Kard.Ambongo:Miaka 30 baada ya'Ecclesia in Africa'inabaki kuwa dira ya Kichungaji
Na Sr. Christine Masivo, CPS, - Vatican.
Wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika ya Kati(ACERAC), uliokusanyika huko N’Djamena kuanzia Januari 25 hadi Februari 1, Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Kinshasa DRC, alisisitiza kwamba Wosia wa Kitume wa Baada ya Sinodi na Mtakatifu Yohane Paulo II ni wa dharura kwa Kanisa barani Afrika. Mada ya mkutano unaoendelea ni, "Changamoto za Kanisa, Familia ya Mungu Barani Afrika: Miaka 30 Baada ya Kanisa Barani Afrika."
Kanisa Barani Afrika kama "Familia ya Mungu"
Kulingana na shirika la kipapa la habari za kimisionari Fides, Kardinali Ambongo katika nafasi yake kama Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM), alibainisha umuhimu wa kudumu wa himizo hilo, ambalo lililiwasilisha Kanisa Barani Afrika kama "Familia ya Mungu." Akihutubia mkutano uliokusanyika N'Djamena akiielezea hati hiyo zaidi ya wazo la kitaalimungu. Kanisa Barani Afrika ilikuwa dira ya kweli ya kichungaji kwa bara linaloibuka kutoka katika ukoloni, udikteta na migawanyiko, ikizungumzia Afrika iliyo na imani hai na tumaini kubwa," alisema. Kardinali Ambongo alirudia maneno ya Papa Yohane Paulo II, mwishoni mwa Mkutano Maalum wa Sinodi ya Maaskofu wa Afrika, na ambaye alitaka Kanisa liumbe ushirika wenye mizizi katika upendo, upatanisho, haki, na amani.
Baada ya miaka 30 ya maono ni ya haraka zaidi
Kardinali Ambongo alisisitiza kwamba hata baada ya miaka 30, maono hayajapitwa na wakati na ni ya haraka zaidi. Na ni wakati wa kujichunguza kikanisa. "Inatualika kutambua kile kilichozaa matunda na kile kilichobaki dhaifu au kisichokamilika, huku tukiboresha kujitolea kwetu kwa utume tuliokabidhiwa." Ni wito kwa Kanisa kuwa wakala wa upatanisho, haki, amani na matumaini, waaminifu wa Injili, huku tukiendelea kujihusisha sana na hali halisi zinazokabiliwa na jamii za Kiafrika.”
Vipaumbele Vitatu vya Kichungaji
Kardinali Ambogo alibainisha vipaumbele vitatu vya kichungaji, ambavyo vimeongoza Kanisa la Afrika ya Kati na kwamba mkutano huo (ACERAC) unatakiwa kuviweka ndani. Kipaumbele cha kwanza ni uundaji wa wapatanishi: "Seminari zetu, vyuo vikuu vya Kikatoliki, na taasisi za elimu lazima ziunde wanawake na wanaume wenye uwezo wa kukuza amani," alisema, akisisitiza umuhimu wa kusisitiza malezi haya katika Injili, mafundisho ya kijamii ya Kanisa, na ujuzi wa vitendo katika mazungumzo na utatuzi wa migogoro.
Utawala wa kichungaji wa sinodi
Kipaumbele cha pili kinahusu utawala wa kichungaji wa sinodi.: Kardinali alitoa wito wa mchakato mgumu wa kusikiliza, uwajibikaji wa pamoja na uwazi katika ngazi ya kijiji na Parokia, ili kuruhusu kanisa kusonga mbele kwa umoja kama familia ambapo maamuzi hufanywa kwa pamoja.
Ushiriki wa kinabii wa kijamii
Kipaumbele cha tatu ni ushiriki wa kinabii wa kijamii: Kardinali alihimiza Kanisa kuendelea kuimarisha tume za haki na amani, kukuza elimu ya uraia, kuwasaidia waathiriwa wa vurugu, na kuunda nafasi za mazungumzo zinazokuza upatanisho na mshikamano wa kijamii. Kadri kikao kinavyoendelea, na Maaskofu wakitafakari pamoja, Kardinali Ambongo aliwahimiza Maaskofu hao kutafakari imani kwamba, baada ya miongo mitatu ya Wosia wa(Ecclesia in Africa), Kanisa barani Afrika, kuhusu Kanisa kuishi kihalisi kama Familia ya Mungu, bado ni dhamira muhimu na yenye kuleta mabadiliko kwa bara hilo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here