Ukraine,Balozi wa Vatican:“Tumejeruhiwa lakini Mungu yuko pamoja nasi”
Na Svitlana Dukhovych – Vatican.
Majengo elfu sita huko Kyiv hayajapata joto tangu January 9, kufuatia shambulio kubwa la Urusi. Kuanzia tarehe 16 Januari 2026, joto lilikuwa limezimwa karibu majengo 100 katika mji mkuu wa Ukraine, kulingana na Meya wa Mji huo Vitaliy Klychko, ambaye alisema kuwa wahandisi wa manispaa walifanya kazi kwa masaa kurejesha joto katika majengo yote. “Hali ya usambazaji wa nishati, ambayo nyumba kadhaa zinahitaji huduma hiyo, bado ni ngumu sana. Eneo la Kyiv bado linakabidhiwa na kukatika kwa Umeme,” aliongeza Klychko, hayo katika mahojiano aliyofanya na Vatican. Akizungumza na waandishi wa habari na baada ya mkutano na Rais wa Czech, Petr Pavel, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, alitoa shukrani zake kwa timu zinazofanya kazi bila kuchoka kila siku kukarabati miundombinu ya nishati ya umeme. “Tunajitahidi kila wakati kurejesha mitambo ya umeme na kuongeza uagiizaji na uwezo wa kiufundi, ambao pia uliharibiwa na mashambulizi ya kila siku ya Urusi,” alisema rais. Kwa njia hiyo Akizungumza na Vatican News, Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas, Balozi wa Vatican nchini Ukraine alieleza hali halisi ilivyo sasa na changamoto zinazowakabili wananchi.
Kwa kuzingatia shida ya nishati inayoathiri mikoa mbalimbali ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na mji mkuu wa nchi hiyo, wananchi wa Kyiv wanaendeleaje na wewe unaendeleaje katika utendaji wako utendaji katika Ubalozi wa Vatican?
Kwa sasa, kwa sababu ya vita, Ukraine ina uhaba mkubwa wa nishati kama matokeo ya milipuko ya mabomu ambayo ilipiga majiji na miji. Huku hali ya hewa ya baridi ya Januari ikisababisha kushuka kwa joto hadi nyuzi joto ishirini chini ya sifuri usiku, tunakabiliwa na hali ngumu, hasa huku Kyiv. Nimeambiwa na Maaskofu, Mapadre na Waamini walei, upo uhaba wa umeme hasa katika eneo la ukanda wa Magharibi . Nimepata taarifa pia kutoka kwa watu kadhaa kuwa wanapata umeme kwa masaa matatu tu kwa siku, kila siku. Kharkiv inapitia pia hali kama hiyo ambapo familia hupata vipindi vya siku mbili bila umeme au joto. Hii ina maana kuwa hata waokaji mara nyingi hawawezi kuoka mkate na kupata aina nyingine za chakula. Hivyo, uhaba wa chakula unasababishwa na uhaba wa nishati ya umeme, mbali na shida zinazowakabili raia kutokana na baridi. Hii inaonekana kufanana na mauaji ya kimbari ambayo Ukraine ilipitia katika miaka ya 1930. Tuna generata letu katika Ubalozi, hii ina maana kuwa tunaweza kuwa na mwanga, maji na joto kuliko watu wengine. Kama hali haitobadilika, inawezekana mji mkuu wote wa Kiukraine utahiji kuhamishwa kama meya wa Kyiv alivyosema siku za hivi karibuni.
Hivi karibuni uliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika madhabahu ya Maria ya Berdychiy katika kumbukumbu ya miaka 35 ya upyaishaji wa miundo ya Kanisa la Kilatini nchini Ukraine na uzinduzi wa mwaka wa Moyo Mtakatifu wa Yesu uliotangazwa na Maaskofu wa Kanisa la Kilatini kwa mwaka 2026. Je, una maoni gani kuhusu tukio hili lililotokea katika mazingira haya magumu?
Tulikuwa na maadhimisho muhimu kwa Kanisa Katoliki la Liturujia ya Kilatini nchini Ukraine katika Madhabahu kuu ya Berdychiv. Maaskofu wa majimbo ya Ukraine walikutana kwa maadhimisho haya mwanzoni mwa mwaka, uliowekwa wakfu kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, kuomba mapokezi ya Huruma, msamaha wa dhambi na ulinzi kutoka katika uovu wowote. Tuliomba kuwa wema wa Mungu ungeshinda dhambi na vita na kutupatia amani. Mwaka 2026, tutatumia muda mwingi kwenye familia na Parokia, na kila mtu anaaswa kuwa na Ibada thabiti kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu. Katika kumbukumbu ya miaka 35 ya kuanzishwa tena kwa uongozi wa Kanisa Katoliki la Kilatini mnamo tarehe 16 Januari 1991. Tunajua kuwa vita inasababishwa na matendo ya shetani, na shetani anaogopa kila tunapomwabudu Mungu, lakini tunafahamu na kuamini kuwa Bwana yupo pamoja nasi. Tulifanya sherehe hizi kwa ushirika na Papa Leo XVI pamoja na Kanisa kwa ujumla. Ilikuwa ni Ibada muhimu na yenye kugusa hisia kwangu, nina matumaini makubwa ya kuzaa matunda.
Ukiwa Berdychin, ulipata nafasi ya kuzumngumza na Maaskofu wa ukanda huo, hasa walioathiriwa na vita? Je Wewe uliwaonaje?
Nilikutana na Mkuu wa Kharkiv Zaporizhzhia na Msaidizi wake, na pia Askofu wa Odesa. Kiroho, nimewaona wote wakimtumaini sana Mungu. Huko Kharkiv, hawakuwa na umeme siku nzima, ni wakati wa kuchosha sana. Ninapenda kuongeza kuwa nimezungumza na Mkatoliki kutoka Sumy, ambaye anafanya utume mbalimbali wa kibinadamu katika eneo la Kharkiv. Aliniambia kuwa amechoka kisaikologia, kwani wenzake wawili waliuawa kwa kushambuliwa na ndege zisizo na rubani walipokuwa wakipeleka misaada eneo hilo. Kila anaposikia mnong’ono wa ndege zisizo na rubani, anakumbuka kwa hisia juu ya tukio hilo. Kwa sasa watu wengi wa Ukraine wamepigwa na kuumizwa vibaya na vita. Ni matumaini yangu kuwa kaka na dada zetu ulimwenguni pote mtashirikiana pamoja nasi kusali juu ya afya njema ya akili kwa ajili ya wale wote wanaopitia vita na madhara ya vita.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here