Angola,POSI:Kazi na mipango ya Utoto Mtakatifu kwa Kanisa la Angola na kimisionari
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Huko Benguela na Ndalatando kuna mipango miwili ya watoto iliyofadhiliwa hivi karibuni na Shirika la Kipapa ya Utoto Mtakatifu(POSI) ambayo iko katika majimbo haya. Padre José Diego Jerónimo Zola, Katibu wa POSI ya Angola, ambaye uhusiano wake na Shirika la Kipapa la Kimisionari(PMS) ulianza tangu enzi zake za seminari, akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides alielezea ukweli na matamanio yanayochochea uwepo mkubwa wa Utoto Mtakatifu nchini kote katika miji mikubwa na midogo. Kinachojitokeza ni sura ya Kanisa, jumuiya ya kikanisa inayopata faraja na utulivu katika kuwasaidia na kuwasindikiza watoto na vijana katika hali ambazo mara nyingi huakisiwa na umaskini kuacha shule, na unyanyasaji.
Shirika la Utoto Utoto Mtakatifu wa Kimisionari linalinga kuwasindikiza watoto, vijana, na waelimishaji wao katika safari yao ya imani, kukuza hata wasiwasi wa kimisionari ndani yao, kuwaunga mkono kwa roho ya mshikamano na wenzao, na kuhamasisha mikutano ya kitaifa ili kuongeza uelewa wa hali halisi mbalimbali zinazopatikana katika nchi kubwa: haya ni miongoni mwa malengo ya POSI. Malengo haya pia yanatekelezwa kupitia mipango inayolenga kuwalinda watoto kwa ushirikiano na serikali na taasisi zingine, au kupitia ujenzi wa shule.
Shule mpya ya La Salette kwa ajili ya watoto
"Papa Leo XIV ambaye anatembelea nchi yetu siku hizi, pia anawakumbatia na kuwabariki watoto na vijana wetu kwa safari yake ya kitume. Tunataka kusikia maneno yake ya amani, upatanisho, na haki ya kijamii; tunataka 'kuinuliwa' na maneno yake ya matumaini. Ni maneno ya Mkurugenzi wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu nchini Angola. Huko Benguela, mnamo Machi iliyopita, jiwe la msingi liliwekwa kwa ajili ya shule iliyokabidhiwa kwa Masista wa Mama Yetu wa ‘La Salette.’ Shule hiyo inalenga kuwaokoa watoto na vijana kutokana na kuacha shule, ambao vinginevyo hawangepata fursa ya kupata elimu na hivyo kujenga mustakabali wao. Padre Zola alishirikisha furaha na shukrani zake kwa watoto wengi aliowaona wakikua katika shule zinazoungwa mkono na POSI, ambao sasa ni madaktari, walimu, na wahandisi, na ambao hawasahau kamwe uzoefu wao katika Utoto Mtakatifu wa Kimisionari. "Ninachopenda zaidi, ni kuwa na watoto, miongoni mwa watoto, kwa ajili ya watoto, na hata kama watoto, kwa matumaini kwamba idadi inayoongezeka ya watoto na vijana inaweza kukuza ustawi wa Kanisa la Angola na la kimisionari,” alibainisha.
Papa anayetembelea nchi yetu anakumbatia safari ya kitume ya watoto
Padre José Diego Jerónimo aliendelea kusema kuwa “Mpango wmingine ninaotaka kuutaja ni ule unaojengwa katika Parokia ya Mtakatifu Teresa wa Avila iliyojengwa hivi karibuni huko Ndalatando. Lengo lake ni kujenga madarasa ya katekisimu, hivyo kuunda mahali pa heshima na penye kukaribisha pa kutoa elimu ya Kikristo kwa watoto na vijana." Padre Zola pia alisimulia jinsi watoto na vijana wengi wanavyoanza kushiriki katika mipango na Katekisimu za POSI bila kubatizwa, hivyo kuanza safari yao katika imani ya Mitume. Kwa mpango wa Katekisimu unaowaongoza kupokea sakramenti za Ubatizo, Ekaristi, na Kipaimara. "Papa Leo XIV ambaye anatembelea nchi yetu siku hizi, pia anawakumbatia na kuwabariki watoto na vijana wetu kwa safari yake ya kitume. Tunataka kusikia maneno yake ya amani, upatanisho, na haki ya kijamii; tunataka 'kuinuliwa' na maneno yake ya matumaini," alihitimisha katibu wa POSI ya Angola.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.