Askofu Mattew Hassan Kukah, wa Jimbo la  Sokoto (Nigeria) Askofu Mattew Hassan Kukah, wa Jimbo la Sokoto (Nigeria) 

Nigeria,Askofu wa Sokoto:Kila siku nchini Nigeria kuna mauaji:jinsi gani nchi isonge mbele?

Askofu wa Sokoto anauliza swali kwamba ni jinsi gani Nchi kwa ujumla inaweza kuendelea mbele kutokana na kwamba kila siku katika nchi hiyo kuna mauaji?Kuhusiana na hili,Askofu huyo anabainisha kwambasuala hili lazima lishughulikiwe kitaasisi.Alionya:"Nchi inayokumbwa na vurugu za kawaida na mgawanyiko unaoongezeka ina hatari ya kupoteza mwelekeo wake wa kimaadili na kitaasisi mpaka viongozi wake wachague umoja badala ya udini."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hakuna nchi yoyte ambayo watu 10  wanakufa  Jumatatu, 50 Jumanne na 100 Jumatano, na hiyo inaendelea kila Juma. Inawezekanaje nchi kwa ujumla inaweza kwenda mbele? Ni maswali ya Askofu Matthew Hassan Kukah,  wa Jimbo katoliki la Sokoto nchini Nigeria. "Kinachoendelea Nigeria hakiwezi kutokea Sudan, Camerun, Niger, Ghana, au nchi nyingine yoyote duniani," aliongeza, akizungumza huko Yola, mji mkuu wa Mkoa wa  Adamawa, wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha wasifu wa Gavana Ahmadu Fintiri.

Kukosoa vyombo vya habari vya magharibi

Askofu wa Sokoto pia alikosoa kile alichokielezea kama tabia inayoongezeka ya kupanga mauaji, kulingana na vigezo vya kidini, akionya kwamba masimulizi kama hayo huongeza kutoaminiana na kupanua mistari ya makosa kati ya jamii. Askofu Kukah alikosoa haya hivyo hasa jinsi vyombo vya habari vya Magharibi vinavyoonyesha mauaji nchini mwake kwamba utaona kuwa: "Ni nchini Nigeria pekee ambapo Wakristo na Waislamu hufa. Vyombo vya habari vya Magharibi huchochea mauaji ya kidini vinaporipoti historia kama: 'Wakristo 20 wameuawa, Waislamu 30 wameuawa.'"

Mgawanyiko unaoongezeka

Kulingana na Askofu Kukah, suala hilo,  lazima lishughulikiwe katika ngazi za kisiasa na kitaasisi, likiwahusisha viongozi wa kidini na jamii, akisisitiza kwamba amani haiwezi kupatikana bila uwajibikaji wa pamoja. Hasa, aliwataka viongozi wa kisiasa na kidini kufanya kazi ili kuimarisha taasisi, ili waweze kuhakikisha usalama, haki, na mshikamano wa kitaifa. Askofu Kukah alimalizia kwa kuonya kwamba "nchi inayokumbwa na vurugu za kawaida na mgawanyiko unaoongezeka ina hatari ya kupoteza mwelekeo wake wa kimaadili na kitaasisi mpaka viongozi wake watakapochagua umoja badala ya udini."

Askofu wa Sokoto nchini Nigeria

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

04 Februari 2026, 11:36