2025.09.30 Little Servants to the Poor (French: l’Institut des Sœurs Oblates catéchistes Petites Servantes des Pauvres

Malawi,Siku ya Watawa Duniani:Wito wa umoja katika Kristo!

Mapadre,watawa na mabruda zaidi ya 2,000 kutoka katika majimbo yote nchini Malawi walikusanyika kusherehekea Umoja wa umisionari wa Kipapa na Siku ya Watawa Ulimwenguni kwa kuongoza nwa kaulimbiu:"Umoja katika Kristo."Maaskofu waliwataka wanaume na wanawake waliowekwa wakfu kuimarisha ushirika wao,kuwahudumia walio katika mazingira magumu na kuendelea kuzingatia wito wao wa kimisionari.

Na Sr. Christine Masivo CPS - Vatican.

Mnamo tarehe 7 Februari 2026, Kanisa nchini Malawi lilisherehekea Siku ya Watawa Ulimwenguni na Umoja wa Umisionari wa Kipapa kwa njia maalum, kama inavyofanyika kila mwaka. Mapadre zaidi ya 600 wa jimbo, watawa wapatao 1,500, na mabruda 200 wanaohudumu Malawi yote walikusanyika kusherehekea kujitolea kwa pamoja na kwa umoja, huduma, na ari ya kimisionari chini ya kaulimbiu: "Mapadre na watawa, muwe wamoja katika Kristo, muungane katika utume." Hafla hii iliadhimishwa na sala, tafakari, na kujitolea upya kwa utume wao wa uinjilishaji.

Sherehe huko Dedza

Mwaka huu 2026, sherehe zilianza katika jimbo la Karonga mnamo  tarehe 2 Februari  na kwenye majimbo mengine, sherehe zilifanyika Jumamosi tarehe 7  Februari.  Sherehe ya kitaifa ilifanyika latika jimbo la Dedza, katika Parokia ya Mtakatifu Martin de Porres. Askofu Peter Adrian Chifukwa aliongoza Ekaristi Takatifu, na aliwaalika watu waliowekwa wakfu kuwa ishara inayoonekana ya Kristo, hasa miongoni mwa walio katika mazingira magumu zaidi. Aliwataka wote kutembea karibu na maskini, wazee, na walioachwa, ili uwepo wa Mungu uweze kupatikana kila siku. Askofu aliwatia moyo wasifikirie magumu wanayopitia katika huduma, bali wategemee baraka ambazo Mungu hutoa kupitia huduma yao kwa kanisa.

Umoja kwa ushuhuda wa kila siku

Magochi: Katika jimbo la Mangochi, sherehe zilifanyika katika Parokia ya Mtakatifu Louis Marie de Montfort huko Balaka na Askofu Montfort Stima. Alisisitiza kwamba umoja katika Kristo unaonyeshwa kupitia huduma ya kila siku. Mapadre watawa wa kiume na kike walikumbushwa kwamba kazi yao si jukumu la kitaasisi tu bali ni ushiriki katika utume wa Kristo mwenyewe.

Mzuzu: Askofu Yohane Suzgo Nyirenda kutoka jimbo la Mzuzu, katika Parokia ya Mtakatifu Austine alisisitiza kwamba, ushirikiano wa kweli na umoja kati ya mapadri na watawa wa kike na kiume ni muhimu kwa uinjilishaji wenye ufanisi.

Kujikita katika Kristo, ni kujitolea kwa utume

Katika Kanisa kuu la Zomba, Askofu Alfred Mateyu Chaima aliwahimiza watawa wa kike na kiume kama mchungaji: "Simamishaeni utume wenu katika muungano mkubwa na wa kibinafsi na Kristo, mkikumbuka kwamba kina cha kiroho huendeleza huduma yenye matunda," alisema.

Lilongwe: Askofu Mkuu George Desmond Tambala, kutoka jimbo Kuu ya Lilongwe katika Parokia ya Mtakatifu Francis aliwahimiza mapadri na watawa "muishi wito wenu kihalisi na kwa furaha; kanisa linashukuru kwa huduma ya ukarimu, kwani nyinyi ni hazina ya thamani kwa kanisa, na mnahitaji kubaki imara na wenye ujasiri katika wito wenu."

Chikwakwa: Askofu Peter Musikuwa kutoka jimbo la Chikwawa pia alijiunga na mapadre, watwa wa kike na kiume katika sala akiwashukuru kwa kujitolea kwao na kuwatia moyo waendelee katika kutoa ushuhuda kwa Kristo.

Ushirika Uliofanywa Upya

Sherehe hizo ziliadhimishwa kwa roho ya shukrani na upya pamoja na ujumbe ulio wazi na thabiti kwamba umoja miongoni mwa mapadri, watawa, na ndugu si jambo la hiari bali ni muhimu kwa utume wa kanisa. Waamini wote walihimizwa kuendelea na maisha na huduma yao katika parokia, shule, hospitali, na jamii za mbali. Wito unasikika tena, kuwa wamoja katika Kristo, wakiwa wameungana katika utume ili kupitia maisha yao, uso wa Yesu uweze kufunuliwa kwa taifa.

 

13 Februari 2026, 15:18