Msumbiji:Kanisala Nampula linatafuta kujiendeleza kwa mpango wa kichungaji 2025-2026
Na Cremildo Alexandre – Nampula.
Akiongozwa na kauli mbiu ya Injili, "Wapeni kitu cha kula," Askofu wa Nampula alitoa wito wa kushiriki, kusimamia rasilimali, na kujitolea kwa jamii ndani ya Kanisa lao lililoitwa kuwahudumia maskini zaidi na kuishi kwa uwajibikaji ndani ya rasilimali zake.
Wapeni kitu cha kula
Jimbo Kuu la Nampula linaanza mwaka wa kichungaji wa 2025-2026 chini ya mada ya Kibiblia: "Wapeni kitu cha kula" (Mt 14:16), iliyopendekezwa na Askofu Mkuu Inácio, kama mwongozo wa kiroho na kichungaji kwa familia nzima ya jimbo kuu. Uchaguzi wa kauli mbiu hii unaweka jukumu la jamii, kushiriki, na ufuatiliaji wa haraka wa juhudi za kujiendeleza kiuchumi za Kanisa la mahali hapo katikati ya huduma ya kichungaji. Katika Barua yake ya Kichungaji, Askofu Mkuu alisisitiza kwamba, ukweli wa Jimbo Kuu unaonyesha tofauti kubwa: huenda ikawa tajiri kwa watu wake na malighafi, lakini ni maskini kwa kiasi kikubwa katika suala la mali halisi. Kwa Askofu Mkuu Inácio, kujiendeleza si jambo la kiutawala tu bali pia ni sharti la kiinjili, kwani utume wa Kanisa inahitaji mipango na programu za kichungaji zinazosimamiwa vizuri na kufadhiliwa vizuri.
Fedha za Kanisa si mwiko
Hati ya jimbo Kuu la Nampula inasisitiza kwamba kujadili fedha za Kanisa haipaswi kuwa mwiko kamwe. Kinyume chake, ni kipimo muhimu ili kuhakikisha uadilifu, uhuru, na ufanisi wa misheni ya kichungaji. "Wema wa kiroho hauwezi kutenganishwa na wema wa kimwili," anathibitisha mchungaji mkuu wa jimbo, akitaka usimamizi wa fedha ulio wazi, uliopangwa, na unaowajibika, ukijengwa juu ya juhudi ambazo tayari zimeanzishwa katika mipango ya awali ya kichungaji. Askofu Mkuu Inácio pia anakumbuka kitendo cha Yesu cha kuzidisha mikate, akisisitiza kugawana kama jibu halisi kwa ukosefu wa usawa wa kijamii na umaskini unaoathiri familia nyingi katika Jimbo Kuu la Nampula. Ukweli wa ukosefu wa ajira, riba, ukosefu wa huduma za afya, elimu, na lishe ya kutosha, miongoni mwa mambo mengine, unaipa changamoto Kanisa la Msumbiji kuwa ishara ya matumaini, udugu, na utunzaji wa pande zote.
Kanisa linaloongozwa na mshikamano zaidi
Kwa kutafakari historia, Barua ya Kichungaji inakumbuka safari ya Kanisa nchini Msumbiji, kutoka enzi za ukoloni hadi uhuru, baada ya uhuru kama kifungu kinachojulikana kwa migogoro na vipindi vifupi vya ushirikiano na Serikali. Kulingana na Askofu Mkuu, kuna haja ya ushirikiano mzuri na uhusiano kati ya Kanisa na serikali. Kipengele muhimu cha uhusiano huu kinapaswa kutambuliwa na Kanisa lisilo na utegemezi, ili lidumishe uhuru wake na aminifu kwa dhamira yake kuu ya uinjilishaji. Kwa kumalizia, Askofu Mkuu Inácio anatoa wito kwa parokia, jumuiya, harakati, na Wakristo wote kuchukua umiliki na kujitolea "kuwalisha" wengine: kushiriki walichonacho, kuepuka upotevu, kutunza mali za pamoja, na kujenga Kanisa linaloendeshwa na mshikamano zaidi, uwajibikaji, na linalojitegemea huko Nampula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here