Talitha Kum Kenya Talitha Kum Kenya  #SistersProject

KENYA:Watawa wakabiliana na biashara haramu ya binadamu katika enzi ya kidijitali

Ingawa wahalifu wanajaribu kuficha,biashara haramu ya binadamu inakiuka utu wa binadamu na kuvuka mipaka,tamaduni,jamii zilizo hatarini,zilizokumbwa na umaskini na waliokata tamaa.Hata hivyo,iko karibu zaidi kuliko tunavyofikiria,ikizingatia simu zetu na mitandao ya kijamii kama meseji zinayojitokeza kwenye skrini.Watawa pamoja na Mtandao wa Talitha Kum,Kenya wanajenga mtandao wenye uwepo wa ndani na athari za Kimataifa.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Wafanyabiashara haramu ya binadamu wamekumbatia enzi ya kidijitali duniani kote. Watawa wako mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya binadamu, biashara yenye faida na teknolojia ya kisasa, kupitiaTalitha Kum Kenya, kitengo cha Mtandao wa kimataifa unaoongozwa na  Umoja wa Kimataifa wa Mama Wakuu wa Mashrika (UISG), wenye makao yake makuu Roma. Sr. Mercy Mwai (FSJ), wa Shirika la Wafransiskani  wa Mtakatifu Yosefu na Mkurugenzi wa Talitha Kum, Kenya, alisimulia jinsi imani, ushirikiano, na vitendo vya ndani vinavyobadilisha mapambano dhidi ya biashara hii haramu ya binadamu.

Vita dhidi ya biashara haramu

Kufuatia na wito wa Papa Francisko wakati wa Mwaka wa Jubilei ya Huruma, Talitha Kum, Kenya ilianzishwa mnamo Februari 2016 ili kuwafikia wale wanaoishi na walioathiriwa na biashara haramu ya binadamu. Mpango huo ulianza mwaka 2022, ukifadhiliwa na Mfuko wa  Conrad Hilton, unaosaidia Watawa wa Mashirika. Talitha Kum Kenya inafanya kazi kama Shirika la upendo lililounganishwa na Mtandao wa Kimataifa wa Talitha Kum, ikiratibu uanachama mpana zaidi ikiwa ni pamoja na watawa wa kike na kiume, vijana, na washirika wa kawaida  Kenya yote, wakisaidia kukabiliana na biashara haramu katika vijiji, maeneo ya mpakani, makazi ya mijini, na uwepo mtandaoni.

Kinga katika ngazi za chini na mtandaoni

"Biashara haramu ya binadamu si tatizo la Kiafrika tu," Sr. Mercy alielezea, huku akisisitiza kwamba ni tatizo la kimataifa linaloathiri watu wa rika zote wanaotafuta fursa bora. Huku biashara haramu ikiingiliana na uhalifu wa mtandaoni, wahalifu hawa hutumia nafasi za kidijitali kuwanasa waathiriwa. Mtandao wa Talitha Kum, unajibu hitaji hili kupitia kuzuia, ulinzi, na ushirikiano, ukitambua kwamba mchakato lazima uunganishwe kama uhalifu wenyewe. "Waathiriwa wengi wanatambua kwamba wanasafirishwa nje ya nchi wakiwa wamechelewa sana," Sr. Mercy alisema. Ahadi za matangazo mtandaoni za kazi za uongo, ahadi za Visa za uongo, na mahojiano ya siri ni mtandaoni kama mitego ya kawaida. Ili kuzuia hili, masista  na wenzi wao hufanya warsha, mabaraza ya jamii na uhamasishaji wa Parokia ili kuelimisha jamii na kuwahamasisha kuhusu biashara haramu ya binadamu na jinsi inavyofanya kazi, na ishara zake za maonyo.

Ushirikiano

Maafisa wa polisi na wafanyakazi wa usalama wa mpakani wamefunzwa kutambua viashiria vya biashara haramu ya binadamu na kujibu ipasavyo, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai (DCI), Sekretarieti ya Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu ya Wizara ya Jinsia, na Idara ya Mambo ya Nje ya Diaspora na Tanzania. Umakini maalum  wa maeneo ya mpaka wa Kenya na Somalia, Ethiopia, Sudan Kusini, Uganda, na Tanzania.

Matrafiki wakishiriki kozi

Uokoaji hadi ujumuishaji

Waathiriwa hutambuliwa kupitia miito ya serikali, mashirika washirika, wajumbe wa mashirika  na simu ya dharura isiyolipishwa. Uokoaji wa kimataifa hufanywa na vyombo vya kutekeleza sheria, na wanaporudi nyumbani, hupokelewa na masista na kusindikizwa hadi kwenye makazi salama. Wanusurika hufanyiwa uchunguzi ili kutathmini mahitaji yao, wengi huihitaji msaada wa kisaikolojia ili kushughulikia kiwewe. Wanapokea huduma za kimatibabu, uwezeshaji wa kiuchumi kupitia biashara ndogo ndogo, na mafunzo ya ufundi ili kusaidia kupona kwao. "Lengo ni kuunganishwa tena kwa ujumla," Sr. Mercy alisisitiza, akielezea kwamba uhuru si tu kuhusu kuokolewa bali pia kuhusu kujenga upya maisha kwa uadilifu.

Watawa katika mstari wa mbele

Watawa ni uti wa mgongo wa utume huu, wakiandaa mafunzo ya jamii, kutambua kesi zinazoambatana na manusura, kutoa ushauri, na kufungua taasisi zao kwa ajili ya mafunzo ya ujuzi. Katika maeneo ya pwani kama Malindi na Mombasa, wanahusika moja kwa moja katika kuwaokoa waathiriwa wa biashara haramu ya binadamu na ukatili wa kijinsia. Sr. Mercy alishirikisha kesi ya kusisimua ya mwanamke wa Burundi aliyesafirishwa kwenda Kenya na baadaye kufungwa na watoto wake, hadi juhudi zilizoratibiwa na Talitha Kum, DCI, wanasheria, ubalozi, na Masista Wamisionari wa Mama Yetu wa Afrika, zilipowahakikishia uhuru wao na kurudi nyumbani salama. Mafanikio yao yanathibitisha kwamba mshikamano na manusura unaenea zaidi ya mipaka ya kitaifa.


Talitha Kum Kenya:Wajumbe wa Mtandao  AGM

Changamoto za kidijitali

Wahusika wa usafirishaji haramu wa binadamu kila kuchao wanaibuka na mitindo mipya ya ulaghai wa mtandaoni, na hata kuwanyanyasa vijana waliosoma sana, wakiwemo wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mwasiliano(TEHAMA), kwa ulaghai wa kidijitali na ahadi za kwenda kufanya kazi nje ya nchi. Talitha Kum Kenya inakabiliwa na vitisho vya moja kwa moja kutoka katika mitandao ya usafirishaji haramu na mahitaji makubwa miongoni mwa waathirika, mara nyingi zaidi ya rasilimali zilizopo. Ufadhili mdogo, hatari za usalama, na waathiriwa wa kiwewe cha kina hubeba kila wakati na  bado wasiwasi unaendelea. Lakini bado masisista hawajakata tamaa ya kuwasaidia watu hawa.

Wajibu wa kimataifa

Usafirishaji haramu wa binadamu unastawi katika ukimya, mgawanyiko, na ujinga. Talitha Kum Kenya inatoa njia tofauti ya ushirikiano, ufahamu, imani, na ujasiri. Kama Sr. Mercy alivyodhibitisha, kuwa hakuna shirika moja linaloweza kukomesha usafirishaji haramu peke yake. "Huu ni uhalifu wa kimataifa, na unahitaji nguvu ya kimataifa," alisema. "Serikali, Makanisa, shule, mashirika yasiyo ya kiserikali, jamii kila mtu ana jukumu. Kwa pamoja tunaweza kupambana na wahalifu na kurejesha uhuru." Kwa kuhitimisha anabainisha kuwa  ushuhuda wa masista katika utume huo unaionesha dunia kwamba hitaji la uangalifu, huruma, na uwajibikaji wa pamoja lazima liende haraka kuliko unyonyaji unaosafiri kwa kasi ya mbofyo mmoja.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

09 Machi 2026, 10:30