2025.12.22 Askofu  Bulus Dauwa Yohanna wa Jimbo la Kontagora nchini Nigeria. 2025.12.22 Askofu Bulus Dauwa Yohanna wa Jimbo la Kontagora nchini Nigeria.  (©Diocese of Kontagora)

Nigeria:Zawadi ya Noeli ya Kontagora:kurudi kwa watoto waliokuwa wametekwa nyara!

Askofu Bulus Dauwa Yohanna wa Jimbo Katoliki la Kontagora,Nigeria,Desemba 22 alithibitisha katika vyombo vya habari Vatican,kuachiliwa kwa wanafunzi 130 na wafanyakazi waliotekwa nyara kutoka Shule ya Msingi na Sekondari ya Mtakatifu Maria huko Papiri mnamo Novemba 21.Watoto na wafanyakazi walikuwa miongoni mwa waathirika 315 waliochukuliwa kwa nguvu na watu wenye silaha kutoka shuleni hapo usiku.

Na Paul Samasumo – Vatican.

Habari za kuachiliwa kwa watoto hao zilitangazwa kwa mara ya kwanza kwenye chapisho la X, na msemaji wa ofisi ya rais wa Nigeria. Kulingana na mamlaka ya Nigeria, hakuna waathiriwa kutoka Shule ya Mtakatifu Maria waliosalia Mateka. Katika ujumbe wake kwa Vyombo vya habari vya Vatican, baada ya kuachiliwa kwa watoto hao, Askofu Yohanna alieleza kufarijika sana, akihusisha maendeleo ya kabla ya Noeli na sala zinazotolewa na waamini Jimboni humo na duniani kote, pia aliwashukuru wote kwa umoja wao.

Jibu la maombi

"Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunijalia na kunilinda katika kipindi hiki kigumu sana. Jimbo Katoliki la Kontagora,  linafuraha kwa kuthibitisha kuachiliwa salama kwa kundi la pili la watoto waliotekwa nyara kutoka Shule ya Msingi na Sekondari ya kikatoliki ya Mtakatifu Maria huko Papiri. Maendeleo haya ni ushuhuda wa maombi yaliyojibiwa na nguvu ya imani katika kudumisha matumaini huku kukiwa na hofu kubwa," Askofu Yohanna alisema.

Alishukuru Shirikisho la Nigeria na mamlaka mahalia,  kwa kufanikisha kuachiliwa kwa watoto hao. "Kuachiliwa kwa watoto hao wakiwa salama, kuliwezekana kupitia juhudi madhubuti na zilizoratibiwa za Serikali katika ngazi ya Shirikisho na serikali. Mamlaka ilichukua hatua za kina ili kuhakikisha kuachiliwa kwao, ikiwa ni pamoja na msaada wa kisaikolojia, uchunguzi wa kiwewe, na matibabu kwa watoto wote," alisema askofu wa Kontagora.

Pongezi kwa Maafisa wa Usalama

Katika taarifa yake aliendelea kusema kuwa, "Ninatambua kwa shukrani nyingi taaluma na kujitolea kwa kikosi cha usalama, wafanyakazi wa matibabu, na washirika wote wanaohusika. Hiki kimekuwa kipindi cha changamoto kubwa, sio tu kwa watoto walioathiriwa lakini pia kwa wazazi wao, familia, Kanisa, na jumuiya nzima ya Kontagora. Wasiwasi, na hisia za kali  kwa kila mtu anayehusika ni nyingi kupita kiasi, ambazo bado tunashuhudia huruma ya Mungu kwa kuwarejesha watoto wetu kwa familia zao salama,” alisema.

Kuombea uponyaji

Tangu wakati huo Askofu alitoa wito kwa waamini wote na umma  duniani kote kuendelea kuombea uponyaji, na ulinzi wa watoto. "Pia natoa wito kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja na mashirika ya serikali, mashirika ya kidini, na mashirika ya kiraia, kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha usalama wa shule na watoto nchini kote," alisema. Aidha Askofu Yohanne alitoa wito kwa wanajumuiya wa Jimbo la Kontagora kuendelea kuwa waangalifu, wenye huruma na umoja katika kusaidia watoto na familia zilizoathirika ili kuhakikisha wanaunganishwa na kutunzwa kikamilifu katika kipindi hiki cha uponyaji. "Hili tukio  lituimarishe katika imani yetu na itukumbushe nguvu ya sala, umoja, na hatua ya pamoja katika kushinda hata hali ngumu zaidi," alisema Askofu Yohanna.

Kwa jumla, wanafunzi 303 na wafanyakazi 12 walitekwa nyara awali kutoka Shule ya Msingi na Sekondari ya Mtakatifu Maria huko Papiri, Jimbo la Niger, tarehe 21 Novemba. Hesabu ya mwisho, kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wamehesabiwa, ilikuwa ikiendelea kuanzia Jumatatu jioni.

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida kwa kubofya hapa: Just click here.

 

22 Desemba 2025, 19:30