu mengine pia. Lakini tunahitaji kuimarisha imani ya Wakatoliki na Wakristo ili waelewe kweli. Kwa hivyo ziara hii ya Baba Mtakatifu ni msukumo mkubwa kwetu muhimu na maalum. Ni wazi ni ziara ya kichungaji. Labda baadhi ya watu wanaweza kuiona kama wakati tu wa tamasha la kitamaduni, lakini wengi wao wamekuwa wakiisubiri kwa muda mrefu kama chanzo kingine cha upyaishaji sio tu kwa walei, bali pia kwetu sisi watawa na mapadre. Yeye ndiye mchungaji wetu.

Furaha ya kumsikiliza Papa
Furaha ya kumsikiliza Papa   (@Vatican Media)

Kanisa huko Guinea ya Ikweta limebadilikaje tangu ziara ya mwisho ya papa mwaka wa 1982?

Kanisa limebadilika sana. Sio kwa sababu mimi ni Mklareti, lakini kama Papa alivyosema wakati huo, uinjilishaji hapa ulifanywa kwa kiasi kikubwa na Waklareti, ingawa wangeweza kuwa Wajesuiti au Wadominika. Kwa hali, ilikuwa zaidi Waklareti walioinjilisha Kanisa hili. Shukrani kwa Mungu, na pia kwa msukumo wa Roho Mtakatifu, sasa kuna mashirika mengi zaidi ya kidini hapa. Wamisionari wa Moyo safi wa Maria pamoja na Maria aliyetungwa mimba pasipo na dhambi, waliofika miaka miwili baada ya wamisionari wa Waklareti kwa ombi lao. Kuna mashirika mengi ya watawa na mapadre wa Jimbo. Kwa kweli ni Kanisa mahalia. Wamisionari kutoka nchi zingine ni wachache kila siku, na ukweli kwamba majimbo yetu sasa yana maaskofu wa Equatoguinea pia ni ishara ya ukomavu wa Kanisa Katoliki huko Guinea ya Ikweta.

Baba Mtakatifu alikuwa katikati ya wanachuo
Baba Mtakatifu alikuwa katikati ya wanachuo   (@Vatican Media)

Uso wake umebadilika kuwa bora. Kuna vijana wengi amabo wangependa kujiunga na maisha ya kitawa na upadre hata maeneo ya mbali zaidi ambayo wamisionari hawakuweza kufikia hapo awali. Sote tuko huko. Leo, hata katika mashirika ya watawa wa kike na wakiume, kwa kiasi kikubwa ni wazaliwa wa hapa nchini. Kwa mfano, katika shirika langu mwenyewe hapa Equatorial Guinea, tuko takriban Waklareti 50, na wawili tu ni wageni, mmoja Mmarekani na mmoja Mhispania. Wengine ni Waguinea. Hii pia ni shukrani kwa wale ambao, kupitia roho yao ya umisionari, walitutia moyo kukumbatia njia hii ya maisha katika Kristo, mapadre wote wa kimisionari na wajimbo.

Papa akisalimia wanachuo wa Guinea ya Ikweta
Papa akisalimia wanachuo wa Guinea ya Ikweta   (@Vatican Media)

Kwa hivyo kuna vijana wengi wenye miito ya maisha ya kitawa?

Kuna vijana wengi. Seminari ya kati ya majimbo huko Bata imejaa na imelazimika kupanuliwa kutokana na ukosefu wa nafasi. Kuna uimarishaji wa imani. Hata hivyo, hili halifanyiki katika mashirika ya wanawake. Hatujui ni kwa nini, na jambo  hili linahitaji uchunguzi wa kina. Katika mashirika ya wanaume, ya kijimbo na ya kimisionari, kuna miito. Kuna ugumu na miito ya wanawake, na tunahitaji kudadisi na kujua ni kwanini na ni sababu gani ikawa hivyo. Tuko katika nchi moja, kwa hivyo si rahisi kuelewa ni kwa nini sasa ni vigumu zaidi kwa wanawake vijana kujiunga na maisha ya utawa.

Chuo Kikuu cha Guinea ya Ikweta
Chuo Kikuu cha Guinea ya Ikweta   (@Vatican Media)

Unafikiri ni kwa nini hivyo?

Nina maoni yangu binafsi: labda mashirika ya wanawake yanapaswa pia kufikiria upya mbinu yao ya malezi. Nilisema katika mkutano, kwamba kwa sababu mbalimbali, elimu ilikuwa na kikomo zaidi. Lakini leo, ikiwa msichana wa miaka 17 au 18 ambaye amemaliza shule ya upili hataki elimu ya juu, hilo linakuwa jambo gumu. Inapaswa na ni muhimu kuhimiza malezi bora ya kwa wanawake wanaojiunga na mashirika ya utawa. Wengi wana matarajio ya kusoma, lakini katika baadhi ya Mashirika, wanatulia: wanaingia katika unovisi, wanakuwa watawa, na huo unakuwa ndio mwisho wa masomo yao. Ninaamini huu ni ugumu. Hili halitokei kwa Mashirika ya kiume au mapadre, kwa sababu hatimaye huendelea na masomo ya chuo kikuu. Ikiwa Mwaamke  kijana hawezi kufanya hivyo, hilo linakuwa kikwazo.

Papa akibariki  Chuo Kikuu kilichopewa jina la Papa leo XIV
Papa akibariki Chuo Kikuu kilichopewa jina la Papa leo XIV   (@Vatican Media)

Zaidi ya hayo, ni lazima tuimarishe utume wa kutafuta miito. Labda tumekuwa watulivu kiasi. Tunahitaji kuwasilisha ujumbe uleule kwa njia mpya, kurekebisha lugha, kuelewa wakati uliopo, na kutobaki tumekwama katika wakati uliopita. Hatuwezi kuliweka Injili kando na mahitaji yake, lakini ni lazima tuirekebishe kulingana na muktadha. Ndiyo maana tunazungumzia  utamadunisho Afrika, wa ujumbe usio na utamaduni. Hiyo ndiyo maoni yangu.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

22 Aprili 2026, 17:20