Wanawake  wakiomboleza kupoteza maisha ya watoto wao katika maandamano ya Gen Z huko Kathmandu nchini Nepal hivi karibuni. Wanawake wakiomboleza kupoteza maisha ya watoto wao katika maandamano ya Gen Z huko Kathmandu nchini Nepal hivi karibuni.  (ANSA)

Nepal:Kanisa linashiriki dhamira ya vijana kwa mustakabali wa Taifa

Hali ya utulivu wa kiasi imerejea nchini Nepal, ufuatia siku kadhaa za maandamano na machafuko.Shule za Kikatoliki na za umma zimefunguliwa tena na maisha ya kila siku yamerejea polepole.Hayo yalielezwa na Padre Silas Bogati,Msimamizi wa Kitume wa Eneo la Nepal akibainisha juu ya hali ya sasa kama isiyo na uhakika na mvutano uliofichika,lakini yenye matumaini.

Sr. Christine Masivo CPS; -Vatican.

Imani imewekwa kwa uongozi wa Waziri Mkuu Sushila Karki, aliyepewa jukumu la kuiongoza nchi kupitia kipindi cha mpito cha miezi sita kabla ya uchaguzi mpya mwaka ujao. Akizungumza na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari (Fides), Padre Silas Bogati, Msimamizi wa Kipapa wa Eneo la Nepal, alielezea hali ya sasa kama isiyo na uhakika na mvutano uliofichika, lakini yenye matumaini."Kama jamii ya Wakristo Wakatoliki, tuna imani kwa Waziri Mkuu Karki," alisema. "Kama mwanasheria, alimtetea mmoja wa padri wetu na watatwa kadhaa walioshtakiwa kwa madai ya uwongo." Padre huyo alionesha matumaini kwamba Karki atahakikisha sheria inaheshimiwa na kanuni za haki zinafuatwa. Padre Bogati alitaja uwezekano wa maandamano zaidi yaliyoandaliwa na vyama vya kisiasa. "Tuna matumaini hayatasababisha vurugu," alisisitiza.

Vijana wanao mwamko wa maendeleo na ukuaji wa taifa

Wakati huo huo, msimamizi huyo alibainisha kwamba mwamko mapya katika jamii ya Nepal ya sauti ya vijana inayoongezeka, ya hisia ya uwajibikaji wa kiraia na kukuzwa na mitandao ya kijamii. Nepal ina takriban ya waktristu wakatoliki 8,000 katika ya 30,000 nchi nzima. "Vijana hawa wanatuma ujumbe thabiti, 'Tunajali,' wakionyesha mwamko wa kina wa wajibu wao kwa maendeleo na ukuaji wa taifa," alisema Padre Bogati. "Hii ni dalili chanya, ikizingatiwa kubaki kwenye misingi ya amani na haki." Msimamizi wa Kipapa alisema msimamo wa Kanisa ni wazi.

Kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo

Padre  Bogati,  alisisitiza kuwa, “Tunakataa aina zote za vurugu, na tunafanya kazi kwa maendeleo ya amani ya jamii, tukiwa na matumaini katika serikali inayoweza kupambana na rushwa, moja ya vidonda vikubwa zaidi vya nchi.” Wakati huo huo, Nepal iliheshimu siku ya kitaifa ya maombolezo tarehe 17 Septemba, kwa kumbukumbu ya waliopoteza maisha yao wakati wa maandamano. Vijana sabini na wawili waliuawa katika vurugu za hivi karibuni, na mamia bado wako hospitalini wakipokea matibabu.

Mandamano ya vijana Nchini Nepal
22 Septemba 2025, 17:26