Kard.Marengo:kwa Wakristo kuna hatari kuchukulia uwepo wa Kanisa
Na Sr Ernestina Patrick Lasway – Vatican.
Kardinal Giorgio Marengo, Mmisionari wa Shirika la Waconsolata na Balozi wa Vatican huko Ulaanbaatar nchini Mongolia, akiwa katika Kanisa la Mtakatifu Petro huko Hazel Grove, Stockport, nchini Uingereza, aliwambia kuwa “Ninaona kwamba ninyi ni jumuiya hai na yenye nguvu! Na kwa sisi tunaotokea kwenye utamaduni wa Kikristo, kuna hatari ya kuchukulia uwepo wa Kanisa kuwa jambo la kawaida.”
Kardinali Marengo aliwahimiza umuhimu wa kutambua na kuthamini kwa shukrani hali ya “kuweza kusikiliza maneno ya Yesu mara nyingi kadiri tupendavyo. Tuna bahati kubwa ya kupokea sakramenti za kanisa.” Kwa njia hiyo ziara ya hivi karibuni ya Kardinali Marengo nchini Uingereza imekwenda sambamba na mikutano na mazungumzo mengi. Kufuatia mwaliko wa Padre Anthony Chantry, Mkurugenzi wa Kitume wa Mashirika ya Kipapa na Kimisionari nchini Uingereza na Wales(PMS) Balozi wa Vatican huko Ulaanbaatar alipata fursa ya kushirikisha uzoefu wake wa kitume wa kimisionari nchini Mongolia katika nyakati mbalimbali kuanzia tarehe 2 hadi 6 Februari 2026.
Maendeleo ya Mongolia tangu 1992
Akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides, Kardinali Marengo alisisitiza kuwa, huo ulikuwa wakati muhimu wa kwa kukutana na kushirikishana uzoefu. Ziara hii iliambatana na sherehe na matukio ya kuhmaisha yaliyoandaliwa huko London - Stockport- Manchester, na Birmingham. Watu wa kujitolea na wafadhili wa Utume wa Uongereza (Missio UK,) pamoja na wanafunzi wa Seminari, walikuwa miongoni mwa wale ambao Balozi wa Vatican huko Ulaanbaatar alikutana nao wakati wa ziara yake nchini Uingereza, na akiwa nao alijadili maendeleo ya jumuiya ya Kikatoliki huko Mongolia tangu mwaka 1992.
Najivunia kuwafanya utume Mongolia
“Najivunia kuwa ninafanya utume Mongolia,” Kardinali Marengo alisema wakati wa mahubiri katika maadhimisho kwenye Kanisa la Mtakatifu Petro huko Hazel kwamba, “nina bahati ya kuwafundisha watu ambao bado hawajawahi kumjua Mungu.” Aliongeza kwamba, nchini Mongolia, hilo si jambo la kawaida, “hivyo watu wanaobadili dini yao kuwa Ukristo wakati mwingine hukumbana na upinzani na hawafahamiki kikamilifu. Ndiyo maana sala zenu, msaada wenu, na shauku yenu kwa kile kinachoendelea huko ni faraja kubwa kwao.” Mmisionari na Kardinali alisema, “katika muktadha kama ule wa Mongolia leo, kila kitu kinazunguka kuhusu ukweli wa kukutana: “Kukutana na Yesu ni jambo bora zaidi linaloweza kutokea maishani mwako. Na ikiwa hakuna mtu anayejitolea kwa Yesu ili wengine wapate kumjua, hilo litakuwa gumu kufanikisha. Roho Mtakatifu anaweza kufanya chochote, lakini Kristo kawaida hufanya kazi kupitia nafasi za kukutana ambazo sisi tunazianzisha.”
Kardinali Mareno na wanafunzi wa Chuo Kikuu
Akiwa mbele ya wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Agostino huko Stockport, waliungwa mkono na kundi dogo kutoka shule ya Mtakatifu James, Kardinali Marengo, alizungumza kuhusu uzoefu wake kama askofu wa jumuiya ndogo ya Kikatoliki yenye wanachama 1,450 tu, akianza na hatua za mwanzo za huduma yake nchini Mongolia,na miradi mingi ya kijamii imeanzishwa, ikiwemo vituo vya kuchezea watoto, shule za ufundi, kniniki, nyumba za wazee, makazi kwa wasio na makazi, na kituo kwa vijana wenye ulemavu. Vituo hivi na miradi ya kijamii hutoa huduma kwa wakazi wote wa eneo hilo. Wakati wa ziara hii, Kardinali pia alipata nafasi ya kujibu maswali ya wanafunzi. “Kukutana na Kardinal ilikuwa fursa ya pekee na adhimu. Maneno yake yalinigusa sana hadi nikatamani kupata uzoefu wa kimisionari katika siku za usoni,” alisema hayo Louisa, mwanafunzi wa darasa la kumi na mbili. “Nafurahi,” aliongeza, “kuwa nilipata nafasi ya kukutana naye; na hivyo kukutana kwetu kulikuwa na mafanikio makubwa kwa sisi sote.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here