Katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere mkesha kwa ajili ya amani, Gaza. Katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere mkesha kwa ajili ya amani, Gaza.  (ANSA)

Jumuiya ya Mt.Egidio na mkesha wa maombi kwa ajili ya Amani huko Gaza,Septemba 22

Mkesha wa maombi uitwao"Amani kwa Gaza,”ulioandaliwa huko Roma na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio Jumatatu,Septemba 22,katika Kanisa la Mtakatigu Maria huko Trastevere,Roma,likisaidiwa na mtandao mkubwa wa vyama vya Kikatoliki,uliowaleta mamia pamoja katika sala na kuakisi sauti za amani na dhidi ya vita zilizosikika kutoka kwa Kardinali Gualtiero Bassetti na Kardinali Pierbattista Pizzaballa.

Na Antonella Palermo- Vatican.

Mamia ya waamini walikusanyika Jumatatu jioni  tarehe 22 Septemba ili kusali kwa ajili ya Amani huko Gaza, iliyoandaliwa na Jumuiya ya Mtakatifgu Egidio na kuungwa mkono na makumi ya mashirika ya Kikatoliki. Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu Mkuu mstaafu wa Perugia-Città della Piavè, na Rais wa zamani wa Baraza la Maaskofu wa Italia, aliongoza mkesha huo, pamoja na maombi kwa ajili ya mateka, wahanga wa vita, na watoto huko Gaza, na ushuhuda kutoka kwa watu walioko ardhini, ikiwa ni pamoja na shairi la kusisimua kutoka kwa mama mmoja  kutoka Gaza.

Waamini katika mkesha Septemba 22 kuomba amani
Waamini katika mkesha Septemba 22 kuomba amani
Kardinali Bassetti
Kardinali Bassetti   (ANSA)

Kardinali Bassetti: Vita vinaweza na lazima vikomeshwe

"Vita si janga kamwe. Vimechaguliwa, linatakwa. Na vinaweza na lazima kusimamishwa."Alisema, “Kila ukiukwaji wa haki za binadamu ni matokeo ya maamuzi maalum. Vita sio hatima, ni chaguo. Na lazima tuchague tofauti."Akimnukuu Hayati Baba Mtakatifu Francisko na Mwanafalsafa Martin Buber, Kardinali Bassetti alisisitiza mazungumzo na utu wa binadamu, akiwataka waamini kamwe wasisaliti ubinadamu wao wa pamoja.

Kardinali Pizzaballa akizungumza
Kardinali Pizzaballa akizungumza   (ANSA)

Kardinali Pizzaballa: Vurugu huchochea mzunguko mbaya

Jioni hiyo pia ilisikika  sauti ya Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Kardinali Pierbattista Pizzaballa, aliyejiunga kupitia ujumbe wa video kutoka Nchi Takatifu, ambamo alibainisha "tumevunjika moyo" na kwamba "katika miaka 35, sijawahi kuona wakati wa giza." Kardinali Pizzaballa aliona kwamba ingawa "tumeacha nafasi kwa watu wenye msimamo mkali wa pande zote mbili," "bado ninaamini watu wengi wapole wa moyo, watu wanaofanya kazi kimya kimya kwa ajili ya haki na amani." Katika hisia hii, alitoa wito kwa ukweli na haki kwa upendo kwa wote, akionya kwamba vurugu huchochea chuki zaidi katika mzunguko mbaya. Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu hasa alikazia kusema kuwa, “Lugha ya nguvu inaposhindwa, muundo huu wote wa jeuri unapoporomoka, ni lazima tuwe tayari, kuleta nguvu za upole ili wote warithi, kwa uzuri na upendo, nchi ambayo Mungu ametupa.”

Waamini katika mkesha
Waamini katika mkesha   (ANSA)
Waamini katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere
Waamini katika Kanisa la Bikira Maria huko Trastevere   (ANSA)
22 Septemba 2025, 22:30