Ziara ya Kitume ya Papa Angola 18 -21 Aprili 2026. Ziara ya Kitume ya Papa Angola 18 -21 Aprili 2026. 

Angola:Papa Leo XIV anasubiriwa kwa shauku kubwa huko Angola

Hatimaye ziara ya Papa Leo XIV nchini Angola imewadia.Papa Leo XIV anakuwa Angola kuanzia Aprili 18 hadi 21.Ni tukio ambalo limeifanya nchi nzima kuchukua hatua kuanzia maafisa wa serikali,uongozi wa Kikatoliki,waamini na taasisi za kidini nchini kote.

Anastácio Sasembele – Luanda na Sr. Christine Masivo, CPS - Vatican.

Askofu Vicente Sanombo wa Jimbo la Kuito-Bié akizungumza Vatican News kwamba anaamini uwepo wa Baba Mtakatifu nchini Angola utakuwa hatua muhimu katika kuimarisha umoja na maridhiano ya kitaifa miongoni mwa Waangola. Kulingana na Askofu, ziara hiyo inatoa fursa ya kipekee ya kukuza maadili ya amani, mshikamano, na mshikamano wa kijamii.

Papa Leo XIV ni mmisionari

Wakati huo huo, Jimbo Kuu la Lubango tayari liliwaandaa waamini Wakatoliki wa kufika  kukutana na Baba Mtakatifu. Lubango iko kusini-magharibi mwa Angola, karibu kilomita 1,000 kutoka mji mkuu, Luanda. Kwa kawaida ni safari ya zaidi ya saa 12 kwa barabara.

Waamini wapatao 500 watashiriki katika sherehe hizo zitakazoongozwa na Papa Leo XIV. Msaidizi wa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Lubango, Padre Maurício Capembe, alisema kwamba mipango ya kichungaji inayohusiana na ziara ya Papa, inaonesha ushiriki mkubwa wa Jumuiya ya Wakatoliki wa eneo hilo wakati huu wenye umuhimu mkubwa wa kiroho na kijamii kwa nchi. Kwa upande wake, mwandishi wa habari mkongwe wa Angola Bwana Moisés Malumbu, mwandishi wa  zamani wa Vatican News - Vatican Radio, aliakisi baadhi ya vipengele muhimu vya wasifu wa Papa Leo XIV. Miongoni mwake, alisisitiza historia ya Baba Mtakatifu kama mmisionari. Ziara ya Papa Leo XIV inasubiriwa kwa hamu si tu na Waangola bali pia na Wakatoliki wote Kusini mwa Afrika.

Ziara ya Papa Angola

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

18 Aprili 2026, 11:29