Watawa Wafransiskani wa Maria (FSM). Watawa Wafransiskani wa Maria (FSM).  #SistersProject

Papua New Guinea:Masista Wafranskani wa Maria wanashiriki moyo wa kichungaji na waamini

Katika eneo lenye miamba na jumuiya za mbali za Papua New Guinea,mandhari ya kijiografia mara nyingi huwa vigumu sana kutoa huduma za kichungaji na kijamii.Masista Wafransiskani wa Maria wa (FSM) hutoa uwepo tulivu na thabiti na kufanya tofauti kubwa katika maisha ya kichungaji ya Kanisa mahalia.

Na Sr. Christine Masivo, CPS

Masista Wafransiskani wa Maria walianzishwa mwaka 1976 katika Jimbo la Mendi, na Askofu Mkapuchini Firmin Schmidt akisaidiwa na watawa wakapuchini kutoka Marekani, masista Wafransiskani kutoka India, na Masista Wamisionari wa Uswiss. Dhamira yao ilikuwa kuanzisha Shirika Mahalia ambalo lingeweza kujibu kwa ufanisi mahitaji ya kichungaji ya Kanisa changa na linalobadilika katika Jimbo ya Mendi.

Shirika lililozaliwa kutokana na mahitaji ya kichungaji

Akizungumza kwa shauku na Vatican News, Sr. Grace Nakan, FSM, alisimulia historia yenye uzito ya utume wao, huduma na kujitolea kwa watu wa Papua New Guinea kutoka Shirika lililozaliwa kutokana na mahitaji ya kichungaji, hasa katika maeneo ambayo mapadre  hawangeweza kwenda kwa urahisi. "Wakati huo," Sr. Grace alielezea, "kulikuwa na wamisionari wachache sana na hawakuweza kufika maeneo yote hasa vituo vya mbali vilivyo mbali msituni." Huku shirika likisherehekea jubilei yake ya dhahabu mwaka wa 2026, masista wanakumbuka kwa shukrani na wakiwa na nia njema na matumaini ya kuendelea mbele kwa kujitolea upya katika utume waliyokabidhiwa siku zijazo.

A visit in the village during pastoral work of the sisters

Kutembelea wenyeji wakati wa uchungaji wa masista hawa 

Kutoa huduma hata mahali ambapo hakuna barabara

Kuwepo katika huduma ya kichungaji ndiyo suala kuu ya Masista, kwani wanafanya kazi kwa karibu na mapadre kwa kusaidia katika katekesi, maandalizi ya sakramenti, na malezi ya imani. Utume wao mara nyingi huwapeleka kwenye vituo vya mbali vya msituni, ambapo kufika huko ni kwa miguu tu, hivyo basi jamii hizo zinaweza kubaki kwa muda mrefu bila kumuona Padre. "Tunaenda kukaa na watu ndani ya kijiji usiku kucha, tukiwaandaa kwa ajili ya sakramenti, kuendesha maombi, na kuwasaidia kuhisi kwamba Kanisa liko pamoja nao," anasema Sr. Grace. Katika maeneo mengi kati ya haya, masista wanaonekana si tu kama mawakala wa kichungaji bali pia kama walezi. Ingawa si wote ni wauguzi kama wataalamu, lakini masista wanasaidiana wanapojibu kwa shauku mateso ya wanadamu. Wao hutoa huduma ya kwanza, hubeba dawa za msingi, na kuhakikisha kwamba wale wanaoishi na virusi vya ukimwi, wanapata dawa hata katika maeneo yaliyotengwa zaidi.

Elimu afya na usimamizi wa utume

"Zaidi ya Katekesi, karama ya Shirika inahusisha ufundishaji, uuguzi na huduma za utawala," alisisitiza Sr. Grace. "Masista hutoa huduma  katika shule za Kikatoliki, ofisi za jimbo, na kliniki za afya zinazoendeshwa na mashirika ya Kikatoliki, hasa katika maeneo ambayo hayahudumiwi kikamilifu na huduma ya serikali." "Katika huduma ya afya, wataalamu wetu wa afya hufanya kazi katika kliniki za Kikatoliki mjini na maeneo ya mbali," Sr. Grace alielezea. "Hii pia ni kazi ya kichungaji, kufanya kazi na watu walio katika magonjwa na udhaifu wao."

Sr. Grace guiding the Catholic students at the University

Sr. Grace anawaongoza wanafunzi wakatoliki katika Chuo Kikuu.

Mshauri na mjenzi wa daraja

Kwa sasa Sr. Grace anasomea shahada yake katika chuo kikuu na anaendelea na utume wake chuoni kama mshauri na mkurugenzi wa kiroho wa Chama cha Wanafunzi Wakatoliki. Zaidi ya uwepo wake kitaaluma, anawatia moyo wanafunzi akiunga mkono ukuaji wao wa kiroho, na husaidia kuratibu sherehe za kiliturujia na mipango ya kichungaji kwa kushirikiana na padre anayewahudumia katika chuo. Uongozi wake pia unahamasisha matendo ya hisani. Akishirikiana pamoja na wanafunzi wengine na wahadhiri wanaounga mkono, yeye husaidia kupanga uhamasishaji katika kambi za magereza na hospitali, kukusanya nguo za mitumba, chakula, na fedha. Mipango hiyo ni kwa kujitolea kwa wanafunzi ikiwa imejikita kwenye sala za pamoja. Kabla ya kutoa chochote kwa wahitaji,” anasema, “tunasali pamoja nao, tunawatia moyo na kuwakumbusha kwamba hawajasahaulika.”

A Franciscan sister serving patients in the clinic

Mtawa akitoja huduma kwa mgonjwa katika Kliniki 

Sauti nje ya Mipaka

Sr. Grace alialikwa kuwawakilisha wanafunzi Wakatoliki wa Papua New Guinea katika mkutano wa Wanafunzi wa Asia-Pasifiki nchini Thailand ambao ulilenga kukuza umoja miongoni mwa vijana na kushughulikia changamoto zinazoshirikiwa kama vile umaskini, ukosefu wa ajira, ugumu wa kiuchumi, ufisadi, amani, na haki. "Fursa hii ilinifungua macho kuona ukweli kwamba mapambano mengi yanayowakabili vijana huko PNG yanasikika katika eneo lote la Asia-Pasifiki," anabainisha. Aliporudi, Sr. Grace alishiriki matokeo hayo na wanafunzi nyumbani, akisaidia kujenga mitandao imara kupitia WhatsApp na vikundi vya barua pepe ambavyo sasa vinawaunganisha viongozi wa wanafunzi Wakatoliki kuvuka mipaka. "Tunasaidiana kwa kushiriki uzoefu na kusaidiana kama wanafunzi Wakatoliki," alikumbuka.

Kuishi utume

Mbali na huduma ya kichungaji na uongozi wa wanafunzi wa Sr. Grace, anahudumu kama kiungo cha mawasiliano ya Kanisa, akikusanya ripoti kuhusu shughuli za Kanisa na kuzishiriki na Radio Maria Papua New Guinea, na kuhakikisha kwamba kanisa la nyumbani linasikika na kuonekana.  Historia ya Sr. Grace si ya umaarufu bali ya uwepo, ushuhuda wa kile ambacho waamini wa mahali hapo wanaweza kutoa ukaribu na uelewa wa kina wa watu wanaowahudumia. Anawakilisha utume unaofikiriwa na mwanzilishi wa Shirika hilo miongo mitano iliyopita, dhamira ya kutembea na watu hasa pale ambapo kuna hitaji kubwa. Katika vijiji, vyuo vikuu, hospitali na kukutana kwa ajili ya sala kwa ajili  ya Papua New Guinea, inafanya utume huo kuendelea kuzaa matunda ya utulivu na pia ya kudumu.

Catholic Students Association at the University on an outreach service in the community.

Chama cha Wanafunzi Katoliki katika Chuo Kikuu kwa ajili ya kuhudumia jumuiya. 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

06 Februari 2026, 09:40