Hali inaendelea vile vile na vipimo vya damu vinaonesha kuboreka kidogo
Vatican News
"Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu zinaonekana kuwa zile zile. Vipimo vya damu, vilivyotathminiwa na wafanyakazi wa matibabu, vinaonesha uboreshaji kidogo, hasa katika uvimbe unaochochewa na madawa. Baada ya kifungua kinywa alisoma baadhi ya magazeti na kisha kujishughulisha na shughuli za kazi na washirika wake wa karibu. Kabla ya chakula cha mchana alipokea Ekaristi. Mchana alipata ugeni kutoka kwa Waziri Mkuu wa Italia Bi Giorgia Meloni, ambaye alizungumza naye kwa faragha kwa dakika 20".
Hayo yameripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican katika taarifa iliyotolewa jioni ya leo, tarehe 19 Februari 2025, ili kusasisha hali ya afya ya Baba Mtakatifu Francisko, ambaye amelazwa hospitalini tangu tarehe 14 Februari 2025.
