Kwa heshima ya utakatifu wake,Sanamu ya Mtakatifu Carlo Acutis ilizinduliwa nchini Myanmar. Kwa heshima ya utakatifu wake,Sanamu ya Mtakatifu Carlo Acutis ilizinduliwa nchini Myanmar. 

Myanmar:Sanamu ya Mtakatifu Carlo Acutis imewekwa kama ishara ya matumaini

Sanamu ya Mtakatifu Carlo Acutis imezinduliwa nchini Myanmar na Padre John Aung Htoi alielezea kuwa itakuwa mfano kwa vijana wa jinsi ya kuishi imani yao,"hata wakati wa majaribu,hasw wakati huu mgumu ambao taifa linapitia."

Na Kielce Gussiena  - Vatican.

Katikati ya mgogoro mgumu wa wenyewe kwa wenyewe, Kanisa Katoliki la Myanmar limetoa ishara ya matumaini na mwanga kwa maelfu ya vijana wanaoishi huko. Sanamu ya Mtakatifu wa Italia aliyevaa viatu vya michezo, Mtakatifu Carlo Acutis, imejengwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Columbanus katika jimbo la Myitkyina, ambayo ni mji mkuu wa Jimbo la Kachin.

Shuhuda katikati ya uwanja wa vita

Kulingana na Shirika la habari la Vatican, la Kimisionari  Fides uzinduzi huo  ulikuwa wa kwanza wa aina yake nchini Myanmar na ulifanyika katika kumbukumbu ya miaka kumi ya ukuhani na kumbukumbu ya kwanza ya kuwekwa wakfu kwa Askofu John La Sam wa Jimbo Katiliki hilo.  Mmoja wa mapadre wa jimbo ,  Padre  John Aung Htoi alielezea nia ya wakati huu wa kihistoria.

Lengo la sanamu hiyo, alisema, ni kwamba Mtakatifu Carlo Acutis anaweza kuwafundisha vijana "jinsi ya kutoa ushuhuda wa imani katika maisha yao, hata wakati wa majaribu, hasa wakati huu mgumu ambao taifa linapitia." Sanamu hiyo imekusudiwa kutumika kama ukumbusho na msukumo kwa vijana kuhusu jinsi ya kuishi imani yao nchini Myanmar kupitia matumizi sahihi ya mtandao na mitandao ya kijamii.

Myanmar Catholics praying in St. Mary's Cathedral in Yangon

Waamini katika kanisa Kuu la Myanmar wakisali

Kwa kuwa Mtakatifu Carlo ndiye Mlinzi wa mtandao, Padre Htoi alimtaja kama mfano kwa vijana nchini  humo ambao "lazima wapitie na kunusurika mgogoro huu unaoathiri nchi iliyogawanyika na vita vya wenyewe kwa wenyewe." Alisimulia jinsi wanavyokabiliana na "vitisho vya kijamii na kimaadili," kama vile vurugu, uhalifu, dawa za kulevya, mmomonyoko wa kiungo cha familia, na mitandao ya kijamii bila ulinzi wa kisheria. Ni katika muktadha huo  ambapo vijana hawa hugeukia Kanisa Katoliki na mafundisho yake yenye misingi imara, ambayo huwatia moyo kutegemea maisha yao kwa Kristo. Ili kuwasaidia, Padre Htoi alibainisha kwamba, majimbo kote nchini hupanga kambi za vijana, programu za malezi ya imani, na programu za elimu kama njia ya kusindikizana na vijana katika safari yao.

Katika hatari ya kuwa "kizazi kilichopotea"

"Vijana nchini Myanmar lei hii wanahitaji uelewa, mwongozo, na uaminifu," Padre alisisitiza. Kwa upande mwingine, lazima pia wachukue jukumu la matendo yao. Padre Htoi alielezea, "vijana ni rasilimali muhimu kwa siku zijazo, na kwa hivyo lazima tuwatunze."

Nchi nzima ya Myanmar  hasa pale ambapo migogoro na vurugu zinaendelea, vijana wanajikuta katika sehemu iliyo hatarini sana ya idadi ya watu. Wengi hawana makazi, wengine ni yatima au hawana familia zinazoweza kuwalinda, hivyo basi, kuwaacha katika hatari ya kuwa "kizazi kilichopotea." Katika roho ya kupambana na changamoto hizi, Kituo cha Vijana cha "Don Bosco", kilichoanzishwa mwaka 2014 katika Jimbo Kuu la Mandalay, vijana wapatao 60 wanaishi hapo wanaotoka katika mazingira magumu mara nyingi yatima au wale wanaoishi mitaani. Katika kituo hicho, vijana hupokea huduma, malazi, chakula, masomo, huduma za afya, na elimu pamoja na michezo, muziki, na shughuli za kiutamaduni kama sehemu ya karama ya wamisionari wa Salesian. Mapadre wa Salesian walibainisha kuwa dhamira yao "ni kuwasindikiza katika ukuaji wao kwa usalama, heshima, na matumaini."

Myanmar soldiers guard a captured methamphetamine lab near Namlan in Shan State

Mabadiliko katika mtazamo

Kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021, ambayo yalivunja mchakato dhaifu wa kidemokrasia karibu muongo mmoja uliopita nchi ya Myanmar ilianguka katika wakati muhimu katika historia yake. Maelfu ya vijana waliandamana kwa amani kwa ajili ya kurejeshwa kwa demokrasia kabla ya kujiunga na vikundi vya upinzani wenye silaha. Miaka mitatu baadaye, jeshi lilitekeleza sheria ya uandikishaji, na kulazimisha vijana wapatao 60,000 kutumwa mstari wa mbele kwenye vita. Kwa hivyo, karibu vijana 100,000 wamehamia, hasa Thailand, au wamejificha. Vijana, kati ya umri wa miaka 15 na 35, ni asilimia 33% ya idadi ya watu wa Myanmar, wakiwa na umri wa wastani wa miaka 27.  Kwa wengi katika kundi hili la watu, mapinduzi ya 2021 hayawezi kuelezewa tu kama tukio la kisiasa, kwani yaliathiri watu binafsi katika uzoefu wao binafsi wa kidemokrasia na uhuru wa mtu binafsi.

24 Januari 2026, 16:22