Maaskofu wa Costa Rica wahimiza uwajibikaji kabla ya uchaguzi wa Februari
Na Sr. Christine Masivo CPS – Vatican.
Wakati nchini Costa Rica inakaribia Uchaguzi wake Mkuu tarehe 1 Februari 2026, Baraza Katoliki la Maaskofu nchini humo wametoa wito wa kichungaji wakiwataka raia kufufua kujitolea kwao kwa ajili ya maisha ya kidemokrasia. Kulingana na ripoti ya Shirika la Kipapa la habari za Kimisionari Fides, wakizungumza kupitia ujumbe wa pamoja uliotolewa huko Mtakatifu José, Maaskofu walithibitisha tena dhamira ya Kanisa ya “kuunda dhamiri, kuelimisha Injili, na kupyaisha kujitolea kwa raia kwa waamini,” huku wakisisitiza kwamba kura ijayo ni kama wajibu wa kiraia na wajibu wa kimaadili.
Wito wa Maaskofu katika wakati muhimu wa Kidemokrasia
Wakionesha wasiwasi kuhusu viwango vya juu vya kihistoria vya kutopiga kura, Maaskofu walihimiza ushiriki wenye taarifa, ufahamu, na matumaini katika uchaguzi kama mchango muhimu kwa manufaa ya wote na uimarishaji wa kidemokrasia. Ujumbe huo ulikuja wakati muhimu kwa taifa hilo.
Wanawake 5 wamo miongoni mwa wagombea 20 nchini Costa Rica
Raia wa Costa Rica watamchagua Rais wa Jamhuri na wabunge, katika uchaguzi wenye wagombea 20 wa urais, wakiwemo wanawake 5. Chini ya mfumo wa uchaguzi wa nchi hiyo, mgombea lazima apate angalau asilimia 40% ya kura zote katika raundi ya kwanza ili kuepuka duru ya pili. Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki alionesha wasiwasi mkubwa kuhusu kupungua kwa ushiriki wa uchaguzi, hali ambayo inatishia uhai wa Taasisi za Kidemokrasia za Costa Rica.
Wasiwasi kuhusu kuongezeka kutokupiga ura kwa wapiga kura
Hata hivyo wakivuta umakini kwenye uchaguzi wa rais wa 2022, Maaskofu walikumbuka kwamba zaidi ya wapiga kura milioni 1.4 waliostahiki walijizuia kupiga kura, na kusababisha kiwango cha juu cha kihistoria cha kutokupiga kura cha asilimia 40. Kwa Maaskofu, kiwango hiki cha kutokushirikishwa si takwimu tu, bali ni ishara ya taadari la kuongezeka kwa kukata tamaa na umbali kati ya raia na mchakato wa kidemokrasia. Uchaguzi ujao, walisisitiza, “unatoa fursa muhimu ya kubadilisha mwelekeo huu.”
Wito kwa vijana
Lengo kuu la ujumbe la Baraza la Maaskofu Katoliki kwa vijana, ambao walizungumza nao kwa dharura na matumaini walisema. "Nyinyi ndiyo mpo Costa Rica kwa sasa," waliwahimiza vijana huku wakiwasihi vijana kwenda kwenye uchaguzi kwa ufahamu, wa kumbukumbu, na "tumaini muhimu." Badala ya kujisalimisha kwa kutojali au kuchanganyikiwa, Maaskofu waliwatia moyo kujijughulisha wote, kushiriki katika mazungumzo, kulinganisha mapendekezo ya kisiasa, na kuweka mahitaji ya walio hatarini zaidi mbele ya maamuzi yao.
Kurejesha Matumaini katika Demokrasia
Maaskofu aidha walisisitiza kwamba demokrasia haiwezi kupyaishwa bila ushiriki hai wa vizazi vipya. Walibainisha kwamba nguvu zao, ubunifu, na hata upinzani wao wa kujenga, ni muhimu kwa kuunda jamii yenye haki na ushirika zaidi. Maaskofu kwa njia hiyo waliwakabidhi vijana wakiomba kwa "Bwana wa uzima na historia," ili wasirithi uchovu au kukata tamaa, bali wawe na hamu mpya ya kushiriki katika maisha ya umma na kujali manufaa ya wote.
Ujumbe huo pia uliwahusu Mapadre huku wakisisitiza jukumu lao katika kuhimiza uwajibikaji wa kiraia miongoni mwa waamini. Maaskofu walithibitisha, kupiga kura ni usemi halisi wa uwajibikaji wa kiraia" na njia halali ya kutafuta manufaa ya wote. Maaskofu walihimizwa kuwasaidia waamini kujielimisha, kutambua kwa busara, na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi, wakikumbuka kwamba mustakabali wa Costa Rica unajengwa kupitia ahadi zilizotolewa leo.
Siku ya uchaguzi inapokaribia, wito wa Maaskofu unasimama kama wito wa dhamiri kwa taifa zima. Wakiwa na mizizi katika maadili ya Injili na heshima kwa taasisi za kidemokrasia, ujumbe wao unawaalika Raia wote wa Costa Rica kuona "ushiriki katika uchaguzi Mkuu kuwa si tu kama haki, bali ni kama jukumu la pamoja kwa sasa na mustakabali wa nchi."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here