Sr Jacqueline Githiri, VDM, wakat kutoa ushauri na wahitaji. Sr Jacqueline Githiri, VDM, wakat kutoa ushauri na wahitaji.   #SistersProject

Kenya:Kurejesha familia na kuponya mioyo kwa upendo

Kupitia ushauri na mwongozo wa kiroho na kujitolea kwao kwa wote bila kuchoka,Sr.Jacqueline Githiri,VDM,hutembea na waliopondeka mioyo katika maisha na kuwasaidia watu kutoka nyanja zote za maisha wanapopambana na vurugu za majumbani na mfadhaiko nchini Kenya.

Na Sr. Christine Masivo, CPS.

Shirika la Jimbo la Mabinti wa Maria kutembelea Elizabeti, nchini Kenya, kwa kifupi wamejitolea na wanaendelea katika maisha yao kuponya mioyo ya waliopondeka na kurejesha matumaini kwa waliokata tamaa, kupitia Programu zinazounga mkono uponyaji wa Familia, na utunzaji wa kichungaji. Na hizo zimejikita katika karama yao ya: kurejesha familia kupitia imani, upendo, na huduma, Mafungo ya kiroho na upyaishwaji kiroho, huduma ya kutembelea nyumba kwa nyumba, maandalizi ya Sakramenti ya ndoa, Utume wa Parokia na ufikiaji wa jamii, usaidizi wa wajane na wanawake wasio na waume na hatimaye ufundaji wa imani kwa watoto na vijana. Kwa upande wa  Sr. Jacqueline Githiri,VDM, wa Shirika hilo, kwa hakika anasimama kidete kama taa ya huruma na ustahimilivu katika uwepo wake kuwatumikia wote kama mtawa wa Shirika hilo(https://visitationdaughtersihm.org/).

Huduma yetu

"Shirika letu bado ni jipya, lilianzishwa mwaka 2020, katika Jimbo Kuu la Kisumu nchini Kenya. Huduma yetu, yenye mizizi katika karama yetu, ni urejesho wa kiroho wa familia, tukielewa kwamba leo hii familia nyingi zinapambana na masuala mengi, hasa yanayohusiana na talaka na masuala mengi ya mfadhaiko yanayoathiri maisha ya familia," Sr. Jacqueline alisimulia.n"Tuligundua kwamba matatizo mengi yanatokana na upweke na utupu wa kiroho na kwa hivyo tunahisi kuitwa kuhudumia familia kutoka chini alisema, huku akibainisha kuwa “Shirika lake linahudumu katika kutoa ushauri kijamii na katika kazi ya kichungaji.”

Utume na wito

Kupitia ushauri na mwongozo wa kiroho na kujitolea kwao kwa wote bila kuchoka, Sr. Jacqueline hutembea nao katika maisha na kuwasaidia watu kutoka nyanja zote za maisha wanapopambana na vurugu za majumbani na mfadhaiko. Yeye huwahudumia vijana na hata Watawa na Mapadre wanaohitaji mwongozo wa maisha, ili kugundua upya utu wao na amani yao ya ndani.

“Niligundua wito wangu wa kuongoza na ushauri, huku nikifanya malezi baada ya kozi yangu ya Katekesi. Watu wengi walikuja na mahitaji yao mbalimbali na sikuweza kuwasaidia baadhi yao," alieleza. "Niliomba na Mungu akajibu maombi yangu na nikajiandikisha kusoma Diploma ya Uzamili katika ushauri nasaha wa mtu binafsi na kikundi kwa ajili ya utume wangu.”

Sr. Jacqueline Githiri, VDM on pastoral ministry with some villagers

Sr. Jacqueline Githiri, VDM katika huduma ya kichungaji na baadhi ya wanakijiji 

Kutembeea pamoja na urejesho

Huduma ya Sr. Jacqueline imegusa maisha ya wengi na kubadilisha maisha yake binafsi. Anakumbuka matukio mawili yaliyoacha alama kubwa. Mama mmoja alimjia akiwa na huzuni sana, baada ya kukataliwa na mumewe, kupigwa, na baadaye kuachwa alipokuwa mjamzito. Sr acqueline alitembea kwa kumuongoza huyo mwanamke na  kumpitia ushauri huku akimtia moyo na kumsaidia kugundua tena maana ya maisha, licha ya matatizo yote aliyokuwa akipitia. “Tulitembea pamoja hadi alipokuwa sawa tena,” alibainisha mtawa huyo. “Kwa sasa huyo mama alijaliwa kuwa na watoto mapacha, na hii inanipatia furaha kubwa kumuona akiwa na furaha sana. Amefanikiwa kupata kazi, na sasa anaweza kuwatunza watoto wake watatu.”

Historia kama hizo zinathibitisha imani

Kisa kingine kilikuwa mtawa ambaye alikuja akiwa na msongo wa mawazo sana, na Sr Jacqueline aliomba Jumuiya yake ili aweze kutembea naye na kumwongoza katika  hali hiyo. “Pole pole, alipata nafuu na akapona, na tuliweza kumrejesha tena na kwenye Shirika lake. Sasa yuko mzima na anafanya kazi tena.” Historia kama hizo zinathibitisha imani ya Sr Jacqueline kwamba uponyaji unawezekana wakati watu wanachukuliwa kwa upendo na uvumilivu. “Nimejifunza kwamba watu si wabaya,” alisema. “Mara nyingi wao ni waathiriwa wa malezi yao, uzoefu, au mazingira yao. Hilo limenifundisha kuwaombea watu, na si kuwahukumu.”

Group discussion during sessions on counselling

Kujadiliana katika makundi wakati wa kutoa ushauri

Rasilimali na faragha

Licha ya furaha ya huduma yake, Sr Jacqueline anakabiliwa na changamoto kubwa. "Baadhi ya visa vinahitaji kufuatiliwa, lakini hatuna mahali pa kuweza kuwaweka wao kukaa nasi ili tuwasaidie katika safari hii ya uponyaji kwa karibu. Hii ni zaidi kwa waathiriwa wa migogoro," alisimulia. "Nimekuwa na visa vingi vilivyohitaji huduma, ikiwa ni pamoja na msichana ambaye alinusurika shambulio la kikatili la familia na nyingine ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu aliyekuwa anasumbuliwa na mfadhaiko mkali na alihitaji uangalifu na ufuatiliaji."

Sr Jacqueline hakuweza kuwashughulikia "inanisikitisha sana," alisisitiza. Ndoto yake ni kujenga Kituo cha Marejesho ya Familia, mahali salama ambapo wale wanaopambana na majeraha ya kihisia au kisaikolojia wanaweza kupata makazi ya muda na huduma kamili. "Kituo hiki pia kitatumika kama kituo cha mafunzo na uelewa kwa familia," alielezea. "Watu wengi huanguka katika mfadhaiko kwa sababu hakuna kinga na hakuna uingiliaji kati wa mapema. Tunatumaini kwamba tunaweza kubadilisha hilo na kuwa  kama daraja la  Shirika."

Katika huduma yake, Sr. Jacqueline anafanya kazi kwa karibu na mapadre, watawa, na watu walei wa kawaida. Anaweka siku maalum kwa kila kikundi ili kuhakikisha usiri na heshima. Kwa sasa katika Shirika lake kuna watawa wawili waliohitimu kuwasaidia watu wenye visa kama hivi na mwingine yuko kwenye nyumba ya malezi katika Shirika lao kuwasaidia wasichana ambao wameonesha nia yao ya kujiunga na Shirika lao ili kumtumika Mungu. Kwa pamoja, wao hutoa semina, warsha, na vikao vya mtu binafsi wakati mwingine chini ya hali hii ngumu. "Hivi sasa, ninatumia chombo kidogo cha usafirishaji kama ofisi yangu ya ushauri," alisema na kuongeza kuwa “lakini tuna imani kwamba siku moja, Mungu atatupatia  mahali pazuri zaidi."

Counseling session

Wakati wa kutoa ushauri

Kenya:Kurejesha familia na kuponya mioyo kwa upendo

Kupitia ushauri na mwongozo wa kiroho na kujitolea kwao kwa wote bila kuchoka,Sr.Jacqueline  Githiri,VDM,hutembea na waliopondeka mioyo katika maisha na kuwasaidia watu kutoka nyanja zote za maisha wanapopambana na vurugu za majumbani na mfadhaiko nchini Kenya.

Kukua kupitia huduma na ushirikiano

"Huduma yangu imefungua macho yangu kwa maumivu ya watu na kunifanya niwe na huruma zaidi," alisema Sr. Jacqueline. "Ninaona kila mtu anaweza kufanya mema mara tu anapoeleweka na kusikilizwa." Sr. Jacqueline anawasihi watawa wenzake na mapadre kuwasikiliza watu. "Popote tulipo, mapadre, watawa wa kike na kiume, ni vema tukubali kutoa na kupokea ushauri," alisema.  "Sio taaluma tu, bali ni utume wa uwepo na watu wanotuhitaji sana. Wengi wanaumia na shida chungu nzima na wanahitaji watu wakutembea nao katika safari hii ya  Ushauri wa Familia na utunzaji wa kichungaji.”

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Bonyeza hapa tu: Just click here.

09 Februari 2026, 11:43